Uwongo umeniponza

Uwongo umeniponza

Pole mwaya. Ktk mapenzi bana hakuna ki2 kinachouma ka kusalitiwa au kumpoteza umpendaye. Nakusihi ucchoke kumbembeleza na uckubali kumpoteza kirahisi. Mwambie kuwa unampenda na bado unamhitaji na kitendo cha kuwa nae ni ishara tosha kuwa umemchagua yeye. Kubali kuwa umemkosea na unachohitaji sasa hivi ni msamaha wake tu ili penzi lenu liendelee. Hizo ni hasira tu zikiisha naamini atakuelewa. Jitahidi kuwa mpole na u2mie kauli nzuri la sivyo utamkosa na mapenzi ya cku hzi yalivojaa gelesha, mmh....!
 
Hata mimi nina mashaka hata akikusamehe kama hao watoto atawakubali toka rohoni. Otherwise waendelee kukaa kwa mama zao asijekukutesea watoto.

Pole sana. Lkn kilichojificha ndani ya kuvunja vitu ni kasoro kubwa na kielelezo cha ROHO MBAYA. Yaani Tukose wote na hao watoto wasifaidi. Hakuna sababu ya kuuma maneno, huyo mtu hawezi kuwapokea hao watoto, na wakirudi kwa baba yao ni mateso mtindo mmoja. Kadri mnapozungumza kupatana, suala la kuvunja vyombo liwe sehemu ya mjadala, msiliweke kando eti ni HASIRA.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Mama wa kambo si mama. Hao wanao mbona watakiona cha mtema kuni? Bora wapeleke huko milimani wakalelewe na bibi yao kuliko kuwaleta hapo nyumbani kwako. Watakufa kifo cha fedheha.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
katika vitu nisivyopenda ni kudanganya (uongo ni mbaya sana) imagine wewe ndo ungekuwa yeye ...nadhani kama ulivyosema kweli we bado mshamba.. halafu sidhani kama huyo atakuwa mchaga ..Most of them niwastaarabu (kuvunja dressing table sijui na makofii olomide ) 🙂 sijui lakini but huwa ni wastaarabu na huwa wanaresolve issue smoothly...inawezekana ni wa pwani pwani Msoga msoga hivi ...any way umefanya kosa kubwa sana ungetakiwa kumwambia ukiwa na confidence wakati wa mwanzo kabisa kama lijali halisi (usiogope kutoswa kwa kusema ukweli wako) japo kutoswa siku hizi si saaana kivile ...
 
Nina girlfriend wangu ambaye amekuwa ni mchumba wangu ila huenda kuanzia sasa uchumba umeisha baada ya kugundua kuwa nimemdanganya.
Nilipokuwa chuo nilizaa na wanawake wawili tofauti si unajua tena mambo ya ushamba.
Baada ya kupata kazi nikapata mchumba ambaye ndiye huyu sasa. Tuna mwaka mmoja na nusu na kwa kipindi hicho chote sikuwahi kumweleza kuwa nina watoto wawili. Yeye alikuwa anajua kuwa ninao wawili. Moto wake si mdogo, kavunja vyombo vyote kabatini, kavunja dressing table, kavunja coffee table yaani ni kasheshe, binti kapandisha majini ya kichaga. Najaribu kumtuliza hatulii, naombeni mnisaidieni kwani nampenda sana na ninamuhitaji maishani na sikupanga kumuumiza moyo

Bw Mikela.
Pole sana bana.
ila, Umenishangaza uliposema kuzaa na wanawake wawili tofauti ni mambo ya kishamba? Kivipi?
Are you ashamed of your kids??? Mimi na machache ambayo huenda yakakusaidia nawe kujiuliza ilikuwaje.
  • je, aliwahi kukuuliza una watoto?
  • uliwahi kumwambia una mtoto mmoja, si wawili?
  • je, (unahisi/inawezekana?) una watoto wengine zaidi ya hao wawili?
...nakushauri mpe muda atulie. Hakuna justification yeyote yeye kuvunja vitu ndani kwako, hata kama
ni yeye alivilipia kununua.
Pamoja na kwamba unampenda na unamuhitaji sana maishani,
Hasira aliyokuonyesha kwa kuvunja vunja samani kwenye nyumba yako ni ishara mbaya sana huko mbele ya safari.

...mpe muda. Akishatulia kaeni chini muambiane UKWELI.
Duniani hakuna mkamilifu bana, hata naye atakuwa na 'tofali' lake bana,
Jiandae tu jinsi ya kulipokea 'kichwani mwako.'
 
katika vitu nisivyopenda ni kudanganya (uongo ni mbaya sana) imagine wewe ndo ungekuwa yeye ...nadhani kama ulivyosema kweli we bado mshamba.. halafu sidhani kama huyo atakuwa mchaga ..Most of them niwastaarabu (kuvunja dressing table sijui na makofii olomide ) 🙂 sijui lakini but huwa ni wastaarabu na huwa wanaresolve issue smoothly...inawezekana ni wa pwani pwani Msoga msoga hivi
kwahiyo alipokuwa akifanya uvunjaji no mizuka ya ngoma ndio iliyokuwa imepanda? Maana pwani na ngoma ni kama kwapa na jasho.
 
The guy is crazly in love ndio maana amechukulia kuvunjiwa vitu positively. Mkishakaa miaka kumi akakuvunja vioo vya gari ndio utajua mziki wake. Ila umesema hutegemei kumuuzi tena kwa hiyo hatavunja vitu tena. Muombe Mungu akusaidie usimamie usemi wako, kwani maudhi hayapangwi utokea. Well hiyo tabia ya kuvunja vitu sidhani kama ina uhusiano wowote na binti kuwa mwaminifu au siyo muaminifu. Ni ukorofi full stop!

Bw Mikela.
Pole sana bana.
ila, Umenishangaza uliposema kuzaa na wanawake wawili tofauti ni mambo ya kishamba? Kivipi?

Are you ashamed of your kids??? Mimi na machache ambayo huenda yakakusaidia nawe kujiuliza ilikuwaje.
  • je, aliwahi kukuuliza una watoto?
  • uliwahi kumwambia una mtoto mmoja, si wawili?
  • je, (unahisi/inawezekana?) una watoto wengine zaidi ya hao wawili?
...nakushauri mpe muda atulie. Hakuna justification yeyote yeye kuvunja vitu ndani kwako, hata kama
ni yeye alivilipia kununua.
Pamoja na kwamba unampenda na unamuhitaji sana maishani,
Hasira aliyokuonyesha kwa kuvunja vunja samani kwenye nyumba yako ni ishara mbaya sana huko mbele ya safari.

...mpe muda. Akishatulia kaeni chini muambiane UKWELI.
Duniani hakuna mkamilifu bana, hata naye atakuwa na 'tofali' lake bana,
Jiandae tu jinsi ya kulipokea 'kichwani mwako.'
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
The guy is crazly in love ndio maana amechukulia kuvunjiwa vitu positively. Mkishakaa miaka kumi akakuvunja vioo vya gari ndio utajua mziki wake. Ila umesema hutegemei kumuuzi tena kwa hiyo hatavunja vitu tena. Muombe Mungu akusaidie usimamie usemi wako, kwani maudhi hayapangwi utokea. Well hiyo tabia ya kuvunja vitu sidhani kama ina uhusiano wowote na binti kuwa mwaminifu au siyo muaminifu. Ni ukorofi full stop!

Nyumba Kubwa, maneno mazito sana hayo.

...waliosema LOVE IS BLIND hawakukosea kabisa.
Marriage Is An Eye Opener kwa waheshimiwa kama Ndugu yangu Bw Mikela.
 
Mume wangu alivunja simu zetu the night before our wedding. Nilimwambia kama hajawahi sikia bi harusi anasema NO kanisani atasikia kwangu. Nilimwambia asishangae kama sitatokea kanisani. Ingawa sijuhi kama nilikuwa serious au nilikuwa namtisha hilo beat lilisaidia. Leo hii mwaka wa tisa kwenye ndoa hajarudia kufanya uharibifu tena ingawa ni mtu wa temper.

Mwanangu pia anatabia akigombezwa na wasichana wa kazi kama ana glass, sahani anarusha ukutani. Aisee huwa nampa kchapo naona nae sasa amehacha huo mchezo kwani mama hapendi.

Unajua inatisha sana mtu akifanya hicho kitu aisee ni kama anakuwa amerukwa na akili kwa muda.

Nyumba Kubwa, maneno mazito sana hayo.

...waliosema LOVE IS BLIND hawakukosea kabisa.
Marriage Is An Eye Opener kwa waheshimiwa kama Ndugu yangu Bw Mikela.
 
Mawaidha yanayotolewa hapa ni mazuri mno, yanatujenga kihisia hata sisi ambao hatujaanza bado kuzipata hizo rabsha
 
Hebu jaribu kumtishia tu mwambie aanze kama hataki kukuelewa uone reaction yake... then tafuta mtu mzima amueleze nikimaanisha akuombee samahani na pia kumkanya kuhusu uharibifu wa vitu vya ndani....mi naita ni ushamba na ni kizamani. Kwani mkiongea tu haitoshi hadi avunje vitu..je haoni kama mnazidi kujirudiha nyuma kimaisha..na hali ilivyo ngumu weee. Na maisha ya ndoa kaka hayakosi mikwaruzano ya hapa na pale je mtakuwa mnabomoa na kujenga kila siku?
 
POLE SANA,
PAMOJA NA HUYO MCHUMBA WAKO, NA NAAMINI KUPITIA HILI UMEJIFUNZA NA KUJUA MADHARA YA UONGO NA USIRI HATA KATIKA
MAMBO YA MSINGI KWA WAPENZI, LAKIN pia SHUKURU KWA SABABU KUPITIA HILO TATIZO UMEWEZA KUJUA TABIA YA HUYO,
MCHUMBA WAKO PINDI ANAPOKASIRIKA. UTAKUWA MAKINI SANA ILI USIMUUDHI,MANAKE UKIMUUDHI IPO HATA WEWE ANAWEZA,
KUKUDHURU,NI MTU AMBAYE HAWEZI KUCONTROL HASIRA ZAKE. JAPO NI KWELI INAUMA LAKIN HAO WATOTO ULIWAZAA UJANANI,
KABLA HAUJAKUTANA NAYE HAKUKUWA NA SABABU YA KUWA MBOGO KIASI HICHO,JE UKIJA KUZAA NJE MKIWA NDOANI ITAKUWAJE??,
ATAKUNYOFOA ULIMI WAKO KWA UKUCHA..lol.

WATU WOTE WAMECHANGIA VIZURI MPE MUDA HASIRA ZISHUKE HALAFU MPATE MUDA WA KUWEKANA SAWA,OMBA MSAMAHA KWA BIDII ZOTE.

Halafu nadhani hata mkioana naona hao watoto wako usiwalete hapo nyumbani kwako,
huyu siyo mama wa kulea mtoto asiyemzaa mwenyewe,
watoto wako watakosa upendo pia nyumbani kwako hakutakuwa na maelewano mazuri kati ya
mama yao wa kambo na watoto wako,kuepusha hayo watunzie mbali na mazingira ya huyo kama
atakuwa mkeo.Ksb nijuavyo mimi hakuna malaika so hao watoto wanaweza kumuudhi then kwa hasira hizo,
anaweza kuwafanya kitu mbaya sana .Kulea watoto kuna changamoto sana,kama mzazi na mlezi lazima,
uwe unajua kudhibiti hasira,upendo,uvumilivu ndani yake.
Kama MNAPENDANA KWA DHATI hao watoto wasiwe kikwazo cha upendo wenu,Omba msamaha maisha ya mapenzi yaendelee.
 
Mikela tupe updates, muda huu bibie wako kisha anza kuezua mapaa au ndio anang'oa geti?
Mpaka ugomvi uishe nyumba yenu itakuwa kama imepigwa bomu.
 
Mikela tupe updates, muda huu bibie wako kisha anza kuezua mapaa au ndio anang'oa geti?
Mpaka ugomvi uishe nyumba yenu itakuwa kama imepigwa bomu.

da! hii kali...lol,

maisha yenyewe yanavyobana kiasi hiki,
halafu unakuwa na mume/mke mwenye hasira hizi,
siku ukimuudhi tu basi kila kitu kinavunjwa,
halafu hasira zikiisha mnaanza tena kupanga bajeti ya ,
kununua upya vitu vilevile upya,
Tena bora akiishia vitu tu vya ndani je akiwasha mto nyumba??,
bora iwe ya kwenu, na je kama ya kupanga???,
patakuwa patamu hapo...lol
 
mbombo ngafu
 
pole sana mpe muda atarecover tu,time is the best healer......baada ya siku mbili tatu akicalm down ndio uongee naye kwa upole,anahitaji reassurance tu kama unampenda na watoto hawataingilia mapenzi yenu...
 
Kuna watu ni wakali na si wasikivu kiasi kwamba hata wenza wao wanaogopa kuwaambia ukweli wa maisha yao. Hata wazazi wapo walio wakali mpaka watoto wanakuwa wanakaa na siri kibao. Kuna relations unakuta mwanamke mkali anamtreat boyfriebd wake kama mtoto wa kumzaa.
 
Mikela tupe updates, muda huu bibie wako kisha anza kuezua mapaa au ndio anang'oa geti?
Mpaka ugomvi uishe nyumba yenu itakuwa kama imepigwa bomu.

hahahhaahha nimecheka saaaaaaaaaaaaaana,ubarikiwe lol
 
Kwanza kabisa UONGO NI MBAYA...natumaini umejifunza hilo na hutorudia tena.Kama ungemwambia mwanzo akakwambia hataweza kulea watoto wawili wasio wake mngeechana kabla mpenzi hayajatulia na hasara ya vyombo isingekuwepo.Sasa unaweza kumpoteza ukiwa tayari unampenda sana na hasara juu!!
Nwyz cha kufanya ni kutafuta sababu ya msingi ya wewe kumdanganya ndani yako mwenyewe...kama ilikua ni hofu ya kumpoteza then tafuta jinsi ya kumjulisha hivyo. Ikiwa unajutia kweli ulilofanya na una uhakika kwamba hutaki kumpoteza kaa chini umwandikie barua inayoeleza ni kwa kiasi gani unatamani ungemwambia tangu mwanzo...usivyotaka kumkosa maishani mwako...unavyomhitaji...unavyompenda na mengineyo hata kama mnaishi nyumba moja!!

Ikitokea akakusamehe na kuruhusu muendelee na mahusiano yenu basi bahati ni yako.Hapo mkalishe chini uongee nae kuhusu athari za kuruhusu hasira zake zimtawale mpaka kuharibu vitu....hasara sio yako ni yenu!!!Akishakuelewa kuhusu hilo ongea nae kuhusu malezi ya hao wanao wa mwanzo na wenu mtakaojaliwa ''NASISITIZA'' kuongea nae kuhusu malezi ya wanao hao ili kama hatopenda waje kuishi na wewe uwaache kwa mama zao au uwapeleke kwa bibi ili wasije wakanyanyasika hapo kwako.Kama hajafurahia kitendo cha wewe kua na watoto wawili kabla na vile ulivyomdanganya anaweza kuwaadhibu wanao kwa makosa yako wewe.

Kama walivyosema wengine hapo juu kwamba ''mama wa kambo si mama'' nakubaliana nao kwa kiasi flani japo najua kuna wanawake wenye roho nzuri out there...hivyo basi kama mtakubaliana waje kukaa na nyie itabidi uwe karibu sana na wanao kujua yanayoendelea wakati haupo ili uhakikishe hawanyanyasiki!!!
 
Back
Top Bottom