Ashasembeko
JF-Expert Member
- Dec 14, 2017
- 226
- 914
Kweli, tumeshazoea wanasiasa wakitoa maneno ya uchochezi wanakamatwa moja kwa moja, hamjiulizi kwanini sasa hizi wanakemewa tu?? Kuna jamboNdio maana hata Siro matamshi hayaishi!
Unaogopa vikwazo ?Katika historia za chaguzi Tanzania, Zanzibar mara nyingi ndio huwa inaleta utata. Kama mnakumbuka uchaguzi wa 2015, alioporwa Maalim Seif, ulisababisha wadau wa maendeleo kukisusia kisiwa hiko. Marekani iliondoa msaada kwa Tanzania wa takribani trillion moja, huku wadau wengine kama UK na nchi za Jumuiya za Umoja wa Ulaya ziligoma kujihusisha na serikali hiyo.
Ni mwaka jana, ndipo balozi wa UK, Sarah Cooke, alikanyaga kwa mara kwanza Zanzibar toka uchaguzi ufutwe 2015, tena alienda kuongea na viongozi wa upinzani na chama tawala kuhusu uchaguzi wa 2020. Huu uchaguzi unaweza kuwa wa kwanza kwa Tanzania bara kuwekewa vikwazo.
Kama mfanyakazi wa moja ya hizi balozi kubwa hapa nchini, naomba niwahakikishie kuwa huu uchaguzi unafuatiliwa kwa ukaribu sanaaaa kuliko hata wa 2015. (Tundu Lissu nae anaelewa hili, angalia tweet yake hapo.
View attachment 1545125
Hawa wadau wanapokea ripoti za kila wiki (zinaitwa "October Elections: Weekly analytical Overview") kuhusu YOTE yanayojiri nchi ikiwemo mambo ya kutekwa, kuchomwa ofisi za upinzani, n.k. Na Magufuli na Kabudi wenyewe wanajua kuwa wanafuatiliwa maana wanainformers mabalozini wanaowapa taarifa.
Ukweli ni kwamba, sababu kuu ya Magufuli na wenzake kutomdhuru na kumkamata Lissu ni jumuiya ya kimataifa. Magufuli knows his actions are being closely monitored na anajua kuna uwezekano mkubwa sana nchi ikawekewa vikwazo kama uchaguzi utakandamiza sana wapinzani.
Magufuli anajaribu kukwepa serikali yake kuwekewa vikwazo hivo, maana yeye ndio atakuwa Rais wa kwanza wa jamhuri ya Muungano kuwekewa vikwazo. Ndio maana unaona, hata tabia za Tume - japo bado sio perfect - zinajaribu kuwa fair, japo bado kuna kasoro kadhaa zinazojitokeza.
Na mimi ninaamini, jina la Tundu Lissu litapitishwa na NEC, uchaguzi utakua competitive lakini, we all know who is going to win - japo not freely and fairly, kwa sababu ana polisi, tume, mahakama na usalama wa taifa mfukoni.
Ila pia natambua kuwa Magufuli hatabiriki, sitoshangaa yaliyofanyika serikali ya mtaa yakajirudia, ila jueni kuwa yakifanyika hayo, mtaona mengi tu. We will for the first time be in the limelight of the international community. Unaona Zimbabwe ilivyosusiwa, ndipo tunapoelekea.
Na naomba nimalize kwakusema, mi nasikikita kuwa, jumuiya ya kimataifa ndio ina-check- mwenendo wa kiongozi wa nchi yetu pamoja na kuwa tuna mahakama, asasi za kiraia na hata media. We can do better as a country.
Hilo sio swali la kuniuliza mimi bali, Mwenyekiti wa Chama tawalaUnaogopa vikwazo ?
Zimbabwe is coming very soonBaada ya uchaguzi, mtafurahi wenyewe
Tz si failed state.
Lol, okayMjinga tu ndio atakubaliana na hicho ulicho andika.
Tatizo, mnasoma kujibu, sio kuelewa. Kuna sehemu nimeandika kwamba tutawekewa vikwazo kisa Tundu Lissu. Nimesema tutawekewa vikwazo kama chaguzi utakandamiza wapinzani na utaonyesha taswira ya kutokuwa huru na haki. Go read about Zimbabwe politics and you will maybe get a glimpse of what i am talking about.Kama ni kweli unafanya kazi Ubalozini basi utakuwa aidha ni dereva au karani kwa maana inaelekea wala hauelewi jinsi Uhusiano wa kidiplomasia unavyofanya kazi, Muzungu hawezi kuiwekea Tanzania yetu sanctions sababu ya Tundu lisu acheni kujidanganya, Muzungu anaweza tu kuiwekea Tanzania yetu sanctions kama Tanzania yetu inahatarisha maslahi yake, hakuna zaidi ya hapo, na mpaka sasa hivi maslahi ya Muzungu na international community yako intact kuanzia kushiriki kwa majeshi yetu kwenye vikosi vya kulinda amani mpaka uwekezaji wa Mkampuni ya Muzungu hapa kwetu kuanzia madini mpaka Benki kama NMB na CRDB kote huko kuko intact sasa sanctions waweke kwa lipi? Isitoshe kwani hao akina Tundu lisu wameanza leo kujiuza huko kwenye ofisi za muzungu kutaka hilo litokee mboa kimya mpaka leo hii na hakuna santions zozote?
Unadhani hiyo ni by choice?? Je unahabari UNDP iligoma kufinance uchaguzi?? Undhani kwanini NEC ilipitisha guidelines za kufanya option kualika wasimamizi wa uchaguzi wa nje... THINK!!. Tena hizo hela za uchaguzi zimetolewa kwenye Foreign Reserve (for the first time ever)Uchaguzi huu tunagharimia kwa asilimia Mia moja bila pesa ya mfaddhili toka Tanzania ipate Uhuru billion 321 pesa zetu zinagharimia tutaelewana tu taratibu
Tatizo, mnasoma kujibu, sio kuelewa. Kuna sehemu nimeandika kwamba tutawekewa vikwazo kisa Tundu Lissu. Nimesema tutawekewa vikwazo kama chaguzi utakandamiza wapinzani na utaonyesha taswira ya kutokuwa huru na haki. Go read about Zimbabwe politics and you will maybe get a glimpse of what i am talking about.
Haisaidii?? Je una habari mwaka 2019 serikali ilibadilisha sheria kandamizi ya Takwimu kisa ya pesa za hawa mnaowaita mabeberu?? Tuache uchaguzi uendelee ndio tutajua unasaidia au lah!!Hizi kelele za hawa mabeberu zingekuwa zina saidia Mataifa kama Uganda, Rwanda, KoreaN, Iran nk yangesha futika katika ramani ya dunia maana hawa ya pende kwelikweli. Kinachotakiwa hapa ni msimamo kisawasawa na kuwapotezea waone vitendo tu. Uzuri wenyewe kibaraka wao tunaye. Na mawasiliano yake na wao unaweza kuyasoma kama hivi.