Uwepo wa maisha nje ya sayari ya Dunia, Utathibitisha hakuna Mungu

Kwa nini kitabu cha Mungu kihitaji habari ya msingi wa kutafsiriwa?

Kwa nini Mungu hakufanya kitabu cha Mungu kila mtu azaliwe nacho kichwani kisihitaji kutafsiriwa wala kubebwa, mtu awe nacho kichwani muda wote?

Teknolojia hiyo ilimshinda Allah au vipi?
 
Nemesema utaelewa sababu una majibu ya hiyo aya ya saba uliyo inukuu.
Unajuaje kwamba majibu hayo nitayaelewa?

Unajuaje kwamba majibu hayo nitayakubali kabla sijayaona?

Unajuaje kwamba unavyofikiri wewe ndivyo ninavyofikiri mimi?

Ndio usomi wako huo? Wa ku assume tu kila mtu kama wewe?
 
Kaka nilipokwambia soma mpaka aya ya 20 nilimaanisha mzee.Ukisoma mpaka huko utapata majibu ya vizibo.

Si kweli kwamba kuielewa Qur'an mpaka utumie uchawi bila shaka hujui nini maana ya uchawi.

Halafu hakuna ugumu wowote katika kusoma Qur'an.Pia unaposema kwanini Allah asingekishusha kwa watoto wanao zaliwa katika lugha zao.Hii ni hoja ya kitoto isiyo na mfano na hoja iliyodhidi yako.

Qur'an ilishushwa au imeshushwa kwa lugha ya kiarabu hii ni kwa sababu mtume alikuwa ni muarabu na watu wake waweze kuelewa ujumbe.

Lakini Qur'an ni kitabu cha muongozo na kwa ajili ya watu wote na ikabidi watu wajifunze lugha ya kiarabu ili kuwafikishia na wenzi wao katika lugha zao.

Ndio maana leo hii au wewe umenukuu tarjama ya kiingereza kutoka katika kiarabu.

Halafu Qur'an haina utata,ndio maana al imaam ash-Shawkani anasema "Maneno ya Allah hayapingani basi ukiona yanapingana basi ituhumu akili yako yawezekana ukawa na elimu ndogo kuhusu maneno hayo."

Sasa hata hizi kinzani ulizozinukuu ni hoja za kitoto ambazo zimekusanywa na watu baada ya kukisoma kitabu hiki nusu nusu kama usomavyo wewe.Na hii ni tabia ya wengi wenye kuhujumu uislamu na waislamu.

Mathalani wewe ungeendelea kusoma mpaka pale nilipokwambia bila shaka ungepata majibu.
 
Unajuaje kwamba majibu hayo nitayaelewa?

Unajuaje kwamba majibu hayo nitayakubali kabla sijayaona?

Unajuaje kwamba unavyofikiri wewe ndivyo ninavyofikiri mimi?

Ndio usomi wako huo? Wa ku assume tu kila mtu kama wewe?
Kaka soma mpaka aya 20.Usiogope
 
Yako wapi, sijayaona, nioneshe.Mstari gani?
Kaka umenukuu aya katika Surat al Baqara aya ya kwanza mpaka ya 8 na aya ya saba ukawa umeikoleza kwa wino mweusi.Kwa maana kiini cha swali lako kipo katika aya ya saba.

Sasa mimi nimekwambia endelea kusoma mpaka aya ya 20 utapata jibu la swali lako.
 
Allah hashindwi na chochote na chochote na ndio maana akajaalia baadhi ya viumbe kuwepo bila mama wala baba na vingine kuwepo bila baba na ndivyo hivyo hivyo aliamua kutuumba tukiwa hatujui chochote na akajaalia elimu na kujifunza ndio msingi wa kila jambo kwa hiyo huo ni utaratibu ambao amejiwekea Allah.

Na akajaalia kuumba kila kitu katika pea(pair) wala haulizwi kwalo na angetaka angefanya usiku peke take bila mchana na amefanya kuwepo usiku na mchana ili waja wake tuweze kushibiti idadi ya miaka na kudhibiti mahesabu na kwa mchana akajaalia kuwa maisha na usiku kupumzika.

Na akajaalia kuwapo na mataifa mbali mbali na makabila mbali mbali ili tufahamiane lakini angetaka iwe kinyume chake ingekuwa.

Kwahiyo Allah hashindwi kitu.
 
Yako wapi, sijayaona, nioneshe.Mstari gani?
Msingi wa kutafsiri lazima uwepo sababu hiyo ni elimu.Na lazima kuhakikisha tafsiri haipotoshwi ndio maana Qur'an inajitafsiri yenyewe na inatafsiriwa na Mtume wetu alayhi salaam.
 
Halafu humu JF kuna freemasons nawapagani siku hizi comments zao zakumpinga mungu tu daily
 
Kwa nini Allah kabagua kawashushia waarabu mtume hajawashushia mataifa mengine mtume?

Kwa nini Alah mjuzi wa yote ajulikane kwa watu aliowaumba mwenyewe kwa kupitia vitabu, vitabu vyenye utata mwingi sana?

Kwa nini Allah hajaliweka neon lake kwenye kichwa cha kila mtu kwa lugha yake kusiwe na haja ya kutembea na Quran?

Hizo hoja za kitoto mbona hujazijibu?

Hoja za kitoto ni rahisi sana kuzijibu.

Unasemaje hoja za kitoto wakati hujazijibu?

Nimekwambia nimesoma mpaka aya ya 20 sijaona jibu, unaweza kunionesha jibu liko wapi?
 
Nimesoma sijapata jibu.

Unaweza kunionesha jibu liko wapi?
 
Unajua kwamba hujajibu swali uliloulizwa na ulilojibu si uliloulizwa?

Nakuuliza kwa nini Allah hajatuumba tukiwa na hiyo Quran kichwani tangu tunazaliwa, kila mtu kwa lugha yake, kusiwe na utata wa tafsiri wala kuulizana kama hizi ni habari za Mungu?

Unaniambia Allah hashindwi chochote.

Kwani nilikuuliza kama anashindwa chochote?

Mbona hujibu ulichoulizwa na unachojibu ni tofauti na ulichoulizwa?
 
Msingi wa kutafsiri lazima uwepo sababu hiyo ni elimu.Na lazima kuhakikisha tafsiri haipotoshwi ndio maana Qur'an inajitafsiri yenyewe na inatafsiriwa na Mtume wetu alayhi salaam.
Hujajibu ulichoulizwa, unachojibu hujaulizwa.

Jibu liko wapi?
 
Hakuna hoja yako ambayo sijaijibu mzee.Soma vizuri kila kitu kipo.
 
Hakuna hoja yako ambayo sijaijibu mzee.Soma vizuri kila kitu kipo.
Unajua kwamba hujajibu swali uliloulizwa na ulilojibu si uliloulizwa?

Nakuuliza kwa nini Allah hajatuumba tukiwa na hiyo Quran kichwani tangu tunazaliwa, kila mtu kwa lugha yake, kusiwe na utata wa tafsiri wala kuulizana kama hizi ni habari za Mungu?

Unaniambia Allah hashindwi chochote.

Kwani nilikuuliza kama anashindwa chochote?

Mbona hujibu ulichoulizwa na unachojibu ni tofauti na ulichoulizwa?

Unaweza kunionesha umejibu hoja gani? Unaweza kunionesha umeijibu wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…