Uwezekano wa Magufuli kuongoza nchi kwa kipindi cha pili haupo

Umechambua vizuri ila katikati ukaingiza ushabiki wako wa kivyama, umeweka vitu ambavyo kiuhalisia havipo. Mtu kama Lowassa huwezi kumpa nguvu za kisiasa ulizompa, hana tena amezipotezea upinzani. Ila ni kweli waliokua wanamuunga mkono wapo lakini walishabadilisha uelekeo kwenda kwa magu. Kundi la kina kikwete lipo lakini ni kama vile limeparalyse, wamebaki wanatapatapa tu kwa maneno, vijembe kama yanayoendelea sasa, lakini hawana ushawishi wowote wa maamuzi kwenye chama.

Magufuli ambae umetaka kutuaminisha kwamba hana nguvu yoyote, kiuhalisia ndo ameshika mpini mpaka 2025. Hivi Mwenyekiti wa chama unakuaje eti huna nguvu kwenye chama. Sekretariati yote ya chama iko chini yako na umeichagua mwenyewe. Isitoshe Serikali unaiongoza wewe. Kwahiyo, maamuzi yote yanayohusu chama na Serikali yeye ndo anayacontrol. Halafu anawezaje asichaguliwe kuongoza kipindi cha pili eti kwa nguvu ya watu wasio na mamlaka. Hebu tuondolee hizi porojo.
 
Vituko havitaisha
Vituko havitaisha duniani.
 
Mkuu naamini kabisa kwamba kundi la Lowassa bado linataka nafasi yake kweli?
 
Kitu kimoja hapo ulichosahau makusudi kabisa ni kuwa unaelewa Mzee Lowassa anaumwa, na unajua kabisa kwa hali yake hawezi gombea na hawezi mikiki tena ya kuzunguka kwa campaign! Kundi la kikwete naona wakina Januar Makamba kuna Membe wako front lkn upande wa Lowassa sioni aliye mbele zaidi yake Lowassa mwenyewe, ila ukweli ni kwamba kwa sasa kundi la mkwere litapitia misukosuko na Rais ataibuka na kundi lake na kusonga 2020 ila come 2022 hapo ndo minyukano itakuwa ya ukweli haswa kwa kuwa kutakuwa hakuna kuogopana it will be war kundi la Lowassa, kundi la Mkwere na kundi la ccm mpya bila kusahau na wastaafu nao sijui wataangukia kundi gani!
 
Duh! Wewe ndio umechemka kabisa kumleta Ngoyai kwenye equation. Mtu ambaye yuko 'ICU' anawezaje kweli kugombea Urais?
Labda hujaona clipp yake ya hivi karibuni... Ngoyai keshajichokea. The best for him now ni kujiandaa kiroho kwa safari inayofuata...

Umeni pre-empty! Kwa vyovyote iwavyo tutaenda na JPM tena 2020
 
Mkuu "you nailed it" lakini ktk hizo nguvu umesahau na nguvu za Mungu, so kwa mtazamo wangu ziko nguvu tatu:
- Nguvu ya Mungu.
- Nguvu ya Wananchi.
- Nguvu ya Dola.
 
Sioni namna ambavyo aliyeko madarakani hivi sasa na ni kiongozi wa chama eti aenguliwe halafu aingie mgombea mwingine aliyeshindwa uchaguzi wa 2015.CCM ya sasa inajisafisha na kuondoa madoa, mengine yanajiondoa yenyewe. Ukiisha fika uzee na wakati mwingine hata kabla ya uzee,mwili ukaonyesha kila dalili za kuchoka, busara inaelekeza utafute ufalme wa mbingu. Namuunga mkono Magufuli amalize kutekeleza kazi ambazo Mungu amempa kwa ajili ya taifa letu na Mungu hajipingi. Huyu anahitaji zaidi kuombewa na kushauriwa kwani kama binadamu ana mapungufu yake. Analysis imekosa mwanga wa Mungu.
 
Wananchi wanaitaji mabadiriko ya katiba mpya atakaye fanya hivyo atapendwa na watanzania wote .Lakini kushabikia utawala wa kuendeleza himaya ya chama kimoja itakuwa shida .Mawazo ya nani atatawala baada ya kiongozi aliyepo sasa sio kipaumbele cha watanzania kwa sasa.Hata hao wanaopendekezwa wakina Lowasa ,Slaa hawana mvuto tena maana siasa ni upepo unabadirika wakati wowote.
 
Bwana Yesu rudi ulimwenguni mambo yamebadilika kila mtu anapataka ikulu sijui kuna biashara gani hapo inayogombewa Baba mwokozi?
 
Magufuli akiongoza muhula mmoja atakuwa amejijengea heshimu kubwa ndani na nje ya nchi. Kinyume na hapo ataondoka nyumba ya chokaa kwa aibu.


Wanzuki oyeeeeeee
 
Hayo makundi ni ya aina gani, maana Mzee Edward alipoondoka mbona hakuna kundi lililomfuata?

Hayo makundi ni ya maslahi tu, ni ya wakati wa kula tu wakati wa njaa humuoni Mtu.
Inajulikana kabisa duniani na mbinguni Rais Magufuli ataendelea kuongoza kwa kipindi kingine cha miaka 5. Hawa wanaosema ataongoza kwa kipindi kimoja tu ni wehu.
 
Paschal Mayalla aione hii kwenye file


 
By the way eti ya kweli haya.. nimeikuta sehemu.

"Serikali Na Kampuni Ya Barrick Wamekubaliana Kuwa Bunge La Tanzania Halitaruhusiwa Kutunga Sheria Yeyote Ambayo Itabadili Makubaliano Yao Na Kodi Zote Zilizokuwa Zinafanya Kazi Wakati Wa Kuingia Makubaliano Hazitaweza Kubadilishwa Kipindi Chote Ambacho Barrick Watakuwa Tanzania."
 
Mwenye uhakika wa kushinda kwa asilimia zote kama atasimamishwa na CCM ni Dr slaa peke yake wengine wasubiri kulambishwa mchanga na CCM yao iliosheheni majizi na mafisadi.

Kwa hiyari yao wenyewe pasipokulazimishwa na mtu yeyote,waliunda tume ya kuchunguza wizi wa mali za chama chao,halafu wanaionea aibu wenyewe kuitoa hadharani kwa kuwa imejaa uchafu mtupu, wameigeuza kuwakitisho cha kuwatishia wanaccm wenzao wanaowakosoa kama hawataacha kuwakosoa wataitoa hadharani ili wananchi waone jinsi walivyo wezi.
 
MWANDISHI HUNA AKILI, UNAOTA NDOTO MCHANA KWEUPEEEEE.. JPMS 2020 ATASHINDA ZAID YA 80%
 
Walianza kusema ni nguvu ya soda tu wanampa mwaka mmoja atakua ameshalegea sasa mwaka wa nne mwendo ni ule ule,ni yetu macho tu
 
Yetu macho, waache watifuane, sisi kwetu ni furaha. Kiukweli jiwe hakubaliki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…