Uwepo wa Mungu unadhihirika kwa alama zake na viumbe vyake

Mimi siwezi kuhoji ukuu wake, mwanadamu analimiti ya kujua mambo ndio maana hata mzazi wako hawezi kukushirikisha kwa kila kitu. Mambo ya kiMungu ni magumu kuyajua kiroho omba neema uwe karibu naye huenda yeye mwenyewe akakufunulia ukawa mshuhuda wetu.
Niseme tu kwamba hata akikugunulia ukaja kuwaambia wengine huenda baadhi hawataamini na wataanza kuhoji kama unavyohoji wewe......
Kuna baadhi ya watu Mungu anapendezwa nao wanapata neema (upendeleo) anawafunulia mambo makubwa sana ndio maana unakuta mtu anagundua kitu flani ambacho hakikuwahi kuwepo kabla.

Mungu yupo na ataendelea kuwepo na nyakati zake zitafika hata yule ambaye haamini atamuamini.
Kwa nini Mungu kaumba ulimwengu ambao unaweza kuwa na Shetani na uovu, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao hauwezi kuwa na shetani wala uovu?
 
Mimi siwezi kuhoji ukuu wake, mwanadamu analimiti ya kujua mambo ndio maana hata mzazi wako hawezi kukushirikisha kwa kila kitu. Mambo ya kiMungu ni magumu kuyajua kiroho omba neema uwe karibu naye huenda yeye mwenyewe akakufunulia ukawa mshuhuda wetu.
Niseme tu kwamba hata akikugunulia ukaja kuwaambia wengine huenda baadhi hawataamini na wataanza kuhoji kama unavyohoji wewe......
Kuna baadhi ya watu Mungu anapendezwa nao wanapata neema (upendeleo) anawafunulia mambo makubwa sana ndio maana unakuta mtu anagundua kitu flani ambacho hakikuwahi kuwepo kabla.

Mungu yupo na ataendelea kuwepo na nyakati zake zitafika hata yule ambaye haamini atamuamini.
Hujathibitisha Mungu yupo, unaongea mahubiri ya imani tu.

Nilishakwambia siko interested na mazungumzo ya imani tu.
 
Mungu mwenye upendo wote , anajua maisha ya kila kitu , anaepanga kila kitu kabla hakijatokea , anaechoma watu baada ya yeye kupanga kila kitu , hayupo.

Udhibitisho wa yeye kutokuwepo upo dhahiri bila kuitaji mahubiri, bali ushawishi wa kuwa yupo unahitaji mahubiri yenye vitisho na ahadi nyingi.
Sasa ndio ututhibitishie hilo.

Nipo hapa.
 
Kwamba ukwel wa Mungu ni upi , ivi unafahamu hata wa dini yako pale anapofanya imagination ya Mungu kichwani kwake ni tofauti na wewe na mwingne?
Kwanza umeelewa nilicho kiandika ?

Ukweli wa Mungu ni kuumbwa ulimwengu. Hoja yako Iko wapi ?

Mungu hadirikiwi kwa akili wala haelezeki kwa makisio sababu akili zetu hazina uwezo huo, ndio maana huwa nastaajabu kuona mnajadili juu ya msilo lijua.
 
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na mwenye upendo wote kuumba ulimwengu ambao watu wanaweza kukosea ni contradiction.

Sasa yeye ndio ametaka iwe hivyo, ndio maana akawa muweza wa yote, hili akili yako inashindwa kuling'amua.
 
Kwa nini swali lako linakuwa "aliye...?".

Huoni kuwa swali lako linalenga kwenye jibu unalolitaka tayari? Huoni swali yako lina bias, kasumba ya kwamba kuna "aliyeumba"?

Sayansi imeshaelezea vizuri kabisa jinsi jua lilivyotokea. Na maelezo hayo hayamuhutaji Mungu.

Wewe umesoma nini kuhusu maelezo ya kisayansi kuhusu jua lilivyotokea?

Tunasoma haya mambo au tunashangaa tu na kusema hii ni kazi ya Mungu?

Mbona vitu vyote vipo mtandaoni? Tatizo ni nini, ni hiki Kiingereza?

Formation​

The Sun formed about 4.6 billion years ago in a giant, spinning cloud of gas and dust called the solar nebula. As the nebula collapsed under its own gravity, it spun faster and flattened into a disk. Most of the nebula's material was pulled toward the center to form our Sun, which accounts for 99.8% of our solar system’s mass. Much of the remaining material formed the planets and other objects that now orbit the Sun. (The rest of the leftover gas and dust was blown away by the young Sun's early solar wind.)
Inajua nn bro inahitaji imani kubwa kuamini sayansi kuliko hata kuamini katika Mungu kuhusu mswala ya uumbaji....
Maisha sijui yalianza majini(water) baabda ya big bang etc hivi unajua kwamba kwa kutumia theory za big bang na mechanism zake wanasayansi wameweza kutengeneza baadhi ya protien zilizopo kwenye cell lakini kamwe hawajaweza kutengeneza Hata single fully functional and independent cell.
Siku ukikutana na issues za spiritualism ndo utaamini. really ningekuwa mchawi mm ningefanya hata nikuroge tu.... Akili ingekukaa sawa iliujue kwamba ipo nguvu kuliko iliyo nje ya mipaka ya ufahamu wako..
Believe me!! siku ukirogwa hutatusumbua tena kama Mungu yupo au la?
 
Kwanza kabisa, sayansi haiaminiwi.

Sayansi haiendi kwa imani.

Mpaka hapo ushajionesha hujui sayansi ni nini.

Pili, sayansi kushindwa kutengeneza chochote si uthibitisho kwamba Mungu yupo.

Tatu, sayansi kushindwa kutengeneza chochote kinachotakiwa ni uthibitisho kwamba Mungu hayupo. Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo angetupa tu sayansi za kujibu maswali yetu wote. Bila kutubania.

Watu wamekufa na kuugua vibaya sana kwa kukosa madawa ya antibiotics tu, kwa maelfu na maelfu ya miaka.

Mpaka mwaka 1928 wanasayansi wakagundua, tena kwa bahati tu, antibiotics.

Sasa huyo Mungu alikuwa wapi miaka yote hiyo anaachia watu wanakufa bila kupenda, kwa mafungu, kwa vitu vidogo tu kama vidonda, wakati dawa anaijua na anaweza kuwapa watu wake wasiumie?

Huyo Mungu yupo kweli? Au mmemtunga tu?
 
You see kama ambavyo wewe umeniambia siikujui sayansi wewe pia hujui unacho kisema kuhusu Mungu, unaweza anza kujifunza lakini hujachelewa.......
Point yangu ilikuwa kama ambavyo mnasema kwamba wanaombini katika Mungu wanaamnini bila kuwa na ushahidi nimekuonesha pia hata wanasayansi wanaamini mambo ambayo hawana ushahidi nayo.... Kushindwa kuelezea cell ilitokanaje na big bang nikukosa ushaidi kwamba big bang inaweza kuwa chimbuko la uhai....
Sasa wanasayansi mnajisifia vipi kwamba mpaka ushahidi mkubali ikiwa kunambavyo vikubali bila ushahidi...
 
Imagine Vita ya Gaza,
Kuna watu wanajitoa muhanga ili wakafe na watu wengine kisa pepo .

Na wengine wanafanya mauaji Kwa kisingizio ardhi wamepewa na mungu, mungu Gani mwenye upendeleo wa kuwapa ardhi watu Fulani Tu,

Je SS wa tz 🇹🇿 mbona ardhi tumeipigania ss wenyewe, bila mungu kutusaidia

Mbona mungu analeta majanga kwa viumbe wake aliowaumba, badala ya kuleta Amani duniani
Unashida mahala hauko saw tatizo la afya ya akili limekuwa tishio sana
 
You see kama ambavyo wewe umeniambia siikujui sayansi wewe pia hujui unacho kisema kuhusu Mungu, unaweza anza kujifunza lakini hujachelewa.......
Point yangu ilikuwa kama ambavyo mnasema kwamba wanaombini katika Mungu wanaamnini bila kuwa na ushahidi nimekuonesha pia hata wanasayansi wanaamini mambo ambayo hawana ushahidi nayo.... Kushindwa kuelezea cell ilitokanaje na big bang nikukosa ushaidi kwamba big bang inaweza kuwa chimbuko la uhai....
Sasa wanasayansi mnajisifia vipi kwamba mpaka ushahidi mkubali ikiwa kunambavyo vikubali bila ushahidi...
Hata ikiwa wanaoamini katika sayansi hawana ushahidi, hilo halithibitishi Mungu yupo.

NI hivi, hata kama wanasayansi wanakosea kila kitu wanachosema, kukosea kwao huko haku contradict ulimwengu ambao hauna Mungu.

Tena, naweza kusema kuwa, inawezekana wanasayansi hawa wanakosea, kwa sababu wanaishi katika ulimwengu ambao Mungu hayupo, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo, angewafungulia ujuzi wawe wana sayansi nzuri yenye majibu ya kweli yanayoelezea kila kitu.

Kwa hivyo, ulimwengu wenye wanasayansi wanaoshindwa mambo ni ulimwengu unaodhihirisha Mungu hayupo.

Jitihada zako za kuwanyanyapaa wanasayansi kama watu wanaokwenda kwa imani tu, wasio na majibu, ukiziangalia kwa juu juu, zinaweza kuonekana zinawashusha wanasayansi na kumpaisha Mungu (logical fallacy, logical non sequitur).

Kiukweli, ukifikiri kwa kina, kimantiki, ulimwengu wenye ujinga wowote, ulimwengu wenye wanasayansi wasio na jibu la swali lolote wanaloweza kulifikiria, ni ulimwengu unaothibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo, kwa ujuzi wake wote, uwezo wake wote na upendo wake wote, Mungu huyu angempa kila mtu ujuzi wa kila kitu, hata mwanasayansi asingekuwepo. Kila mtu angekuwa anajua majibu ya mambo yote anayoweza kujiuliza au kuulizwa.

Umeelewa?
 
Hiyo aya ndo nilikuwa naisubiri uweke
Hawezi kuweka miaka na miaka ameshindwa kufanya hivyo,...atakachokifanya ni kwenda Google ku copy mambo meengi na kuja ku paste hapa., Wakati njia nyepesi ni kuleta Aya moja tu ili tuone kama ina contradiction kama anvyodai.

Akiambiwa aweke Aya moja tu inayoonyesha contradiction anakimbia.

NB: Qur'an si kama vitabu vingine mnavyovijua,.Ipo tofauti sana clear na rahisi kuelewa.
 
Hata ikiwa wanaoamini katika sayansi hawana ushahidi, hilo halithibitishi Mungu yupo.

NI hivi, hata kama wanasayansi wanakosea kila kitu wanachosema, kukosea kwao huko haku contradict ulimwengu ambao hauna Mungu.

Tena, naweza kusema kuwa, inawezekana wanasayansi hawa wanakosea, kwa sababu wanaishi katika ulimwengu ambao Mungu hayupo, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo, angewafungulia ujuzi wawe wana sayansi nzuri yenye majibu ya kweli yanayoelezea kila kitu.

Kwa hivyo, ulimwengu wenye wanasayansi wanaoshindwa mambo ni ulimwengu unaodhihirisha Mungu hayupo.

Jitihada zako za kuwanyanyapaa wanasayansi kama watu wanaokwenda kwa imani tu, wasio na majibu, ukiziangalia kwa juu juu, zinaweza kuonekana zinawashusha wanasayansi na kumpaisha Mungu (logical fallacy, logical non sequitur).

Kiukweli, ukifikiri kwa kina, kimantiki, ulimwengu wenye ujinga wowote, ulimwengu wenye wanasayansi wasio na jibu la swali lolote wanaloweza kulifikiria, ni ulimwengu unaothibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo, kwa ujuzi wake wote, uwezo wake wote na upendo wake wote, Mungu huyu angempa kila mtu ujuzi wa kila kitu, hata mwanasayansi asingekuwepo. Kila mtu angekuwa anajua majibu ya mambo yote anayoweza kujiuliza au kuulizwa.

Umeelewa?
Kama hata msipokuwa mnajua bado haithibishi uwepo wa Mungu, kumbe pia manweza mkawa mnakataa kwa sababu ya ufinyu wa maarifa.... So 'why even arguing '
Pili kwa ninavyofahamu mm huyo Mungu hafanyi vitu kama mm ninavyotaka..
Kanuni zake zinasema ufuata kila anachosema ufuate ndipo atakapotimiza mema yote kwako..
Mungu asingeweza kulazimisha mtu amfuate sababu Mungu ni Upendo na upendo haulazimishwi kwa mtu bali hutoka ndani kwa mtu.....
Habari njema ni kwamba siku moja wote tutamwona kila mmoja atakiri kwamba Mungu yupo na wewe ukiwemo then kila mmoja ataifuata hatima yake... #Mungu anakupenda na akubariki...
 
Inaonekana wewe bado mchanga sana kuelewa mambo haya.

Upeo wako wa kufikiri bado ni mdogo sana. Kama kingereza bado ni shida inabidi ujifunze mambo kwa mapana zaidi.

Mkuu Kiranga hapa ni sawa na kumfundisha mtoto wa chekechea hesabu za Calculus au Quantum physics.

Hawezi kuku elewa.
Kujua kiingereza hakuonyeshi kwamba wewe ni mwerevu kuliko wengine.

Mbaya zaidi mtu yoyote anayejiona ati ni mwerevu kisa anajua lugha ya kiingereza basi huyo ana ujinga na ushamba ndani yake.
 
Kama hata msipokuwa mnajua bado haithibishi uwepo wa Mungu, kumbe pia manweza mkawa mnakataa kwa sababu ya ufinyu wa maarifa.... So 'why even arguing '
Pili kwa ninavyofahamu mm huyo Mungu hafanyi vitu kama mm ninavyotaka..
Kanuni zake zinasema ufuata kila anachosema ufuate ndipo atakapotimiza mema yote kwako..
Mungu asingeweza kulazimisha mtu amfuate sababu Mungu ni Upendo na upendo haulazimishwi kwa mtu bali hutoka ndani kwa mtu.....
Habari njema ni kwamba siku moja wote tutamwona kila mmoja atakiri kwamba Mungu yupo na wewe ukiwemo then kila mmoja ataifuata hatima yake... #Mungu anakupenda na akubariki...
Tuseme mimi nahoji tu uwepo wa Mungu. usinihusishe sana na sayansi, sijawahi kutoa theory ya sayansi.

Kupinga uwepo wa Mungu haimaanishi uko upande wa sayansi.

Nielezee uwepo wa Mungu nimuelewe vizuri tu.

Kuna vitu viwili hujafanya.

1. Hujathibitisha kimantiki Mungu yupo.

2. Hujaeleza kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.
 
Kama Mungu yupo na alitaka tusimkufuru, Aliumbaje binadamu wenye uwezo wa kumkufuru?

Mungu huyo, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu watakao mtii siku zote pasipo kumkufuru?
Nadhani ungekua umeelimika vya kutosha usingeuliza swali la kitoto kama hilo.

Kuwa humble kisha kubali ujifunze, shida ni kwamba unaamini unajua vitu kumbe hujui,...kama upo open minded na free kujifunza chochote nenda kasome Qur'an utapata jibu la swali lako jepesi.

Nadhani ukishasoma hii Aya hapa chini hautorudia tena kuuliza swali lako hilo unalopenda kuuliza kila siku ukiamini umeuliza swali la msingi au lisilo na majibu kumbe ni uchache wa elimu tu:-

Surah Al-An'am , verse 149:

ولو شاء ربك لآمن من في الأرض كلهم جميعًا ۚ أفأنت تكره الناس حتى يكونوا مؤمنين

Translation: "And had your Lord willed, those on earth would have believed, all of them entirely. Then, do you intend to force people to become believers?
 
Sasa kama watu hawafosiwi kuwa believers, Allah huyo anataka aaminiwe ili iweje?

Kwa nini wasio mwamini Allah waje wapewe adhabu?

Ilhali Allah huyo amesema kwamba hafosi mtu amwamini.
 
Kujua kiingereza hakuonyeshi kwamba wewe ni mwerevu kuliko wengine.

Mbaya zaidi mtu yoyote anayejiona ati ni mwerevu kisa anajua lugha ya kiingereza basi huyo ana ujinga na ushamba ndani yake.
Sasa mleta mada anawekewa hoja kwa kingereza anasema hajui kingereza.

Anataka awekewe hoja kwa kiarabu au kiswahili.

Sasa hapo utajenga naye hoja vipi?

Yani uanze kujipa kazi ya kumtafsiria neno baada ya neno.
 
Back
Top Bottom