Uwezo wa kuongea na wafu: Elimu Iliyoshindikana duniani

.
tapatalk_1522869400930.jpeg
 
Hivi ni kwamba haiwezekani kuongea nao au ni elimu ngumu? Maana hata Bibilia inaonyesha wafu waliamshwa
 
Ni aina ya elimu inayojulikana kizungu kama forbidden knowledge
 
Mbona mi nakutana na wapendwa wangu waliotangulia mbele ya haki, ndotoni nakunipa ishara fulani nikiifata kweli inakuwa huvyo kama nilivyo agizwa
 
Hakuna ufundi mkubwa zaidi ya kumsogelea na kumwambia taratibu kile unachotaka kumwambia
Kumbuka hatakujibu wala kugeuka au kushtuka lakini akikubaliana na ombi lako utagundua tu tofauti
Kwa mfano kama mikono ilikuwa inakakamaa kwenye kumvalisha mikono hiyo hiyo hulainika
Sasa mikono ikilainika mimi nafaidika nini, swali ni nawezaje kuongea nae
 
Mbona mi nakutana na wapendwa wangu waliotangulia mbele ya haki, ndotoni nakunipa ishara fulani nikiifata kweli inakuwa huvyo kama nilivyo agizwa
Ni jambo jema kwakuwa wanaweza kukuepusha na hatari nyingi na kukuelekeza mengi
 
Mkuu Mshana.

Tanga twaamini sana matambiko na hiyo ndiyo jadi yetu si wabondei, wazigua wasambaa na hata wasegeju.

Hata baadhi ya makabila mengine wana taratibu zao za kutambika.

Wakati naishi Ireland niliwahi kuona wenzetu wazungu wa kabila la Irish wale wanaoitwa Gipsy wao wanakwenda kwenye makaburi ya waliotangulia na kutumia siku nzima kushehereka kwa kunywa pombe pamoja na kucheza muziki kwenye eneo hilo.

Haya matukio ya jadi hizi yapo sehemu nyingi duniani na watu hupita wakifanya mambo haya waziwazi.

Lakini je, ni vizuri kila siku kusafisha kaburi kwa mazungumzo na roho ya marehemu au inahitajika kipindi maalum kila mwaka?

Ikiwa ni roho tu basi twaweza kuzungumza nayo mahali popote tulipo bila kwenda kaburini.

Je, jadi yaweza kuachwa bila madhara?

Au wewe waonaje kwenye hili?

Maana mimi nimekuwa mzito sana kwenda Potwe miaka hii.
Nvihi vihi mgosingwa ,hangi kaya nwagima?
 
Hivi ni kwamba haiwezekani kuongea nao au ni elimu ngumu? Maana hata Bibilia inaonyesha wafu waliamshwa
Mkuu unapolinganisha vitu vya kwenye biblia uwe makini,hao wafu walioamshwa kwenye biblia walimshwa na nani?Hilo ni la msingi sana otherwise shetani anaweza akakuletea mtu ukazani ameamshwa na akafanana na ndungu yako sura hata sauti kisha ukawa umepotezwa.Shetani ni mjanja sana,tangua agundue mmeshitukia waganga wa kienyeji sasa hivi ana watu wanakuwa kama watumishi wa Mungu lakini ni watumishi wake,injili inahubiriwa kwelikweli lakini kama unalijua neno utawagundua otherwise wengi wamekamatwa huko.
 
Nakubali ila Samweli aliamshwa akatoa unabiii
 
Unauhakika yule aliyeamshwa na mwanamke mwenye pepo la utambuzi alikuwa ni Samweli mtumishi wa Mungu?Hapa sitakuwa wazi ili tujifunze kitu na wengine wachangie kutokana na level za ufahamu wao.Hiyo habari ipo 1Samwel28:3-25, ukiwa unasoma ,soma kwa kutafakari zaidi ya mara moja 1Samweli28:6-7
 
@aqua si kila mmoja ni msomaji wa Bible ikikupendeza unaweza kuweka vifungu kamili....
 
Mshana Jr ni kweli nimefanya hivyo makusudi,lakini hiyo story ni kama imechukua sura nzima,kwa muda huu nikisema kesho nitakosea.Baadaye nitaweka vifungu vilivyo vifupi,ila nitakuwa kimya watu wachangie je aliyeamshwa na yule mwanamke ni Samweli wa ukweli mtumishi wa Mungu au janja ya shetani?Hapo tunamwitaji Roho mtakatifu atufundishe kwani yeye pia ni mwalimu.
 
Back
Top Bottom