Uwepo wa Mungu unadhihirika kwa alama zake na viumbe vyake

Tupe uzibitisho Kwamba hivi vitu vimeumbwa na mungu,
Mbona haendelei na huumbaji?
Nikuulize watu wanapofanya tendo la ndoa anapatikana mtoto unafikili hapo sio uumbaji unaendelea kufanyika??
 
Labda ningeanza kwa kukuuliza
Hivi wewe una Akili.?...... Samahani mm nilisema vile kwa ku conclude kwamba unazo...
Labda na wewe hukunielewa mm kukuuliza hivyo maana yangu ni kwamba ' NOT EVERY THING THAT IS REAL MAKES SENSE' kwa kudhibitika kwa Logic....
Mfano mwingine binadamu tunakubali katika uwepo wa Muda (time) lakini lakini nikikwambia thibitisha... Sidhani kama utakuwa na majibu..
Vivyo hivyo kushindwa kuthibitisha uwepo wa Mungu kwa mantiki haimfanyi asiwepo....
Kama ambavyo ukishindwa kuthibitisha uwepo wa vijidudu kwenye maji haiifanyi visiwepo.. Inawezekana tu huna nyenzo za kukuonesha...
 
Sasa ndugu hivi vitu ni akili ya kuchotea maji mtungini...
Wewe ulitoka kwa wazazi wako.... Wazazi wako kwa wazazi wao trend inaenda mpaka tusikokujua..
Hoja yako haiwezi kuwa mjadala sababu tayari tumeshajiridhisha kwamba kila kitu lazima kiwe na origin... Shida tu ni kwamba origin ya baadhi ya vitu haijaweza kufahamika..
Lakini pia origin haitumiki kupinga existence.... Yaani hata kama hatujui wewe ulitoka wapi lakini tayari tunajua upo.... Vivyo hivyo hata kama hatujui Mungu alitoka wapi lakini tayari yupo... Sasa basi sisi tunafahamu kwamba huyo Mungu ambaye hatujui alikotoka ndio origin ya dunia na maisha yaliyopo duniani...
 
Kwa wewe unamini nini??
Na unaamini ukifa unaenda wapi??
 
Kwa wewe unamini nini??
Na unaamini ukifa unaenda wapi??
Nilizaliwa,sijaumbwa. Siamini katika uwepo wake na vitu mnavyompamba.

Sasa nikishakufa,naenda wapi? Nazikwa au nachomwa moto,nikifia kwenye maji,viumbe majini watakula,nikifia polini mifisi itakula. Biashara inaishia hapo. Wapi pa kuweka jam sasa!?
 
Akili ni nini?

Mara ya tatu nakuuliza swali.

Hulijibu, unazunguka tu na kurudia kutumia neno akili, ambalo hujali define.

Akili ni nini?
 
Nikuulize watu wanapofanya tendo la ndoa anapatikana mtoto unafikili hapo sio uumbaji unaendelea kufanyika??
Hayo ni matokeo ya tendo ya ndoa, na sio uumbaji , ingekuwa mungu anaumba tunapo fanya tendo la ndoa Basi kusingekuwepo kwa ugumba ,

Je mungu anapendelea kuumba na wengine kuwaacha.

So process ya kujamiana ni science na Sio uumbaji.

Hata tunapo kula na kunywa tunaenda haja , Je mungu kaumba haja,sio Kweli, kula na kunywa ni tendo la kisayansi

Isipo kula na kunywa hutaweza kwenda haja
 
Bac ukishapata nyenzo za kutuonyesha utuonyeshe Mungu..
 
Sasa umetumia Nini kujua kwamba
1. Mungu yupo?
2. Dunia na maisha vina origin?
3. Hiyo origin ni Mungu?
 
Vitu ambavyo ni complex lazima vimeumbwa/vimetengenezwa lakini si lazima process hii irudi nyuma ad infinitum kwani kwa logic hai make sense au haiwezekani ila kwa logic ina make sense kuwa itabidi iishie mahali fulani.
 
Mola mlezi chanzo cha kila kitu.

Sent from my SM-N975U using JamiiForums mobile app
 
Sasa umetumia Nini kujua kwamba
1. Mungu yupo?
2. Dunia na maisha vina origin?
3. Hiyo origin ni Mungu?
1.Nikijichunguza mwenyewe kama binadamu, dunia na vitu vyote vilivyomo design yake ni ya ajabu sidhani kama ni chance/probability ya hivi vitu kuwa hivi, hapo ndo nikawaza kwamba pengine kuna mtu/nguvu yenye maarifa iliyofanya yote haya.... Nilipozaliwa sikujua hili lakini kadri unavyokuwa ndio unapata kukuta theories kutoka kwa watu waliokutangulia na kuniambia hiyo nguvu/mtu mwenye maarifa anaitwa Mungu.....
Lakini pia imani za kishirikina nilizoshudia live sio kwa kuhadithiwa zikafanya niamini kuwa kumbe hata huyu Mungu ambae simuoni na hathibitiki kwa akili YUPO... Sababu imani za kishirikina pia hazithibitiki kwa akili.
2. Dunia na maisha vina origin sababu hata mm sio wa kwanza hapa duniani, hilo tu linaonesha kwamba kila kitu kina chanzo chake na hicho chanzo(origin) kwa viumbe na dunia ni Mungu...
 
Hayo ni mawazo yako ni sawa na mi niseme kila demu mweupe ana mapepe...ni mawazo tu.. hujaprove bado kuwa Mungu yupo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…