Katika historia za chaguzi Tanzania, Zanzibar mara nyingi ndio huwa inaleta utata. Kama mnakumbuka uchaguzi wa 2015, alioporwa Maalim Seif, ulisababisha wadau wa maendeleo kukisusia kisiwa hiko. Marekani iliondoa msaada kwa Tanzania wa takribani
trillion moja, huku wadau wengine kama UK na nchi za Jumuiya za Umoja wa Ulaya ziligoma kujihusisha na serikali hiyo.
Ni mwaka jana, ndipo balozi wa UK, Sarah Cooke, alikanyaga kwa mara kwanza Zanzibar toka uchaguzi ufutwe 2015, tena alienda kuongea na viongozi wa upinzani na chama tawala kuhusu uchaguzi wa 2020. Huu uchaguzi unaweza kuwa wa kwanza kwa Tanzania bara kuwekewa vikwazo.
Kama mfanyakazi wa moja ya hizi balozi kubwa hapa nchini, naomba niwahakikishie kuwa huu uchaguzi unafuatiliwa kwa ukaribu sanaaaa kuliko hata wa 2015. (Tundu Lissu nae anaelewa hili, angalia tweet yake hapo.
View attachment 1545125
Hawa wadau wanapokea ripoti za kila wiki (zinaitwa "October Elections: Weekly analytical Overview") kuhusu YOTE yanayojiri nchi ikiwemo mambo ya kutekwa, kuchomwa ofisi za upinzani, n.k. Na Magufuli na Kabudi wenyewe wanajua kuwa wanafuatiliwa maana wanainformers mabalozini wanaowapa taarifa.
Ukweli ni kwamba, sababu kuu ya Magufuli na wenzake kutomdhuru na kumkamata Lissu ni jumuiya ya kimataifa. Magufuli knows his actions are being closely monitored na anajua kuna uwezekano mkubwa sana nchi ikawekewa vikwazo kama uchaguzi utakandamiza sana wapinzani.
Magufuli anajaribu kukwepa serikali yake kuwekewa vikwazo hivo, maana yeye ndio atakuwa Rais wa kwanza wa jamhuri ya Muungano kuwekewa vikwazo. Ndio maana unaona, hata tabia za Tume - japo bado sio perfect - zinajaribu kuwa fair, japo bado kuna kasoro kadhaa zinazojitokeza.
Na mimi ninaamini, jina la Tundu Lissu litapitishwa na NEC, uchaguzi utakua competitive lakini, we all know who is going to win - japo not freely and fairly, kwa sababu ana polisi, tume, mahakama na usalama wa taifa mfukoni.
Ila pia natambua kuwa Magufuli hatabiriki, sitoshangaa yaliyofanyika serikali ya mtaa yakajirudia, ila jueni kuwa yakifanyika hayo, mtaona mengi tu. We will for the first time be in the limelight of the international community. Unaona Zimbabwe ilivyosusiwa, ndipo tunapoelekea.
Na naomba nimalize kwakusema, mi nasikikita kuwa, jumuiya ya kimataifa ndio ina-check- mwenendo wa kiongozi wa nchi yetu pamoja na kuwa tuna mahakama, asasi za kiraia na hata media. We can do better as a country.