Uwelewa wa Wayahudu na wakristo kuhusu mtume Muhammad na kitabu Cha Quran

Uwelewa wa Wayahudu na wakristo kuhusu mtume Muhammad na kitabu Cha Quran

Wazolee

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2018
Posts
4,177
Reaction score
4,887
A) Wayahudu
Wakati mtume Muhammad anaanza kupokea ufunuo kutoka Kwa Allah kipindi hicho Saudi Arabia kulikuwa na Wayahudu wengi sana
Wale waarabu ambao wanampinga mtume Muhammad ikabidi waende Kwa wayahudu kupata ushauri kuwa wafanye nini Ili kujua kuwa Muhammad ni mtume kweli au ni muongo

Wayahudu wakawaambia nendeni mkamuulize haya maswali 3 kama atajibu basi kweli ni mtume wa Mungu

1) kuhusu watu wa pangoni

2) kuhusu mfalume aliyetembea mashariki Hadi magharibi ya Dunia (Dhulkalinainy)

3) kuhusu roho

Haya maswali yote Allah akawajibu Kwa ufasaha kabisa

Kuhusu watu wa pangoni

Quran 18:10
Vijana hao walipo kimbilia kwenye pango walisema: Mola wetu Mlezi! Tupe rehema itokayo kwako, na tutengezee uwongofu katika jambo letu.
Quran 18:11
Tukayaziba masikio yao kuwalaza humo pangoni kwa muda wa miaka kadhaa wa kadhaa.
Quran 18:18
Nawe utawadhania wamacho, na hali wamelala. Nasi tunawageuza kulia na kushoto. Na mbwa wao amenyoosha miguu yake ya mbele kizingitini. Kama ungeli watokea hapana shaka ungeli geuka kuwakimbia, nawe umejaa khofu.
Quran 18:25
Na walikaa katika pango lao miaka mia tatu, na wakazidisha tisa.

Hapo Wayahudu wakasalimu amri wakasema kweli wewe ni mtume wa Mungu likini sisi hatukufati Kwa sababu wewe sio myahudi mwenzetu

Kwahiyo wayahudu wanajua kabisa kuwa Muhammad ni mtume wa Mungu na Quran ni Maneno ya Mungu ila ni jeuri Yao tu ndio inayowafanya wasifuate mafundisho ya mtume Muhammad

B) Wakristo
Wakristo Kwa maana ya wafuasi wa Yesu Wana generation 2
Kuna wakristo waliyokuwa wanafuata mafundisho ya Yesu mfano Stefano waliamini kuwa Yesu ni nabii, Mungu ni Mmoja na Ibada zao walikuwa wanafanya ndani ya Sinagogi hawa ni sawa na kusema waislam wa zamani

Kuna wakristo wa uzao wa Paulo hawa ndio waliyopo Sasa hapa Duniani
Hawa hawajui kuwa Muhammad ni mtume wa Mungu na Quran ni Maneno ya Mungu na hawajui watumie vipimo gani Ili kujua kuwa kweli Muhammad ni mtume wa Mungu au sio mtume wa Mungu kama walivyo Fanya wenzao wayahudu maana hao Wazungu waliyowaletea hiyo dini wamewakologa sana

Kwa Sasa tunaweka mada za wenye uwelewa na ufahamu wa juu
 
Back
Top Bottom