Ave Ave Maria
JF-Expert Member
- Apr 22, 2011
- 10,707
- 5,678
Pole sana. Lkn kilichojificha ndani ya kuvunja vitu ni kasoro kubwa na kielelezo cha ROHO MBAYA. Yaani Tukose wote na hao watoto wasifaidi. Hakuna sababu ya kuuma maneno, huyo mtu hawezi kuwapokea hao watoto, na wakirudi kwa baba yao ni mateso mtindo mmoja. Kadri mnapozungumza kupatana, suala la kuvunja vyombo liwe sehemu ya mjadala, msiliweke kando eti ni HASIRA.
Nina girlfriend wangu ambaye amekuwa ni mchumba wangu ila huenda kuanzia sasa uchumba umeisha baada ya kugundua kuwa nimemdanganya.
Nilipokuwa chuo nilizaa na wanawake wawili tofauti si unajua tena mambo ya ushamba.
Baada ya kupata kazi nikapata mchumba ambaye ndiye huyu sasa. Tuna mwaka mmoja na nusu na kwa kipindi hicho chote sikuwahi kumweleza kuwa nina watoto wawili. Yeye alikuwa anajua kuwa ninao wawili. Moto wake si mdogo, kavunja vyombo vyote kabatini, kavunja dressing table, kavunja coffee table yaani ni kasheshe, binti kapandisha majini ya kichaga. Najaribu kumtuliza hatulii, naombeni mnisaidieni kwani nampenda sana na ninamuhitaji maishani na sikupanga kumuumiza moyo
kwahiyo alipokuwa akifanya uvunjaji no mizuka ya ngoma ndio iliyokuwa imepanda? Maana pwani na ngoma ni kama kwapa na jasho.katika vitu nisivyopenda ni kudanganya (uongo ni mbaya sana) imagine wewe ndo ungekuwa yeye ...nadhani kama ulivyosema kweli we bado mshamba.. halafu sidhani kama huyo atakuwa mchaga ..Most of them niwastaarabu (kuvunja dressing table sijui na makofii olomide ) 🙂 sijui lakini but huwa ni wastaarabu na huwa wanaresolve issue smoothly...inawezekana ni wa pwani pwani Msoga msoga hivi
Bw Mikela.
Pole sana bana.
ila, Umenishangaza uliposema kuzaa na wanawake wawili tofauti ni mambo ya kishamba? Kivipi?
Are you ashamed of your kids??? Mimi na machache ambayo huenda yakakusaidia nawe kujiuliza ilikuwaje.
...nakushauri mpe muda atulie. Hakuna justification yeyote yeye kuvunja vitu ndani kwako, hata kama
- je, aliwahi kukuuliza una watoto?
- uliwahi kumwambia una mtoto mmoja, si wawili?
- je, (unahisi/inawezekana?) una watoto wengine zaidi ya hao wawili?
ni yeye alivilipia kununua.
Pamoja na kwamba unampenda na unamuhitaji sana maishani,
Hasira aliyokuonyesha kwa kuvunja vunja samani kwenye nyumba yako ni ishara mbaya sana huko mbele ya safari.
...mpe muda. Akishatulia kaeni chini muambiane UKWELI.
Duniani hakuna mkamilifu bana, hata naye atakuwa na 'tofali' lake bana,
Jiandae tu jinsi ya kulipokea 'kichwani mwako.'
The guy is crazly in love ndio maana amechukulia kuvunjiwa vitu positively. Mkishakaa miaka kumi akakuvunja vioo vya gari ndio utajua mziki wake. Ila umesema hutegemei kumuuzi tena kwa hiyo hatavunja vitu tena. Muombe Mungu akusaidie usimamie usemi wako, kwani maudhi hayapangwi utokea. Well hiyo tabia ya kuvunja vitu sidhani kama ina uhusiano wowote na binti kuwa mwaminifu au siyo muaminifu. Ni ukorofi full stop!
Nyumba Kubwa, maneno mazito sana hayo.
...waliosema LOVE IS BLIND hawakukosea kabisa.
Marriage Is An Eye Opener kwa waheshimiwa kama Ndugu yangu Bw Mikela.
Mikela tupe updates, muda huu bibie wako kisha anza kuezua mapaa au ndio anang'oa geti?
Mpaka ugomvi uishe nyumba yenu itakuwa kama imepigwa bomu.
da! hii kali...lol,
maisha yenyewe yanavyobana kiasi hiki,
halafu unakuwa na mume/mke mwenye hasira hizi,
siku ukimuudhi tu basi kila kitu kinavunjwa,
halafu hasira zikiisha mnaanza tena kupanga bajeti ya ,
kununua upya vitu vilevile upya,
Tena bora akiishia vitu tu vya ndani je akiwasha mto nyumba??,
bora iwe ya kwenu, na je kama ya kupanga???,
patakuwa patamu hapo...lol
Mikela tupe updates, muda huu bibie wako kisha anza kuezua mapaa au ndio anang'oa geti?
Mpaka ugomvi uishe nyumba yenu itakuwa kama imepigwa bomu.
hahahhaahha nimecheka saaaaaaaaaaaaaana,ubarikiwe lol