pulex
JF-Expert Member
- Nov 3, 2023
- 536
- 2,213
TOP ya Maraisi kulingana na uwezo wao:
1. Nyerere
Alitumia akili nyingi kutupatia uhuru bila kumwaga damu, aliongea vitu vingi ambavyo vingine vinatokea sasa, uzalendo usiokuwa na mashaka, nchi aliunganisha kwa makabila yote na kupatikana mswahili na pia alijua ni lazima atoke madarakani ili awe mfano kwa wanaokuja asitokee mtu akakalia kiti hadi Kufa. Kosa lake aliamini Ujamaa sana na hvyo Tanzania ikachelewa kimaendeleo.
2. Magufuli
Kiongozi aliyekuwa anajua ugonjwa wa TZ uko wapi, na nini kufanyike ili kuleta maendeleo, alikuwa na maamuzi magumu ambayo mtu unaweza usimuelewe muda huo ukaja kumuelewa baadae, alikuwa mzalendo aswaa, alijua jinsi kuifanya Tanzania ijiletee maendeleo kwa namna ambayo kila mtu aliona haiwezekani, alikuwa na uwezo kuhifadhi vitu kichwan na akavitoa kwa namna ambayo hata mtu bongo lala unamuelewa na mwisho alikuwa yuko vizuri kwenye namba (mathematician). Udhaifu wa Magufuli likitokea kosa, na watu wakamsema ilikuwa ngumu kubadili mawazo yake maana aliamini akibadili atakuwa ameonesha hana msimamo au ishara ya udhaifu mfano ile sakata la Paul Makonda.
3. Mkapa
Alikuwa Rais ambaye aliweza kutumia ufinyu wa taarifa alizonazo kuleta maendeleo, alikuwa anajua kipaji cha mtu kwnye uongozi na kumtumia vyema, ni mzalendo. Udhaifu wake ulikuwa ni kwenye kuamini taarifa zisizo kamilika na kufanya maamuzi mfano la ubinafsishaji viwanda.
4. Mwinyi
Alijua kuwa ujamaa unaturudisha nyuma, na alifungua nchi sana ikiwemo kuiweka karibu na nchi za magharibi, ndo kipindi chake teknolojia mpya zilianza kumiminika kwa wingi Tanzania. Udhaifu wa Mwinyi ulikuwa ni kukosa misimamo, mvivu, na kuruhusu kutaliwa kimaamuzi, japo alikuwa na uwezo mzuri wa kujua hapa mekosea na kujisahihisha, alikuwa ana heshimu watu asa mawazo ya mwalimu pale akifokewa, hakuwa na kiburi cha madaraka, au kisasi.
5. Kikwete
Kikwete alikuwa na uwezo wa kuwaadaa watu, na kupendwa, ana uwezo mkubwa wa unafki japo alikuwa anajua kucheza na wapinzani wake na upinzani ulistawi sana kipindi chake. Makashfa mengi ya ufisadi na rushwa yalifumuka sana kipindi chake, na kurasa za watu wasiojulikana zikaaza kama kutekwa kwa akina Dr ulimboka.
6. Samia
Ndio Raisi wa ajabu kutokea Tanzania maana sioni hata zuri moja la kuliweka, aliingia kwa kupendwa ila amekuja kuchukiwa mno kwasababu ameachia nchi wengine "wamsaidie kuongoza". Utekaji, usifisadi na uuaji umeshamili, upinzani kudidimizwa, uchu wa madaraka, na makashifa mengi, uzalendo sifuri, Mwepesi wa kudanganywa pale maovu yakitokea, anashauriwa tofauti na wanaomzunguka na anaulinda uovu huo.
Nyingine ongezeni wenyewe.