Uwezo wa kuongea na wafu: Elimu Iliyoshindikana duniani

Braza mshana jr ni MTU muhimu sana hapa jukwaani...ukianza kusoma thread zake huwez acha
Tumuombee long life anatusaidia sana
Be lessed kaka
 
Elimu ya kuongea na wafu ipo na inafanya kazi vizuri sana. Tanzania nina mfahamu mtu mmoja mwenye elimu hiyo. Elimu hiyo kwa kitaalamu inaitwa Necromancy ama kwa lugha ya kiswahili unaweza kuiitwa RITIFAA. Nikipata nafasi nitakuja hapa na maelezo ya kina kuhusu MWENYE HEKIMA huyo mwenye uwezo wa kuzungumza na nafsi za watu walio fariki.
 

Mkuu wapo watu wenye uwezo wa kuongea na wafu. Kuna mtoto wa Mfalme wa Norway anaitwa Märtha Louise Harald. Huyu ana uwezo wa kuongea na watu live. Mwaka 2008, aliiomba Serikali ya nchi hiyo kuanzisha shule kwa ajili ya kufundisha watoto na watumbali mbali namna ya kuwasiliana na wafu moja kwa moja. Ila serikali haikukubaliana na hoja yake hiyo kwa madai kuwa hakuna tija yoyote kuongea au kuwasiliana na wafu. Ila kiukweli watu hawa wapo
 
Walikosea sana kumkatalia hii elimu ingetatua vitendawili vingi vya vifo vyenye utata
 
Imani zingine hazina ukweli ila zipo kutia watu hofu tu.We mwenyewe unaweza kuunda uoga au ujasiri.Jinsi uonavyo ndiyo jinsi ulivyo.Unaongozwa na akili yako.
 
Mshana jr asome sana BIBLIA ili awe na rejea nyingi na Mungu amtie nguvu aweze kutuletea mada nyingi humu ndani.
 
Mshana jr asome sana BIBLIA ili awe na rejea nyingi na Mungu amtie nguvu aweze kutuletea mada nyingi humu ndani.
Biblia pekee haitoshi bali lazima na kupata mtazamo wa upande mwingine ile kuweza kupata mizania ya kile unachotaka kukijengea hoja
 
uongo mtupu kudadeki
binadamu akifa yan hapo no connection no converstion no communication kwamba kinachobaki pale ni mwili tu.. na ayo mambo ya roho na nafsi vnakwenda wap tunamuachia SIR GOD

ayo mamvo mengine mnayosema ni swwaga za kale walikua wanazitumia mababu zetu pasipo kumjua MUNGU
 
Marehemu huwa anaskia mkuu amini
 
Vuta kumbu kumbu zake kwa yale yote mema alokufanyia na unapolala sema kimoyo moyo nataka kuongea na wewe baba Mara 3 alafu taja kile kitu unachotaka kumuuliza alafu lala hakika atakujia na kukupa majibu stahiki
 
Ni hakika hata mimi mama alifarki mda mrefu ila napokuwa na jambo ambalo nataman kumuuliza huwa nafanya ivo
Pia napotaman kumuona huwa nafanya ivo nae hunitokea na huwa hunieleza mengi mkuu
 
Shetani ana njia nyingi na mbinu za kuwahadaa binadamu. Anaweza akajibadili akakujia katika ndoto katika umbo la marehemu fulani, wewe ukakurupuka kuwa marehemu kakutokea katika ndoto! Watu wa Mungu mtaangamia kwa ukosefu wa maarifa yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…