Uwekezaji: PPF yaendeleza eneo la ekari 5 jijini Dar

Uwekezaji: PPF yaendeleza eneo la ekari 5 jijini Dar

Kiwanja ni kikubwa sana zamani kulikuwa na kampuni ya kufyatua matofali pale... Kwa eneo lile dola milion 8 siwezi kubisha
mkuu mark my word gharama ya hiyo kiwanja haiwez kuzid 1m usd tatizo ni hiyo chain ya kuanzia mwenye kiwanja ,dalali, mkurugenzi , nadhani hata katibu mkuu wa fedha anahusika hapo
haya mashirika ndio maana yanafilisika
na ndio maana rais alisema yale madeni yasilipwe kwanza yahakikiwe
 
Kiwanja ni kikubwa sana zamani kulikuwa na kampuni ya kufyatua matofali pale... Kwa eneo lile dola milion 8 siwezi kubisha
Alafu wenye viwanja na nyumba za kawaida ukanda ule watakuja piga hela sana, maana ule ukanda utakuja kuwa wa magorofa mpaka huku TCRA.
 
Nadhani tuambiwe hilo eneo hapo lina ukubwa gani?

Kwa Billioni 16 nategemea kwa bei ya kifisadi kabisa kiwanja kina ukubwa wa hekta tatu hivi. Kinyume na hapo ni wizi wa wazi kabisa.
 
Alafu wenye viwanja na nyumba za kawaida ukanda ule watakuja piga hela sana, maana ule ukanda utakuja kuwa wa magorofa mpaka huku TCRA.
Sana si umeona pale jirani landmark anajenga showroom ya maduka ya kisasa... Within 10yrs hili eneo litakuwa juu sana
 
Sana si umeona pale jirani landmark anajenga showroom ya maduka ya kisasa... Within 10yrs hili eneo litakuwa juu sana
Vipi wewe umepanga hapo au ndo wale wanaovuta pumzi waje uza nyumba/ viwanja vyao mabilioni ya hela?
 
kama 8m usd kwa exchange rate ya sasa
2200x8000000=17b
nadhani unaweza kuinunua stand ya ubungo yote na change inabaki
waache kuchezea hela zetu ndio maana hiyo mifuko inafilisika
 
Aliyeuyza kiwanja anapaswa kuchunguzwa na kulipa kodi
 
Ndugu zangu, hii si siri ila nimeamua tu kuwanong'oneza tu, sio tetesi ni taarifa za kweli na zinazoweza kuthibitishwa kwa nyaraka, vielelezo pia ushahidi.. Plz naomba msininukuu vibaya.. sijasema hili ni jipu, tezi, busha wala uvimbe.. hamkawii kunisingizia..

Ni taarifa zenye mapana ya ukweli unaoweza kuthibitishwa kuwa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya umma japo kwa sasa wahusika na kuhifadhi na kulipa pensheni kwa sekta binafsi na zisizo rasmi.. Katika mipango mikakati ya kuwekeza michango ya wanachama wake kupitia sekta ya ujenzi wa nyumba, majumba n.k hivi karibuni mfuko umenunua kiwanja pembezoni mwa barabara ya Sam Nujoma {Mwenge-Ubungo} toka kwa kampuni binafsi kwa bei ya Dola za Kimarekani Milioni 8 sawa na zaidi ya bilioni 16.

Kwa ufahamu wangu mdogo sana, hizi ni pesa nyingi sana kutumika kununua kiwanja pakee katika maeneo husika.. Yamkini huu ni muendelezo wa maamuzi yasio na weredi, uzalendo, harufu ya ubadhirifu, kujinufaisha na tuhuma za wizi, ufisadi pia matumizi mabaya ya madaraka toka kwa viongozi/wafanyakazi/watumishi wanaopewa dhamana husika.

Kumekuwepo na kawaida yenye mizizi kwa wafanya manunuzi toka taasisi za Serikali {Mashirika ya Umma,Wizara na Wakala} kuweka cha juu mbali na asilimia 10 ambayo wamekuwa wakipata kwa lazima toka kwa wazabuni wenye kufanya kandarasi ktk taasisi husika.. Mzabuni asietoa asilimia 10 huyo amekuwa akikanwa, nyanyapaliwa, tengwa na zabuni zake kutupwa ama malipo yake kucheweleshwa kwa makusudi kabisa.

Kwa hili la PPF yamkini na taasisi zingine zenye kufanana na hii, Michakato ya manunuzi ya viwanja vya uwekezaji imekuwa ikihusisha idara zaidi ya moja katika kufikia maamuzi kama Miradi /Uwekezaji,Manunuzi {PMU}, Masoko {Marketing}, Sheria, Uhasibu na Utawala..

Hivyo basi kwa kuwa roho ya urafi, tamaa, wizi, ubadhirifu imekuwa mtambuka kwa kila mmoja kwa nafasi yake kushiriki {Mbuzi hula majani kwa urefu wa kamba yake} vivyo hivyo mapana ya chajuu huwa makubwa zaidi ili kukonga nyoyo za washiriki.

Hili laweza kuthibitishwa na ukweli wa mali wanazomiriki wahusika wakuu wa hii michakato kutofautiana mno na uhalisia wa vipato vyao halali na pia mapato yao ,vitega uchumi vyao kuongezeka mara tu malipo yanapofanywa kwenda kwa wazabuni walio katika miradi dili .

Uchunguzi mahsusi waweza baini taarifa za kina kwenye miradi yote mikubwa inayohusisha matumizi ya mabilioni ya kodi, michango, misaada, ruzuku kama Ujenzi wa Bomba la gesi, Ununuzi wa Vivuko, TPA, RITA, TCRA, UTT, NSSF, PSPF, SUMATRA, DART, TANESCO, TFDA, MSD, VETA, Gaming Board, NMB, EPZA, TANROADS, TBA, REA, WMA, TANAPA, NFRA, MNH, TPF, TPDC, TPDEF, UDSM, DIT, TAMISEMI {Halmashauri, DAWASA, Mamlaka za maji, Wizarani...n.k.

Uchunguzi uende mbele zaidi hata kuwabana wafanyabiashara wasio na maadiri wanaofanya biashara na serikari..

Mfano ktk hili la PPF je baada ya malipo nani na nani waligawiwa,walitumiwa fedha,walilipwa,walitafunishwa mishkaki ama kuyweshwa mvinyo wa ushindi...yale ya Mkombozi na Tegeta Escrow yaweza jitokeza ama la ya viroba, lumbesa, Visandarusi {Stanbic}

Nakiri mimi si mtakatifu, Si msafi, Si Mzalendo wa kutukuza... Tanzania inapaswa kufanyiwa kupasuliwa na kutakaswa kweli kweli... Mwenyezi Mungu awatie nguvu na maarifa viongozi wetu wenye kiu na nia ya dhati kurejesha heshima, utu, usawa na heshima kwa wote.

Hapo mahali hakuna uwanja wa thamani hiyo.
 
Ngoja wanaokijua hicho kiwanja waje watueleze vizuri, huwezi jua labda ni eneo lote linalopakana na barabara ya Sam Nojuma kutoka pale njia ya kwenda TRA-Mwenge mpaka kwenye taa za njia ya kuelekea Sinza makaburini!
 
Sana si umeona pale jirani landmark anajenga showroom ya maduka ya kisasa... Within 10yrs hili eneo litakuwa juu sana
halafu nyie acheni kutetea wezi mkishaa kula MLUNGULA mnakimbilia huku kuja kupima upepo watu wanasema nin. ilo eno limeshaakuwa juu sikunyingi tu hata bila kuwepo hiyo landamark maduka ya kisasa kama unavyodai na uwekezaji wa namna hiyo ni wa kijinga ni sawa na wale wa mahotel wanaotegemea wafanye biashara na serikali kwenye kumbi zao za mahotel lakin kutoa 16bilion kwa ajili ya kununua kiwa kiasichozidi 4000sqm ni matumizi mabaya ya pesa za umma nadhani hatua sahihi zitachukuliwa na DR JPM
 
Ngoja wanaokijua hicho kiwanja waje watueleze vizuri, huwezi jua labda ni eneo lote linalopakana na barabara ya Sam Nojuma kutoka pale njia ya kwenda TRA-Mwenge mpaka kwenye taa za njia ya kuelekea Sinza makaburini!
Wee unaongelea kiwanja gani?? Hiki kipp pale nafikiri kituo cha basi kivulini kwa wale wa kina sisi wa daladala, utaona kimezungusjiwa uzio na nondo zimetanda na mawinch yako juu.
 
hii kampuni na ccm ni dugu moja maana hata kipindi inajenga barabara ya tegeta jpm aliichimba mkwara lakini mwisho wa siku kanywea
 
dah umemaliza mkuu, hutowaona wale waliokuwa wakimkandia dr dau humu, wanachungulia tu
Tupeni ushahidi ya dau ushahidi upo ni audit report ya 2014/14 sasa mkianza kuchokonoa tutaweka na Picha za nyumba anazomiliki TZ na london
 
Hawa jamaa hawana uchungu na hela maana wanazikusanya bila jasho na huku mfanyakazi anayekatwa anasitaafu akiwa hana hata kibanda cha kulala, amekatwa makato makubwa na kodi zisizopimika, inauma sana!
 
Wee unaongelea kiwanja gani?? Hiki kipp pale nafikiri kituo cha basi kivulini kwa wale wa kina sisi wa daladala, utaona kimezungusjiwa uzio na nondo zimetanda na mawinch yako juu.
Kiwanja chochote maeneo hayo japo sipafahamu vizuri hakiwezi kufikia bei hiyo, labda kama UDSM wameamua kukumilikisha nusu ya eneo lao lote. Ndio maana nikasema labda kama ni kutoka kwenye traffic light za kwenda Sinza makaburini mpaka round about ya Mwenge njia panda ya kwenda TRA/NMB.
Na kumbuka hii ni pesa ya shirika la umma, labda kama wamegundua kiwanja hicho kina deposit ya almasi au gemstones.
 
Back
Top Bottom