Wahenga walisema miamba inapopigana basi nyasi ndio zinaumia. Kama ulikuwa haujuwi basi leo ngoja nikujuze.
Kwa tathimini iliofanyika baada ya Rais wa Marekani kujitoa kwenye WHO macho ya watafiti yamegeukia Africa ambao sisi niwanufaika wakubwa wa mzigo anachangia WHO. USA ana contribute mpaka USD 534m kwa mwaka. Mfano mwaka 2019 USA walichangia USD 419m kwenye fuko la WHO jambo ambalo hakuna taifa linachangia kiasi hiko.
Tanzania nimoja wa wanufaika wa michango anayotoa USA ktk fuko kuu la WHO na moja ya manufaa ni vidonge vya ARV. Tusione vile vidonge vinatengenezwa nakugaiwa bure ila thamani yake ni mpaka tshs 713k kwa kila mgonjwa na kwa tanzania tuna zaid ya wagonjwa 2.15k wakati kila mwaka kuna wastani wa wagonjwa wapya 79.9k.
Serikali zetu zimejiandaaje kutoa dawa bure bila support ya fuko la wakubwa? Hili ni swal ambalo mabunge na Serikali za Dunia ya tatu na marais lazima wakae chini nakutafuta njia mbadala. Las hivyo watu wetu watakufa na maambukiz kuongezeka kwa kiwango cha juu sana.