Uwekezaji huu wa Diamond Platnumz, kamwe hatafulia kama wengi wanavyodhani

Uwekezaji huu wa Diamond Platnumz, kamwe hatafulia kama wengi wanavyodhani

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Wakuu habari,

Mimi ni shabiki mnazi wa Diamond Platnumz kwa muda mrefu.

Nimekuwa nikosoma sehemu mitandao mbalimbali hata humu JF watu wakisema kuwa Diamond siku zake zinahesabika kushuka kimuziki na mkwanja. Wanadai hajui kuimba na nyimbo zake ni Big G. Kuhusu nidhamu ya pesa wanadai ana matumizi makubwa sana halafu ana msururu wa wategemezi usiopungua 50.

Pamoja na hayo kijana ameonesha kupiga hatua kubwa sana kuzidi wasanii wote nchini. Ndani ya muda mfupi usiozidi miaka minne kijana ameweza kujiwekea vitega uchumi ambavyo mpaka anakufa vitakuwa vinamuingizia kipato.
- Ana mikataba kibao na makampuni
- Zari, Tiffah, Mama Mond wote ni brand wana mikataba
- Anamiliki nyumba za kutosha
- Anamiliki studio ya Muziki
- Anamiliki studio ya kupiga picha
- Soon kujiunga na lebo kubwa ya muziki inayomilikiwa na msanii mkubwa Marekani
- Ana wasanii (Wasafi) wanaoingiza pesa nzuri tu
- Ana mke/hawara mwenye akili
- Ana mashabiki lukuki
- Anapata show za kutosha na msanii anayelipwa pesa nyingi
- Vitega uchumi vingine ambavyo sivijui

Diamond sasa kila wimbo anaogusa ni moto huko youtube na ameweza kuvunja rekodi hadi alizoweka mwenyewe. Mfano...

- Salome unafanya vizuri duniani

- Zigo remix, huu bado ni moto na gumzo dunia (Una views za kutosha Youtube), Nani anajua AY katoa wimbo mpya unaitwa EL Chapo? Wachache sana maana Mond hajatia maguu.

- Waache waoane , Chege hakuwahi kufikisha views hata 700k youtube lakini uwepo wa Mond,Chege kavunja rekodi ndani ya wiki.

- Make me Sing, A.K.A alisherekea kuvunja rekodi SA ndani ya wiki, hakuwahi kabla

- Sweet Love, Akothee kila siku anamshukuru Diamond kumvunjisha rekodi na kupelekea kujulikana Afrika

- Watora Mari, Jah Prayzah kaporomosha bonge la party kwa mara ya kwanza kufikisha views 1m tokea aanze kuimba.

- Bado, nani asoujua huu wimbo. Uwepo wa Diamond ulisababisha kuwa wimbo wa taifa na Harmo kuvunja rekodi ya views etc etc

Kijana pia ana moyo wa kurudisha kwa jamii wahitaji.Katoa madawati kwa wanafunzi, katoa 20m kwa GSM wengine wakajikweza kuongeza 1m ili wamzidi.

Ndani ya wiki mbili kanunua nyumba mbili, Tabata na SA
13.jpeg

11.jpeg

Kijana kama huyu sio wa kumbeza, anajua anachokifanya.

Poleni kwa kuwachosha.
 
Ungekuwa shabiki namba moja wa chama chetu CCM ndiyo nigeona kuna ukweli kwani CCM itaendelea kutawala siku zote na haitakuja kufirisika kamwe maana ni tajiri wa viongozi na uongozi. Ila kwa huyu kijana mwenzetu hali inaweza kubadilika, kumbuka kama akina Jackson etc waliishiwa sembuse yeye. Kumbuka pia umaarufu + uwekezaji==Ghararama hupanda, na ikitokea mirija imekata basi kila kitu huporomoka. Kikubwa kijana anatakiwa awe na watalaamu wa uchumi na mahesabu ili wamsharui vizuri asiwekeze tu ili mradi kaambiwa na mganga wa kienyeji.
 
Kwanza kuwa na heshima kwa Mr Nice. Huwezi kuweka andiko bila wa kumtolea mfano? Kama Mr Nice angewekeza, pengine huyo unae muona asingejua lolote kuhusu kuwekeza. Pili hivyo vitu vyote unavyo vitaja hatujaona evidance yoyote kama ni vyake., weka evidance hata hati ya mahuziano basi ili tukuamini, msitufanye watoto zenu kila mkijamba tuvumilie.
 
Ungekuwa shabiki namba moja wa chama chetu CCM ndiyo nigeona kuna ukweli kwani CCM itaendelea kutawala siku zote na haitakuja kufirisika kamwe maana ni tajiri wa viongozi na uongozi. Ila kwa huyu kijana mwenzetu hali inaweza kubadilika, kumbuka kama akina Jackson etc waliishiwa sembuse yeye. Kumbuka pia umaarufu + uwekezaji==Ghararama hupanda, na ikitokea mirija imekata basi kila kitu huporomoka. Kikubwa kijana anatakiwa awe na watalaamu wa uchumi na mahesabu ili wamsharui vizuri asiwekeze tu ili mradi kaambiwa na mganga wa kienyeji.
Acha roho mbaya, umesahau kuwa yeye ndie aliyewapigia kampeni .....?
 
A

Acha ungedere, umesahau kuwa yeye ndie aliyewapigia kampeni .....?

Shubaaaa miti
wewe nadhani utakuwa na ule ugonjwa wa lisu wa kupungukiwa na akili au akili kuhamia kwenye makalio yako. Mimi sijamponda mond, nilichoshauri na kusema ni kuwa ma celebs wengi pamoja na uwekezaji huwa wanagharama kubwa sana ya maisha. Hivyo vyanzo vyao vikiyumba kidogo tu huwa wanaporomoka haraka na mpaka chini. Soma story ya Dr Dre, au fifty cent.
 
Hawezi kufilisika kutokana na mipango yake siyo kwa sababu ya idadi ya nyumba. Zamani watu wengi walikuwa wanaamini kuwa kila nyumba ni asset lakini kuna nyumba ambazo ni liabilities.

Nyumba inakuwa asset pale tu inapokuingizia pesa kwa kuwa nayo, lakini kama inachukua pesa haiwi asset tena. Jambo la muhimu ni kuwa nyumba alizonazo zinamwingizia nini.
 
wewe nadhani utakuwa na ule ugonjwa wa lisu wa kupungukiwa na akili au akili kuhamia kwenye makalio yako. Mimi sijamponda mond, nilichoshauri na kusema ni kuwa ma celebs wengi pamoja na uwekezaji huwa wanagharama kubwa sana ya maisha. Hivyo vyanzo vyao vikiyumba kidogo tu huwa wanaporomoka haraka na mpaka chini. Soma story ya Dr Dre, au fifty cent.
kwenye makalio yako....yasiyokuwa na muonekano... yamelegea kama ugali muhogo..... Ngedere wewe
 
wewe nadhani utakuwa na ule ugonjwa wa lisu wa kupungukiwa na akili au akili kuhamia kwenye makalio yako. Mimi sijamponda mond, nilichoshauri na kusema ni kuwa ma celebs wengi pamoja na uwekezaji huwa wanagharama kubwa sana ya maisha. Hivyo vyanzo vyao vikiyumba kidogo tu huwa wanaporomoka haraka na mpaka chini. Soma story ya Dr Dre, au fifty cent.
Una shauri wewe kama nani....!? Unajipendekeza pendekeza tu
 
Back
Top Bottom