Iko hivi sikuwa anakataa live bali wakati wa kumvisha kama ni koti shati au hata suruali kuna kiungo kimoja hukakamaa kwa mfano kama ni mkono haunyanyuki au haukunjiki, kama ni mguu unajipinda au unakuwa mzito kunyanyua
Hivi vitu vinafanyika kwa namna ya ajabu na ya kipekee kabisa
Vilevile kuna kukosea vifungo au zipu kujichanganya! Yani mnaanza kufunga kifungo cha kwanza vizuri kabisa mkifika mwisho aidha vimepishana au mmeruka matundu, tulishawahi kukosea vifungo Mara SABA
Ni mpaka nilipotumia elimu niliyojifunza kuongea na marehemu kwa upole na kwa kumbembeleza ndio mambo yakawa sawa, na pia ndani ya chumba husika kama yupo mtu alikuwa na ugomvi na marehemu hakuna kitakachokwenda sawa hapo mpaka yule mtu atoke