Uwezo wa kuongea na wafu: Elimu Iliyoshindikana duniani

Uwezo wa kuongea na wafu: Elimu Iliyoshindikana duniani

ata mimi nakumbuka babu yangu alipofariki nilijikuta namwambia "BABU KUBARI TUKUSAFIRISHE KWENYE NYUMBA YAKO YA MILELE SALAMA" alifariki huku dar na tulikuwa tunasafirisha kuelekea huko singida saa ya kwenda tulisafiri salama tukazika salama ila kimbembe kilitokea muda wa kurudi tuligombana kwenye gari kufika dar kila mtu akashika njia yake bila maelewano na mwenzake....
Kuna kitu kisicho cha kawaida kilitokea huko msibani ambacho hakikumfurahisha marehemu
 
Japo mwili hutawanyika na kuwa kitu kisicho kamili lakini maneno yoyote ya marehemu hubebwa na roho na nafsi yake
Hizi habari za wosia si kitu cha kupuuza hata maramoja waliopuuza walipata habari yake mifano halisi ipo mingi kama marehemu alisema sitaki hivi na mkafanya tofauti baada ya yeye kufa maafa hutokea mara zote

Hii kitu iliwahi kuipata familia yangu Jamani mjomba wetu akiwa hai alisema Hata siku akifa hataki kusafirishwa kuzikwa kwao. Bahati mbaya aliyezungumza naye maagizo haya familia nzima inamdharau tu sijui Kwa sababu gani anadharaulika namna ile .
Mjomba akafa siku Hiyo Yule mjumbe akasema marehemu alisema azikwe popote atapofia kila mtu akasema lake na Kama kawaida maagizo yakapuuzwa utaratibu wa kusafirisha mwili ukaendelea. Kuipata laki TISA Kwa ajili ya usafiri ilichukua siku nne pesa hazitimii hadi gari walilotaka kusafirishia wakabwaga manyanga wakasema hawawezi kuuzuiwa Kwa siku nyingi hivyo .
Jamani hali ikawa ngumu kuweka msiba mjini siku nne jasho linawatoka wafiwa mwisho wazee wakasema bora kuzika hapahapa alipofia. Cha ajabu umati wa watu uli miminika siku ya mazishi michango ili tajwa Kwenye mrejesho ikifika mil 2.7 na marehemu alikuwa ni fundi ujenzi tu wa maisha ya chini kabisa. Mtu akikataa asifanyiwe kitu fulani akifa inabidi kuheshimu maana yanawakuta watu ni mengi mno.
 
kuna wakati mnachimba kaburi na kuuweka mwili na jeneza lake, udongo wote unaishia kaburini na kaburi likabaki nusu! halijai, udongo hautoshi, nyie achene tu, haya mambo yasikie kwa wengine......
 
Kaka umenifanya nifahamu mengi toka asubuhi napitia threads zako ulizowahi kupost.....yani ni mambo yaliyojificha sana ila tunayapata bure ata hatulipii ...japo yanatisha ila ndio ukweli wenyewe.....wanasema ukishamfahamu adui Hugo si adui tena....Big up
 
Duu yale ni mfano wa makaburi yamekaa kama ma toy ungeenda kinondoni au ungekuja msata
Ha ha ha haaaaa....wakuu lakini chini si wapo waheshimiwa wamepumzika kwa amani?
Huko Kinondoni na Msata ambapo ukikuta mtu tu kasimama nywele na mwili vinasisimka nani aende!!
Kile kituo cha kinondoni makaburini ikifika muda fulani abiria wenyewe hawaaminiani.
Hahaha wewe umeenda kwenye yale makaburi ya kinyangema makaburi yana bustari nzuri za maua zimefagiliwa na Pana pendeza kweli... Hata mimi ningeweza kwnda kulala kabisa
 
Ha ha ha haaaaa....wakuu akini chini si wapo waheshimiwa wamepumzika kwa amani?
Huko Kinindoni na msata ambapo ukikuta mtu yu kasimama nani aende!!
Kile kitu cha kinondoni makaburini ikifika muda fulani abiria wenyewe hawaaminiani.
Hahaha [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Mkuu Mshana unapenda sana hizi story sasa zitatusaidiaje humu kila saa kutishana tu mkuu
 
Mwanadamu anapofariki ubongo huwa wa mwisho kufa, huweza kuchukua mpaka masaa ma3 au zaid.
 
Mkuu Mshana unapenda sana hizi story sasa zitatusaidiaje humu kila saa kutishana tu mkuu
Mmh ukiingia kilabu cha pombe za kienyeji bila kulazimishwa halafu ukawauliza uliowakuta kuwa kwanini kila siku mnakunywa hii pombe watakushangaa sana kisha watakuona wa ajabu mno
 
Unajua ni kama software kubwa sana haizimi kama bulb ya Wat 10
Haswaaaa ila sijajua inakua vipi naskia maiti inaweza kufumbua jicho kisha ikafumba. Hapa inakuaje?

Au kuna maiti nyingine zinaleta utata wakati wa mazishi ni vihoja vitupu.

Katika uzoefu wako wa miaka mi3 umeshuhudia hayo?
 
Haswaaaa ila sijajua inakua vipi naskia maiti inaweza kufumbua jicho kisha ikafumba. Hapa inakuaje?

Au kuna maiti nyingine zinaleta utata wakati wa mazishi ni vihoja vitupu.

Katika uzoefu wako wa miaka mi3 umeshuhudia hayo?
Vituko na vibweka vya maiti ni vingi mno hasa zile ambazo vifo vyake ni
Vya ghafla
Vya mateso
Vya kisasi nk nk
 
Mshana naomba ushauri wako.Je ni weza kumuomba msamaha marehemu ambaye nilimkosea akiwa hai na ameshazikwa?Kama hilo linawezekana je anatakiwa awe ameshaishi kaburini kwa muda gani ndio bado anaweza kuwasiliana nami?
 
Mshana naomba ushauri wako.Je ni weza kumuomba msamaha marehemu ambaye nilimkosea akiwa hai na ameshazikwa?Kama hilo linawezekana je anatakiwa awe ameshaishi kaburini kwa muda gani ndio bado anaweza kuwasiliana nami?
Hakuna muda maalum ndio maana mpaka leo hii Kuna ibada ma matambiko makaburini kwa ajili ya mambo kama hayo
Naamini una wazee wa kimila na kikabila wanaweza kukupa mwongozo kulingana na tamaduni mila na desturi za kabila lenu
 
mshana jr sasa nakuuliza swali ambalo hujaulizwa kabsa humu plz usinijibu kama wa saaa swali langu ni hivi je marehemu au mzimu wake huchukia au huumia au kupata wivu endapo mke/mme alomuacha akaolewa/kuona au kuwa na mtu mwingine hii ni kwa faida ya wajane wote
 
mshana jr sasa nakuuliza swali ambalo hujaulizwa kabsa humu plz usinijibu kama wa saaa swali langu ni hivi je marehemu au mzimu wake huchukia au huumia au kupata wivu endapo mke/mme alomuacha akaolewa/kuona au kuwa na mtu mwingine hii ni kwa faida ya wajane wote
Hapa kuna ndio na hapana
1. Ndoa ni mkataba wa watu wawili wasio ndugu wa jinsia mbili tofauti na ambao wamevuka miaka 16 kuishi pamoja kama mke na mume baada ya kuendana kwa kweli na kwa dhati....
Kama mapenzi yao yakidumu hadi uzeeni hata mmoja anapotangulia mbele za haki huyu mwingine aliye hai hawezi kuwa na mwingine si kwa masharti wala maagano bali ni mapenzi ya dhati
2. Shida hutokea kwa wale walioingia kwenye maagano ya viapo na yamini ya kutokuwa na mwingine hata baada ya kifo.... hapa kitakachofanya kazi sio ile roho ya marehemu bali ile roho ya maagano mliyojiundia
3. Kuna watu hufa huku wanawapenda na kuwajali wenza wao lakini kumbe hao wenza rohoni wana lao jambo na hawana mapenzi kabisa. kwa sababu zozote zile kuna nguvu ndio itakayoamua kufanya kazi positively au negatively
4. Kuna wale ambao hufanya mipango ili wenza wao wafe na wao warithi mali na wapenzi wao ya hawa huwa hawadumu roho ya kisasi huwaandama
Mwisho roho ya marehemu haina wivu nk kwakuwa ngono ni matendo ya kuridhisha hamu za mwili uozao
 
Back
Top Bottom