Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
UWEKEZAJI WA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KATIKA KILIMO UNA DHAMIRA KUZALISHA AJIRA KWA VIJANA-NDG KAWAIDA
Mwenyekiti Mohammed Ali Kawaida (MCC) ameadhimisha Sikukuu ya Miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kutembelea na kukagua maendeleo ya programu ya Boresha Kesho Iliyo Bora (BBT) leo tarehe 26.04.2023 kituo cha Atamizi cha Hort Tengeru Jijini Arusha.
Akiwa katika Ziara hiyo Mwenyekiti Kawaida amewaambia Vijana juu ya dhamira njema ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuunga mkono sekta ya Kilimo ambayo ni nyenzo muhimu kwa vijana katika kujikwamua na umasikini.
Aidha, Mwenyekiti Kawaida amesema ili kudhihirisha hilo Mhe Rais ameweza kununua Pikipiki kwa Maofisa Ugani, Vipima Afya ya udongo, uaandaaji wa Mashamba makubwa(Block Farm), Ujenzi wa Miundombinu ya Umwagiliaji, sambamba na hilo amenunua ndege ya mizigo kwa ajili ya kurahisisha usafiri wa mizigo ambayo itawasaidia wakulima ambao wanasafirisha mazao yao kwenda nje ya nchi.
Kutokana na changamoto ya vijana kukosa mitaji ya kujikwamua katika Kilimo na sekta ya uchumi Serikali ya awamu ya Sita imeamua kugharamia mafunzo, Chakula, na Malazi bure kwa vijana wa kitanzania ili wafikie lengo la kuwa mabilionea kupitia Kilimo nchini.
Imetolewa na:
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM-Taifa.