Uwepo wa Rev. Fr. Charles Kitima kwenye utiwaji saini wa Mkataba wa DP World unahitaji majibu

Ushaabiki na uzandiki ni mwingi sana kwa bongolala. Sisi hatukupinga uwekezaji bali aina ya mkataba. Sijauona huo mkataba uliosainiwa lkn walau sasa wanatamka wazi ukomo wa mkataba na mipaka ya uwekezaji hata hao wa serikali wana ujasiri wa kuitamka. Hicho ndicho tulichokuwa tunakitaka.
 
Acha uongo,wewe kubali tu kuwa baada ya walaka safari za uarabuni zimekuwa nyingi mno na matokeo yake sasa hivi ni wazi kuwa ni miaka 30.
 
Kwa kuwa wewe ndo uliyekuwa kinara wa kupinga uwekezaji wa DP World hapa Nchini, na leo umehudhuria kikao cha utiaji saini jambo lile lile ulilolipinga kwa nguvu zote,
Hakuna wakati wowote ule ambapo Dr. Kitima au TEC waliwahi kutamka kwamba wanapinga uwekezaji katika bandari. Hukuelewa kwa vyovyote inavyoonekana, lakini pia rudia kusoma waraka.
NB: Fr. Kitima hawezi kwenda as an individual, lolote alilosoma au kusema, alifanya hivyo kama Katibu wa TEC
 
Kikubwa miaka iliyokuwa haijulikani imejulikana na wataishia bandari ya dar tu
Hiyo ni HGA, inahusu eneo moja tu la uwekezaji. IGA ndiyo inayohusu miradi yote, na ndiyo inayotamka kuwa haturuhusiwi kuleta mwekezaji mwingine mpaka tuwataarifu DP. IGA ipo vile vile. Hivyo DP wakitaka bandari ya Mwanza, itaandaliwa HGA ya bandari ya Mwanza, na yenyewe itahusu bandari ya Mwanza tu. Ikija ya Tanga, Mtwara au nyingine yoyote, itakuwa hivyo hivyo.
 
Hata kama mama alichukua points walizozisema TEC na akazifanyiakazi.

Lakini tunaomfahamu mama, alishaanzaa kakikundi ka chawa watakaofanya charracter assassination kama weww na wengine watakaojitokeza
 
... Binafsi sitatoa sadaka wala mchango wowote ule Kanisani, kwani sitakuwa tena na Imani na Kasisi yeyote yule.

(2) Nitajiuzuru nyadhifa zangu zote katika Kanisa na kuwashawishi wengine kufanya hivyo.
Haya yote nenda kamueleze Paroko wako usaidie mchakato wa kuondolewa sakramenti zako, maana RC huwa hawabembelezi wasioamini. Kutumia ID feki ni kama unatishia nyau
 
Ukweli ni kwamba Serikali imechutama kwa TEC...hadi wamewaita kurekebisha vipengele
Teh teh teh TEC yako imekula za uso hawana namna na nyie waamini mbumbumbu mtadanganywa mpaka mtie akili.

Nilisema since day one hakuna chokoraa yeyote wa kuizuia serikali kuendelea na uwekezaji sasa kiko wapi?

IGA ni ile ile haijabadilika chochote halafu udanganywe eti kuna marekebisho yamefanyika.

IGA imepitishwa na bunge ndiyo muongozo wa mikataba mingine iweje halafu unajitekenya eti mkataba umefanyiwa marekebisho.

Serikali ni dude kuuuuubwaaa.
 
Tuwekee huo mkataba hapa unaoonesha ukomo miaka 30.

Mnapenda kujipa umuhimu msiokuwa nao haki ya Mungu nyie.

IGA imepitishwa na bunge na mikataba yote inapita mle mle kwenye IGA.
 
Acha uongo,wewe kubali tu kuwa baada ya walaka safari za uarabuni zimekuwa nyingi mno na matokeo yake sasa hivi ni wazi kuwa ni miaka 30.
Mkuu mimi sijaongopa chochote, kelele zilikuwa zinapigwa kuhusu IGA hii iliyosainiwa jana ni HGA kwahyo mabadiliko unayoyasema hata hayahusiani, na safari nimeona ni QATAR wakati mkataba ni wa Emirates.
 
Tuwekee huo mkataba hapa acha kujilisha upepo.
 
[emoji38][emoji38][emoji1787][emoji1787][emoji1787] aise mnapenda kujipa umuhimu msiokuwa nao hadi mnatia huruma.

Hayo uliyoyasema hebu tuwekee huo mkataba hapa ili iwe source ya taarifa yako.

Mikataba yote ni siri sasa umeyajulia wapi hayo kama sio kujitia upepo?
 
Umemshambulia personal badala ya kujibu hoja yake kuu kwamba kitu walichowaaminisha waamini wao kwamba hakipaswi kuwepo iweje jana wawepo kwenye utiaji saini?
 
Kitima waeleze Wakatoliki kwanini uliwasumbua waumini na ngonjela za WARAKA wa kitume wa kupinga mkataba wa bandari? Leo uko kwenye sherehe kuonesha kuwa sasa TEC hama pingamizi tena. Umeuona mkataba wanaosema umerekebishwa?
Kumbe nyote ni hopeless!
 
Unawashwa washwa
 
Mktaba umebadilishwa sana
 
Tulishawaambiaga siku nyingi acheni kuwa mateka wa wanaharakati kama hawa akina Kitima na kundi lake
 
Kitima waeleze Wakatoliki kwanini uliwasumbua waumini na ngonjela za WARAKA wa kitume wa kupinga mkataba wa bandari? Leo uko kwenye sherehe kuonesha kuwa sasa TEC hama pingamizi tena. Umeuona mkataba wanaosema umerekebishwa?
Kumbe nyote ni hopeless!
Jana nimecheka sana na kujidharau. Asubuhi nikiwa kanisani paroko wetu alizungumzia tena kuhusu mkataba wa bandari tena kwa uchungu mkubwa. Lakini masaa machache baadae, nilichokiona katika mitandao kikaniacha hoi.

Ila nimepata fundisho, akili yangu ndio ya kuiamini zaidi kuliko akili za wengine. Chochote kitakachotokea leo na baadae, nitaisikiliza zaidi akili yangu kuliko hizi sauti za kitapeli za Viongozi wa dini, wanaharakati, wanasiasa na wajuaji wengine

Sent from my Infinix X6816 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…