Uwezo wa kuongea na wafu: Elimu Iliyoshindikana duniani

Nimepapenda "marehemu huwa hawataki dharau"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni sawa na kusema:-
1- Mwili ni Hardware
2- Nafsi ni Software
3- Roho ni Electricity (Power)
 
Umezungumzia kuhusu kuongea na wafu elimu iliyoshindikana duniani. Ukweli hii elimu haijashindikana, ipo! Ila ni elimu inayokutaka utoke kwenye ukawaida uliyo wa ukawaida.

Ni elimu ambayo haijikiti na mwili! Ni elimu ambayo inajikita na roho. Ni elimu ambayo ili uifikie inabidi ujikane wewe mwenyewe kwanza. Kwa sababu ulimwengu wa kuyashuhudia hayo si ulimwengu wa kimwili bali wa kiroho.

Wazee wa kale hawakuwa wakiwaita wafu bali ni viumbe vyengine vilivyokuwa na ukaribu A-Z na aliyefariki. Vile ndivyo vinavyokuja mbadala wa vile vilivyokufa na kukuaminisha kwamba ndiyo wao ila uhakika wa mambo si hao wafu ndiyo waliyokuja. Walijitambulisha kama mizimwi muda mwengine.

Uzi uliyonipa kama marejeleo hakikuwa ninachomaanisha. Ukiipata elimu ya kiriho ya inayokutaka kujikana mwenyewe utawaona na kugundua si kila aliyekufa amekufa!

Na ni wenye msaada mkubwa kwako pengine. Na pengine ndiye waliyokuwa walezi wako tangu ulivyozaliwa mpaka ulipofikia sasa pasipo wewe mwenyewe kujua.

Ni elimu iliyotoka kwenye ukawaida wa ubinadamu haieleweki kwa maelezo bali inaeleweka kwa vitendo.
 
Ni elimu iliyotoka kwenye ukawaida wa ubinadamu haieleweki kwa maelezo bali inaeleweka kwa vitendo.....
Asante kwa maarifa nimekupata vizuri sana
 
Mshana Jr Sasa Kama anakutokea kila siku inakuwaje na unapewa mjumbe mzito
 
Hii ngumu kidogo. Kma anaweza kataa nguo ina maana hubaki na mawasiliano katika ya nafsi, roho na mwili?
Hii nimeshuhudia live marehemu alikataa kuingia ndan ya jeneza!
Kisa kilipoanzia:
Muda wa kwenda kuchukua mwili umefika na jeneza lipo wakat huo marehemu amevalishwa vema.lile jeneza lililoletwa akaingizwa lakn shingo plus kichwa havikuenea
( Si Kama hawakumpima na vipimo vilifanyika)

Basi yule mtu wa mochuari akawaambia ndugu waliokuja kuchukua mwili ilibidi ku mmbembeleze kikwenu familia iwasiliane mambo yaende vema. Basi wakajipanga kwa kuvuta kumbukumbu na mtoto wa kwanza wa marehem wanapatana na marehemu akapigiwa simu na kuelezwa yaliotokea mochwar ,jaman tembea uone! Mtoto wa marehem akasema mpen simu marehem simu ikawekwa sikion ikiwa loud ( aliongea kwa kilugha chao tena Cha kumbembeleza)
Jeneza lilivokuja lingine maana walikwenda kubadili walihisi n dogo ijapo walimpima
Khe!, Marehem alitosha mpaka kupwaya na ndan kukabak kukubwa tu

Mpaka shughuli za mazishi zinamalizika walimtumia mtoto anaepatana na marehemu!.
 
Hiki kisa kimenisisimua ...haya ndio tunayokutana nayo mochwari na kwenye shughuli nyingi za wafu
 
Mshana jr hii imekaaje? mmemuwek vema marehemu Kama kumfunga mdomo lakn baada ya muda mnakuta meno yote yako nje mithili anacheka
 
Mshana jr hii imekaaje? mmemuwek vema marehemu Kama kumfunga mdomo lakn baada ya muda mnakuta meno yote yako nje mithili anacheka
Hiyo mara nyingi hutokea kwa wale marehemu wa vifo vya ghafla kama ajali au kuuliwa huku wakipambana wasife...
 
Hahahaha hii post jaman hahaha u made my day hahah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…