Bado roho yake ilikuwa inailinda na kuifuatilia familia yake na kwakweli walipaswa kuisikiliza sauti yake
Kusema wasali ni Dalili njema kuliko angesema wafanye ushirikina
Ngoja takujibu kwa kina
Nakubaliana na wewe katika hili, miezi kadhaa baba angu mdogo alifariki, baada ya kumzika ikawa kila siku lazma nimuote, siku za mwanzo nikaona ni kawaida may be nna mawazo ya kifo chakeKwanza lazima tukubaliane kuwa ndoto ni vague memories ya matukio yote ya kila siku yawe ya kuwaza kunena na kutenda lakini inapotokea marehemu kakutokea ndoroni na ujumbe fulani kwako hiyo ni ndoto ya ujumbe yenye uhalisia
Mm huwa nasikia kabisa sauti ikinikataza nisiende sehemu fulani km nilipanga kwenda huko, zaman nilikuwa sijali na nikienda huko nilikokatazwa napata kasheshe lolote lile. Pia nikiwa kwenye matatizo mazito sana sana ile sauti naisikia ikinielekeza nn cha kufanya na yanakuwa mepesi kuliko mwanzo.
Hakuna ufundi mkubwa zaidi ya kumsogelea na kumwambia taratibu kile unachotaka kumwambia
Kumbuka hatakujibu wala kugeuka au kushtuka lakini akikubaliana na ombi lako utagundua tu tofauti
Kwa mfano kama mikono ilikuwa inakakamaa kwenye kumvalisha mikono hiyo hiyo hulainika
Hii ni ile hisia ya sita na inafanya kazi karibia na uhalisia wake... Kwa kiswahili cha kawaida ni machale
Mkuu Mshana, kwa nini binadamu tuna kawaida ya kutowekea maanani hisia ya SITA??
Mkuu humu wataanza kukuogopa...
Iko hivi sikuwa anakataa live bali wakati wa kumvisha kama ni koti shati au hata suruali kuna kiungo kimoja hukakamaa kwa mfano kama ni mkono haunyanyuki au haukunjiki, kama ni mguu unajipinda au unakuwa mzito kunyanyua
Hivi vitu vinafanyika kwa namna ya ajabu na ya kipekee kabisa
Vilevile kuna kukosea vifungo au zipu kujichanganya! Yani mnaanza kufunga kifungo cha kwanza vizuri kabisa mkifika mwisho aidha vimepishana au mmeruka matundu, tulishawahi kukosea vifungo Mara SABA
Ni mpaka nilipotumia elimu niliyojifunza kuongea na marehemu kwa upole na kwa kumbembeleza ndio mambo yakawa sawa, na pia ndani ya chumba husika kama yupo mtu alikuwa na ugomvi na marehemu hakuna kitakachokwenda sawa hapo mpaka yule mtu atoke
Hahahaaaaa Zamaulid nimecheka hadi kidogo nipaliwe nakumbuka siku ya kwanza Kupewa maiti niiweke vizuri sikulala na kwakweli sikula nyama karibia wiki 2! Ilikuwa maiti iliyochomwa moto halafu ukazimwa kabla haijateketea yote
Na kuna wakati nikakosa mchumba hivi hivi baada ya kumwambia nafanya kazi gani hakulala aliaga na hakurudi tena