Uwezo wa raia kununua/kufanya manunuzi umeshuka

Uwezo wa raia kununua/kufanya manunuzi umeshuka

JF Member

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2014
Posts
7,914
Reaction score
10,793
Ni wakati mgumu sana kwa wafanya biashara; purchasing power ya wananchi imeshuka mno.

Pesa inaenda moja moja serikalini bila kupitia kwa wafanya biashara

Tozo ni laana kali Sana. Wachumi fanyani kazi yenu la sivyo kila kitu itasimama. Hakuna tena kuzungusha hela ni kulipa Tozo tu.

Wenye vibanda vya mpesa wengi wamefunga. Wamachinga Hari ni ngumu. Mitaji inakufa. Kila mtu analia..N.k
 
Ni wakati mgumu sawa kwa wafanya biashara; purchasing power ya wananchi meshuka mno.

Pesa inaenda moja moja serikalini bila kupitia kwa wafanya biashara; Tozo ni laana kali Sana. Wachumi fanyani kazi yenu la sivyo kila kitu kitasimama.
Wafanye nani,wachumia tumbo tuwajuao au wachumi huru wenye taaluma yao.
 
Uko sawa kabisa. Nichukue mfano wa hapa Mwanza. Hapa Mwanza siku ya Jumatatu, Jumanne na Jumatano mitaa ya Nyerere, Rwegasore, Liberty mitaa hiyo inajaa wafanyabiashara wanaotoka vijijini kuja kununua bidhaa na kurudi vijijini na mtu hupati hata mahali pa kutia mguu kutokana na utitiri wa watu. Leo hii tembelea mitaa hiyo, hakuna wafanyabiashara kama zamani ni wachache sana na maduka mengi yanafungua na kufunga jioni bila hata kuuza bidhaa. Hii inaonyesha dhahiri kuwa uwezo wa wananchi kununua bidhaa kwa ajili ya matumizi yao umepungua hata kwa asilimia 70. Wachumi tunao na hili hawalioni.
 
Ni wakati mgumu sana kwa wafanya biashara; purchasing power ya wananchi imeshuka mno.

Pesa inaenda moja moja serikalini bila kupitia kwa wafanya biashara;
Tozo ni laana kali Sana. Wachumi fanyani kazi yenu la sivyo kila kitu itasimama. Hakuna tena kuzungusha hela ni kulipa Tozo tu.

Wenye vibanda vya mpesa wengi wamefunga. Wamachinga Hari ni ngumu. Mitaji inakufa. Kila mtu analia..N.k
RRONDO
 
Wafanye nani,wachumia tumbo tuwajuao au wachumi huru wenye taaluma yao.
Watu Wana furahi kuongeza mapatato tu bila kujua mamma ya kutengeneza. Kuna ombwe la uongozi hii nchi.

Serikalini imefeli pakubwa na sijui itajinasuaje!
 
Yaani ni kwamba, unafika ofisini, una subiri wateja, wateja hawaji, unajiinamia kwa kiti, using izi unakupitia, una amka mwenyew bila kuamshwa labda na mteja, yaani njaa inakuuma, unakopa kwa mama ntilie, ukidhani labda atakuja ata mteja mmoja ijapo upate cha Kimlipa mama ntilie lkn wapi NG yangu?
Jaman kama vyuma kukaza Basi vimekaza zaidi yaani,
Maduka ya Akina mangi kitaa hawauzi mafuta ya kupikia sasa hivi, wanasema bei ipo juu, hamna faida
 
Hii hali ilianza tangu kipindi cha jiwe, kwa sasa ni mwendelezo wa hali mbovu ya uchumi wa mtu mmoja mmoja tokea jiwe aingie madarakani na ku implement austerity policies....
 
Serikali yeyeto inayovuta bange upenda kuumiza watu wake.
 
Back
Top Bottom