Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pole sana kama nilivyosema hapo juu mafundi wetu hawana uhadilifu ndio maana wanakuwa masikini muda mwingi hawana kazi wanafanya vibarua tuTanzania Ina mafundi wezi sana
Mdigi alijenga eneo Fulani Kwa haraka ili tuhamie duh nyumba alilipuliwa kinoma huwezi kujua maana rangi safi ndani sebuleni pakaanza kutoka rangi ukigusa ukuta ni mchanga tu nje usiseme balaa lilipoanza mvua kupiga Kwa miezi kadhaa palikuja kipind Cha mvua noma nje ilibabuka alitumie Tena SI chini ya mil 15 kukarabati msingi maana kwa chni palilika sana japo tuko ndani ila tuna hofu inaweza kuanguka wakichimba usawa wa msingi ukiangalia mawe yamepangwa Kuna gape then juu wamekimbilia kupiga zege
Ilikaa miaka 5 ndo ikaanza matatizo mpaka Sasa mara karekebisha ukuta pale sebuleni karudia upya palikuwa na vumbi na like feni
Ila aliharibu sana mtu alimuuzia kiwanja ni fundi ujenzi ambaye ndo baada ya kununua akampa huyo huyo dili la kujenga pale
Hatuna mafundi wasomi, wengi ni ujanja ujanja tu, ndio shida.Hawezi kukupa ushauri wa kifundi, au ukimwambia kwanini hapa umefanya hivi na sio hivi hana jibu.Mafundi wa Tanzania bado wanasafari ndefu sana ya kujifunza kutoka kwa mafundi wa nje . Mashundi wetu wanapenda sana short cut na kona … ukiwapa mwanya kidogo tu wanakuibia vifaa vya ujenzi , wanajenga kwa kuripua yaani ili mradi tu .
Hawana uhadirifu kabisa sasa mtu atafute pesa ya kuwalipa na bado awepo site muda wote ili kulinda ubora wa kazi na vifaa. Wangekuwa na akili wangejua kwamba ukitaka kufanikia jambo la kwanza ni uhadirifu, ukiwa muhadilifu kila utakayemfanyia kazi ataku-refer kwa wengine so more jobs and more money lakini sasa kama lazima nikuchunge muda wote unazani naweza kumshauri mtu mwingine akutumie?
Mimi nilijenga sqm 1060 kwa tofari 4760,cement mifuko 120,kokoto Lori 5 nondo 12mm 108 mchanga Lori 6 get 2ml hadi kulifunga,gharama za ujenzi 3ml! Piga hesabu na hapo ukuta sijafanya finishing plasta bado Renta ya juu bado na ulembo wa getiniNina wasiwasi huyu jamaa ametoa tuhuma za wizi bila kujiridhisha.
Kiwanja cha 1,000 sqm= 33×30m.
Hiki kinaweza kujengwa tofali zisizopungua 3,700.
Bado cement
Mchanga
Nondo
Urembo
Plasta
Gate
Gharama za mjenzi.
Hii pesa ni ndogo
Usijenge kwa remote control , kwa project kama hiyo ni bora urudi usimamie mwenyewe then unageuza fasta , kama nafasi hairuhusu ni bira ukae na pesa yako hadi utakaporudi.Mimi naishi nje ya nchi mwezi uliopita nilijenga uzio wa kiwanja huko kigamboni nilitumia 22millions kwa kiwanja cha 1000sqm huo uzio nilioonyeshwa yaani natamani hata niubomoe kabisa
Ni tatizo kubwa kwa kweli na serikali ndio inalea hili tatizo watu hawa wangekuwa wanafungiwa kujenga permanentlyKuna contractor mmoja nilimpa kazi alichokifanya kwanza aliminya sqms kurudi katika ramani na uhalisia tofauti! Kanipiga cm 147! Kumuuliza akasema kulikuwa na shida basi fundi kusoma vipimo tukamaliza baada ya kuvunja msingi wa mita 25 urefu na upana cm147! Akawa ameongeza, nikawa naenda site nikakuta kuwango cha sementi siyo, nikamuuliza akasema kipo poa baada jua kuwaka ni kokoto na mchanga akarudia! Sasa issue nilisafiri kurudi nakuta juu kenchi siyo mbao treated pia siyo mbao zilizopigwa randa ni kama mabanzi kayapasu tukagombana sana! Mabati tulikubaliana gauge 28 Alaf nikakuta shanishea gauge 32 hiyo hadi polisi akasema anakuja kubadili hakuja nanilikuwa almost 95% hivyo nikaja kubadili mwenyewe jamaa nitapeli sana. Ukikuta contractor anaitwa KIFARU CONTRACTOR Ogopa usijiassociate naye kabisa ni hovyo kabisa!