Uwekezaji wa UTT liquid Fund faida yake mbona ni tofauti na uhalisia wanaousema

Gotze Giyani

Senior Member
Joined
Feb 28, 2022
Posts
127
Reaction score
194
Habari wadau poleni na majukumu ya taifa lisiloeleweka kama sio lenye jana janja nyingi na yote ni kutokana na watanzania wengi kutokujali.

Tuachane na hayo niliwai kusoma uzi mmoja huku jamii forums nikavutiwa nao nikajitaidi kufuatilia na kuuelewa zaidi basi nikaamua kuwekeza UTT amis mfuko wa Liquid fund ni miezi kama 9 hivi na wanasema kwa mwezi ni asilimia mpaka 1 ila mbona ni tofauti mfano unaweza kuwa na milioni 5 kwa mwezi faidi hapo ilitakiwa iwe 50000 kuendelea ila unaweza ishia 45000 hivi wana calculate vipi wakati thamani ya kipande aijashuka.

Kama ujui kaa kimya sitaki matusi na ujuaji wa kijinga wadau mnaojua kuhusu huu mfuko na wakaribisha mnieleweshe maana naona kama ni uwekezaji kichaa hata kama ela ni nyingi faida ni ndogo.
 
Habari wadau poleni na majukumu ya taifa lisiloeleweka kama sio lenye jana janja nyingi na yote ni kutokana na watanzania wengi kutokujal...
Hiyo asilimia moja huwa wanaipata kwa kujumuisha faida iliyopatikana kwa kipindi cha mwaka mzima gawanya kwa 12. Kwa hiyo ukifuatilia kila mwezi utaona kuna upishano. Mfano mwezi wa nane faida ilikua 0.9731% na mwezi Septemba mpaka tarehe 29/09/2022 faida ni 1.1636%
 
Hiyo 1% ni kwa mwaka mzima. Km una iyo 5mln utapata 5mln×1%=500k kwa mwaka mzima, ina maana kwa wastani kwa kila mwezi utapata 500k÷12=41,666.666666667 sawa na 1,388.8888888889 kwa kila siku. inasaidia kutunza thamani ya pesa yako tofauti km ungeweka iyo pesa benki.
 
Benki ina interest kubwa, ukiweka savings. Pia jaribu benki ya posta. hao matapeli tu.
 
Habari wadau poleni na majukumu ya taifa lisiloeleweka kama sio lenye jana janja nyingi na yote ni kutokana na watanzania wengi kutokujali...
Mbona mifuko ni mingi asilimia 1 ya uhakika ni mfuko wa bond fund sahihi zaid
 
Hizo faida au hasara zinatokana na nini??

#MaendeleoHayanaChama
 
5m x 1% = 500k? ??? Hesabu za wapi hizi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…