Uwepo wa Mungu unadhihirika kwa alama zake na viumbe vyake

Uwepo wa Mungu unadhihirika kwa alama zake na viumbe vyake

Kama vilivyo complex hivi vyote vyenye high order hivi ulivyovitaja, bahari, jua, watu, wanyama, ni lazima viwe vimeumbwa na higher intelligence, basi complexity haiwezi kutokea bila kuumbwa na higher intelligence.

Sasa, hapo hapo linakuja swali, kwa kanuni hiyo hiyo ya kwamba kilicho complex hakiwezi kuwepo tu, ni lazima kiwe kimeumbwa, hata Mungu wako naye atahitaji kuwa ameumbwa, na aliyemuumba naye atahitaji kuwa na muumba, hivyo hivyo, bila mwisho.

Kwa hiyo, ukisema kuwa bahari, jua, watu ni lazima vimeumbwa, kwa sababu complexity haiwezi kutokea tu, kimsingi hapo unasema Mungu hayupo, labda hujaelewa tu kwamba unajenga hoja kwamba Mungu hayupo.

Ni hivi.

Ama, hivi vitu complex ni lazima viwe vimeumbwa, ama si lazima.

Kama si lazima viwe vimeumbwa, hapo Mungu hahitajiki, kwa sababu kama ulivyosema, unatumia dhana ya kwamba Mungu kaumba kudhihirisha Mungu yupo. Kama vitu hivi si lazima viwe vimeumbwa, basi Mungu hahitajiki.

Kama ni lazima viwe vimeumbwa, basi huyo unayemuita Mungu naye ni lazima awe kaumbwa, na kama ni lazima awe kaumbwa, huyo si Mungu.

Sijui hata kama una uwezo wa kuelewa hizi hoja.
👍👏👌🤝
 
Back
Top Bottom