mshan jr;
Siamimi habari za mizimu kuwa rafiki ila najua ipo, na inafanya mengi tu. Kwetu tumezaliwa wengi kidogo. Mdogo wangu anayenifuata siku alipofariki ghafula niliona maajab.
Kwanza ilikuwa hivi; Jana yake tuligombana tukapigana ka watoto wafanyavyo. Kwa kuwa nilikuwa sikubali kupigwa na mdogo, nikamshikisha adab. Keshoye kafariki ghafula, japo si kwa kipigo changu kwani naye alinitwanga si kidogo. Ni kwa ugonjwa sikuujua kwani tulikuwa wadogo tu. Umri wa 12 kwa 10.
Cha ajab, usiku wa alipozikwa, nikiwa nimelala kitanda kimoja na baba mzazi, jamaa alikuja, akaniamsha, alianza kunipiga mangumi, mateke mpaka damu zikanitoka puani. Nikapiga yowe, baba akaamka ghafula, akawasha taa. Damu zinatiririka puani, kuuliza kisa nikamwambia kuwa ni jamaa alikuja akanipiga. Baba akaona kuwa ni ndoto. Akaamuru nilale.
Mara tukasikia hodi zinapigwa huko nje. Mama mdogo kamleta mdogo wangu mwingine kutoka kwake, ati alienda kupiga hodi huko anataka chakula. Alipoulizwa amekuja na nani usiku ule, akasema ni huyo jamaa alimfungulia mlango wa chumba cha mama yetu na kumleta huko ili wale chakula.
Je, ni ndoto au ni kweli? Mimi nasema ni kweli kwani nilimwona na alinipiga ngumi ya pua damu zikatoka. Believe it or not, this is a true story
Lakini hapo hebu nambie kuna hiz wanasema misukule yan unaligwa na unakufa gafla lakini kumbe hukufa, labda ukute mdogo wako alifanywa msukule maana misukule waga inasumbua sana, mzim na msukule ni vitu 2 tofaut kabisa,