Uwezo wa Watanzania Ma CEO Makampuni ya Kimataifa, Je Tunao?, Tuna Uwezo?. Big Up Helios Towers, Kuing’arisha Tanzania, Fursa kwa Watanzania!

Uwezo wa Watanzania Ma CEO Makampuni ya Kimataifa, Je Tunao?, Tuna Uwezo?. Big Up Helios Towers, Kuing’arisha Tanzania, Fursa kwa Watanzania!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na kwa maslahi ya taifa.

Mara yangu ya kwanza kutinga New York, kutembelea Makao Makuu ya UN, nilitembezwa sehemu mbalimbali za UN, huku nikitambulishwa kwa staff wa UN ambao ni Watanzania, ukiondoa UN Radio, huko kuingine kote Watanzania ni wa kutafuta kwa tochi, wenzetu Wakenya, Waganda na Wasomali kibao!, nikamuuliza mwenyeji wangu, kwa nini Watanzania ni wachache compared na majirani zetu?.

Ndipo akanieleza, UN wanaajiri kwa quota system, Tanzania iko kwenye kundi la East Africa & The Horn of Africa, akasema Watanzania hawa apply UN kila zinapotokea job openings, na wachache wanao omba they can't compete, hivyo wenzetu wanatushinda. Nikajiuliza ni hatuna uwezo au ?.

Nikafarijika kukutana na Binti mmoja ni Mtanzania Mzanzibari ni meneja City Bank New York, nikaja kukutana na binti mwingine Mtanzania, binti wa Kitanga, ni Meneja Standard Chartered Bank London, ila sijabahatika kukutana na Watanzania ma CEO wa makampuni ya Kimataifa.

Juzi kati nikiwa Arusha, ndipo nikakutana ni kampuni hii ya Helios Towers!.

Tuige Kampuni ya Helios Towers, Yaing’arisha Tanzania, Kitaifa, Kiafrika na
Kimataifa, Huku Watanzania Waking’ara Yaudhamini Mkutano wa Kimataifa wa Connect 2 Connect (C2C) Afrika, Watanzania ni Wazuri, Sijui Tunakwama Wapi Kushika Usukani?, ni hatuna watu wenye uwezo huo, au watu tunao ila hawana uwezo, au watu tunao, wana uwezo ila wanabaniwa?,

Nchi yetu ya Tanzania, ni nchi iliyobarikiwa sana na Mungu, ina watu wakarimu, watulivu na wasio na fujo na vurugu, ina ardhi kubwa ya kutosha yenye udongo wenye rutuba kuotesha kila aina ya mazao ya chakula na biashara kuweza kulisha Afrika na dunia, lakini kitu cha ajabu ni tunaagiza vyakula kutoka nje na vingine vinatoka kwenye vinchi vidogo ambavyo havina kitu ukilinganisha na sisi!.

Tanzania tuna vyanzo vingi vya maji, mito,vijito, maziwa na chemchem kuweza kuendesha schemes za kilimo cha umwagiliaji, lakini kitu cha ajabu Tanzania, kilimo chetu ni kilimo cha kutegemea mvua, badala hata kuvuna hayo maji ya mvua kwa kujimba mabwawa, na kulima mwaka mzima!.

Tanzania ndio nchi inayoongoza duniani kwa kivutio kikubwa kabisa cha Utalii, Mbuga ya Serengeti, na kwa Afrika tuna vivutio vingi na vizuri vya asili kuliko nchi zote!, lakini kitu cha ajabu, ukiangalia idadi ya watalii, wanaotembelea Tanzania ulinganishe na nchi nyingine ambazo hazina hata nusu ya tulichonacho, utaishia kushangaa!, eti Tanzania ni ya 5 kwenye top ten ya nchi zinazotembelewa na watalii wengi! Africa, , tumepitwa na Kenya!, nusu ya watalii wa Kenya wanakuja kupanda mlima Kilimanjoro!, Kenye inautangaza zaidi kuliko wenye mlima wenyewe!

Tanzania tunayo madini mengi na ya thamani, mfano madini ya Tanzanite, yanapatikana nchi Tanzania pekee, lakini ukiangalia urari wa mauzo ya Tanzanite kwenye soko la dunia, Tanzania ni nchi ya 4 kuuza Tanzanite, nchi ya kwanza ni India, nchi ya pili ni Africa Kusini, ya tatu ni Kenya, ya nne ndio Tanzania!, mtu unajiuliza kama Tanzanite zinaptikana Tanz ania pekee, hao India, Afrika Kusini na Kenya, hizi Tanzanite wanazoziingiza kwenye soko la dunia, wanazitoa wapi?!.

Tanzania ni nchi ya tatu kwa utajiri wa dhahabu Afrika ikitanguliwa na Ghana na Afrika Kusini, na ni nchi ya 16 duniani, Tuna migodi lukuki, ukiondoa mgodi mmoja tuu wa Stamigold, kule Biharamulo, unaomilikiwa na Stamico, migodi mingine yote inamilikiwa na wageni, na ukifika migodini, wazungu wanapishana, menejimenti zote ni wazungu, na kuna baadhi, kuna Watanzania wachache wa kuzugia tuu!.

Sasa tumegundua gesi asili, tunauza vitalu vya gesi kwa mnada, kianzio ni dola milioni moja, mpaka sasa tuna mikataba (PSA) 21 ya gesi asili, kitu cha ajabu ni hakuna hata kampuni moja ya Kitanzania wala ya Kiafrika, zote ni za Wazungu, na sijabahatika kumsikia Mtanzania yeyote ni top executive kwenye makampuni ya gesi!.

Hali hii ni tofauti kwa Kampuni ya kwanza ni Total Energies, na sasa kampuni ya Helios Towers, inayoongoza kwa miundombinu ya mawasiliano kwa njia ya minara, imepongezwa kwa kuing’arisha Tanzania kitaifa, Afrika na kimataifa, kulikopelekea kuuvutia mkutano wa 8 wa Connect 2 Connect (C2C) Afrika 2024, kuja kufanyikia Tanzania, Helios akiwa ndie mdhamini mkuu wa mkutano huo ulianza uliofanyika kwa siku mbili katika Hoteli ya Gran Melia jijini Arusha na unaratibiwa na kampuni ya Extensia Limited, kwa ushirikiano na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Tanzania.

Kilichonigusa kuhusu hii Helios, japo ni kampuni ya Uingereza, na iko kwenye nchi 9, kati ya hizo,nchi 8 ziko barani Afrika na
nchi moja ya Oman iko Arabuni, The Top Boss wa Helios Tanzania, yaani Mkurugenzi Mtendaji wa Helios Towers Tanzania na Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki ya Afrika, ni Mtanzania, Gwakisa Stadi, kati ya hizo nchi 8 za Afrika ambazo Hellios wapo, mabosi wa nchi 3 ni Watanzania!, na kitu kizuri kuhusu sisi Watanzania, hata top boss wa kwanza kuanzisha Helios ya Oman ni Mtanzania!.

Huu ni uthibitisho Watanzania wana uwezo wa kushika nafasi za juu za kimataifa kama wakijengewa uwezo!, kama kwenye Helios Watanzania wameweza, huko kwingine, tunashindwa nini?.

Kitu kizuri kuhusu menejimenti za Helios, wakati sehemu nyingi wanawake wakiwekwa nyuma na sehemu nyingine ni wa kutafuta kwa tochi, menejiment ya Helios Tanzania kwenye usawa wa kijinsia, yaani gender balance ni 50/50.

Kitu kingine kizuri kuhusu Helios, kila kwenye mnara wa Helios, jamii husika hufaidika kwa kupatiwa misaada ya kijamii, mfano baada ya mkutano, menejiment ya Helios ikiongozwa na Gwakisa Stadi, walikwenda kutoa msaada wa chumba cha kompyuta shule ya sekondari ya jamii ya Wafugaji ya Endevesi, iliyoko Oljoro na kutoa msaada wa compyuta 28.

Kampuni ngapi za kibiashara zinafanya biashara vijijini, mfano migodini wanaishi kama peponi, vijiji jirani kwanini wanaishi kama jehanum kwenye lindi la umasikini uliotopea, wakati hiyo dhahabu inayovunwa ni yao?, kwa waliofika Mwadui enzi za Williamson Diamond, na vijiji vya jirani!, Waliofika Geita enzi za GGM na vijiji jirani, Gesi ya Mtwara, Bomba la Mafuta la Lindi, na vitegauchumi lukuki vya uwekezaji, kwanini wasiinge mfano wa Helios Towers?. Kampuni nyingine ya kimataifa inayowajali Watanzania ni TotalEnergies Marketing Tanzania Limited, meneja wa TotalEnergy Kenya ni binti wa Kitanzania!.

Na kuhusu huu mkutano wa C2C, Mkurugenzi Mtendaji wa Helios Towers Tanzania na Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki ya Afrika, Gwakisa Stadi, amesema Mkutano wa C2C Afrika ni tukio la kipekee katika sekta ya mawasiliano, likiwaleta pamoja wakurugenzi waandamizi, na viongozi wa katika sekta ya mawasiliano kujadili, fursa, na changamoto zinazokabili sekta ya tehama barani Afrika.

Gwakisa Stadi alisema: "Kama mdhamini mkuu wa Mkutano wa C2C Afrika kwa mwaka huu, kampuni ya Helios Towers inajivunia kuchangia katika mazungumzo yatakayounda mustakabali wa uunganishaji barani Afrika. Tunaamini kuwa miundombinu ya mawasiliano yenye nguvu, endelevu, na inayoweza kupanuka ni ufunguo wa kufungua uwezo wa kidijitali wa kanda hii. Natarajia kushirikiana na viongozi wenzangu wa sekta tunapofanya kazi pamoja ili kuendeleza mabadiliko ya kidijitali na kuunda matokeo chanya ya muda mrefu katika eneo la Afrika ya Kusini mwa Jangwa la Sahara.”

Helios Towers ni kampuni inayoongoza katika miundombinu ya mawasiliano yenye idadi kubwa zaidi ya minara barani Afrika na Mashariki ya Kati. Kampuni hii inaratibu ufanisi wa kushirikiana miundombinu na makumpuni ya mitandao ya simu (MNO) ili kufanikisha upatikanaji wa mitandao ya simu kwa haraka, kwa gharama nafuu na kuzingatia utunzaji wa mazingira kwa kupunguza matumizi ya alama za kaboni (carbon footprint). Hii kwa upande wake inasaidia upanuzi na ubora wa mawasiliano kwa njia ya simu, ikichochea maendeleo endelevu katika masoko yake.

Big Up Sana, Helios Tower kwa kuonyesha njia, wengine wafuate!.

Wasalaam

Paskali.
 
Nawapongeza. Ila mkuu ungejikita kuelezea huo mkutano ulioandaliwa na Helios bila kuzunguka sana. Kama lengo ilikuwa kuielezea Helios na mkutano wao basi utakuwa umefikisha ujumbe kwa namna ngumu sana.
 
Tuige Kampuni ya Helios Towers, Yaing’arisha Tanzania, Kitaifa, Kiafrika na
Kimataifa, Huku Watanzania Waking’ara Yaudhamini Mkutano wa Kimataifa wa Connect 2 Connect (C2C) Afrika

Mkuu Helios Towers sio kampuni ya kitanzania bali wanaoperate Tanzania kwa jina la Helios Towers Tanzania (HTT) aka HTT Infranco...

Wana market share kubwa Tanzania na DRC kwa Africa lakini wapo nchi kadhaa kama Malawi, Madagascar, Congo B, Senegal, Ghana etc, huku target yao ni Africa na Middle East...

HQ ya Helios Towers ipo London na huko ndipo iliposajiliwa...
 
Uwezo wa Watanzania Ma CEO Makampuni ya Kimataifa, Je Tunao?, Tuna Uwezo?. Big Up Helios Towers, Kuing’arisha Tanzania, Fursa kwa Watanzania!.​

Subscribe
•••
[IMG alt="Pascal Mayalla"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/17/17813.jpg?1493942121[/IMG]

Pascal Mayalla

Platinum Member​

Wanabodi,
Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na kwa maslahi ya taifa.

Mara yangu ya kwanza kutinga New York, kutembelea Makao Makuu ya UN, nilitembezwa sehemu mbalimbali za UN, huku nikitambulishwa kwa staff wa UN ambao ni Watanzania, ukiondoa UN Radio, huko kuingine kote Watanzania ni wa kutafuta kwa tochi, wenzetu Wakenya, Waganda na Wasomali kibao!, nikamuuliza mwenyeji wangu, kwa nini Watanzania ni wachache compared na majirani zetu?.

Ndipo akanieleza, UN wanaajiri kwa quota system, Tanzania iko kwenye kundi la East Africa & The Horn of Africa, akasema Watanzania hawa apply UN kila zinapotokea job openings, na wachache wanao omba they can't compete, hivyo wenzetu wanatushinda. Nikajiuliza ni hatuna uwezo au ?.

Nikafarijika kukutana na Binti mmoja ni Mtanzania Mzanzibari ni meneja City Bank New York, nikaja kukutana na binti mwingine Mtanzania, binti wa Kitanga, ni Meneja Standard Chartered Bank London, ila sijabahatika kukutana na Watanzania ma CEO wa makampuni ya Kimataifa.

Juzi kati nikiwa Arusha, ndipo nikakutana ni kampuni hii ya Helios Towers!.

Tuige Kampuni ya Helios Towers, Yaing’arisha Tanzania, Kitaifa, Kiafrika na
Kimataifa, Huku Watanzania Waking’ara Yaudhamini Mkutano wa Kimataifa wa Connect 2 Connect (C2C) Afrika, Watanzania ni Wazuri, Sijui Tunakwama Wapi Kushika Usukani?, ni hatuna watu wenye uwezo huo, au watu tunao ila hawana uwezo, au watu tunao, wana uwezo ila wanabaniwa?,

Nchi yetu ya Tanzania, ni nchi iliyobarikiwa sana na Mungu, ina watu wakarimu, watulivu na wasio na fujo na vurugu, ina ardhi kubwa ya kutosha yenye udongo wenye rutuba kuotesha kila aina ya mazao ya chakula na biashara kuweza kulisha Afrika na dunia, lakini kitu cha ajabu ni tunaagiza vyakula kutoka nje na vingine vinatoka kwenye vinchi vidogo ambavyo havina kitu ukilinganisha na sisi!.

Tanzania tuna vyanzo vingi vya maji, mito,vijito, maziwa na chemchem kuweza kuendesha schemes za kilimo cha umwagiliaji, lakini kitu cha ajabu Tanzania, kilimo chetu ni kilimo cha kutegemea mvua, badala hata kuvuna hayo maji ya mvua kwa kujimba mabwawa, na kulima mwaka mzima!.

Tanzania ndio nchi inayoongoza duniani kwa kivutio kikubwa kabisa cha Utalii, Mbuga ya Serengeti, na kwa Afrika tuna vivutio vingi na vizuri vya asili kuliko nchi zote!, lakini kitu cha ajabu, ukiangalia idadi ya watalii, wanaotembelea Tanzania ulinganishe na nchi nyingine ambazo hazina hata nusu ya tulichonacho, utaishia kushangaa!, eti Tanzania ni ya 5 kwenye top ten ya nchi zinazotembelewa na watalii wengi! Africa, , tumepitwa na Kenya!, nusu ya watalii wa Kenya wanakuja kupanda mlima Kilimanjoro!, Kenye inautangaza zaidi kuliko wenye mlima wenyewe!

Tanzania tunayo madini mengi na ya thamani, mfano madini ya Tanzanite, yanapatikana nchi Tanzania pekee, lakini ukiangalia urari wa mauzo ya Tanzanite kwenye soko la dunia, Tanzania ni nchi ya 4 kuuza Tanzanite, nchi ya kwanza ni India, nchi ya pili ni Africa Kusini, ya tatu ni Kenya, ya nne ndio Tanzania!, mtu unajiuliza kama Tanzanite zinaptikana Tanz ania pekee, hao India, Afrika Kusini na Kenya, hizi Tanzanite wanazoziingiza kwenye soko la dunia, wanazitoa wapi?!.

Tanzania ni nchi ya tatu kwa utajiri wa dhahabu Afrika ikitanguliwa na Ghana na Afrika Kusini, na ni nchi ya 16 duniani, Tuna migodi lukuki, ukiondoa mgodi mmoja tuu wa Stamigold, kule Biharamulo, unaomilikiwa na Stamico, migodi mingine yote inamilikiwa na wageni, na ukifika migodini, wazungu wanapishana, menejimenti zote ni wazungu, na kuna baadhi, kuna Watanzania wachache wa kuzugia tuu!.
 
hata top boss wa Helios ya Oman ni Mtanzania!
Close
jadawy-al-riyamy.jpg

Jadawy Al Riyamy​

MD Helios Towers Oman
Joined 2021
Jadawy Al Riyamy
was appointed Managing Director of Helios Towers Oman in July 2023. Prior to this, Jadawy had held the position of Middle East Business Development Director at Helios Towers since February 2022, successfully engaging customers across the Middle East and supporting the acquisition Omantel’s tower assets as part of Helios Towers’ first expansion into the region.
Jadawy is an experienced Technical and Management Professional with a track record of over 20 years of success in overseeing and delivering strategic projects. He has worked for Emirates Airlines, Motorola, and consulted on Technical Services delivery industries. He attended the University of Strathclyde for his undergraduate engineering degree in Electrical and Electronics Technology and also holds a Masters Certificate from George Washington University in Project Management
 
Asante sana kwa ujumbe mzuri.

Tatizo letu Tanzania ni ubinafsi, ukienda mahali popote duniani ambapo yupo mtanzania sio rahisi kumpa ushirikiano ama fursa mtanzania mwenzie.

Mimi nakuahidi nitakuwa mmoja wa wafanyakazi wa UN anayewakilisha Tanzania.
 
Pascal Mayalla Tanzania ina vijana wengi Wazuri tuu. Ila wanaharibika wakishapata teuzi za CCM….wewe fanya utafiti utagundua😂😂😂😂😂😂😂😂
Waoga sana kufanya kazi nje ya mfumo wa mwamvuli wa chama dola kongwe. Wanaambiwa nje hakuna amani, Tanzania ni shwari wasiende nje kuna changamoto nyingi.
 
Back
Top Bottom