Uwepo wa Panyaroad mkoa wa Morogoro

Uwepo wa Panyaroad mkoa wa Morogoro

Daslama wakilia kuhusu panyaroad mnawacheka
Zamu ya mkoani sasa mnalala mapema zaidi ya kuku.

Ikiwa mnatoka kwenye jamii Moja,jamii mnayofahamiana basi mnaweza kutambua wenye hiyo michezo ya ajabu,kaeni,shirikianeni,tafuteni njia Nina hakika mtaweza kutatua lakini Kwa upande wa mamlaka/police si rahisi kugundua kwa haraka zaidi mtajikuta mnabebwa ambao hata sio wahusika ilimradi umekutwa umenyoa kiduku,denge,umevaa suruali kama sindano na shati kama pazia watakuambia wewe ni panyaroad/kibaka ,sehemu nyingine kama kawaida wameweka polisi jamii,sungusungu.

Anzeni nyie mkishirikisha mamlaka husika na kama matukio mengi yanafanyika usiku basi mtapata njia ya kudhibiti na kuwafahamu wahusika wanaofanya matukio kwa muda huo
 
JamiiForums tafadhari fuatilieni taarifa za Morogoro Kihonda kumekuwa na vijana nyakati za usiku wanagonga nyumba za watu ukifungua wanaiba na kushambulia watu kwa mapanga.

Inasemekana ni panya road. Mabalozi wa mitaa wametupa taarifa wananchi hatuna amani.

Hali imezidi kuwa Tete hakuna amani wapendwa kumechafuka mpaka sasa wameua mtu mmoja.
Solution ni Kuanzisha Ulinzi Shirikishi katika Mitaa yetu kila Balozi awe na Sungusungu wake. Wahalifu ni Wanamtaa na Sungusungu ni Wanamtaa
 
Lamobeni matakko yao kisha muwainamishe hao madogo.

Msicheke na nyani watawazoea au wangese.
 
Back
Top Bottom