Uwongo umeniponza


This is great piece of advice....ni vizuri kuwa wazi kwa mpenzi wako before its too late for both partners...good luck!
 
Aisee ushauri wa akili mhusika fanyia kazi
 
Inaonekana vitu vyote anavyovunja amenunua yeye. Na ndio anakupa bye bye sasa kazi ni kwako kumuomba msamaha na kumweleza huhusiano wako na wamama wa watoto hao. Lazima umekuwa unaenda behind her back kuwasiliana nao au kuona watoto wako.

Na kama unawakiume uko nje hapo ujue ni kazi zaidi maana tayari unayemtoto wa kuendeleza jina lako

Pia uombe mungu asiwe mtu ambaye hata kusamehe kwa kuwa muongo na kutomwambia ukweli tangu mwanzoni ili angajijua mapema ni wapi anaingia

Haya tuupdate
 
Nimesoma zaidi pointi zingine na kuona wengi wanaongelea wewe juu kuleta watoto wako ndani ya nyumba yako

Hivi utafikiriaje hivi kuoa hamjaoana, kuoa na yeye kuzaa wake bado. Fanya haya watoto wenu wakianza kukua au kwenda shule basi leta wengine akikubali ili wasiwe mzigo kwake at all costs.
 
Mikela kanipigia simu saa saba usiku, anasema bibie hataki kurudisha moyo wake nyuma.
 
Ni mapema mno ku conclude. Ampe muda atarudisha huo moyo mwenyewe kama kweli kulikuwa na penzi!

Mikela kanipigia simu saa saba usiku, anasema bibie hataki kurudisha moyo wake nyuma.
 
Hayo ndiyo matunda ya uongo,nadhani binti anahisi kuna mengi zaidi ya hayo na hapo ni baada ya kugundua mwenyewe.
kazi kubwa unayo ya kujenga ulichobomoa"uaminifu".
Na hapo hasira hiyo hujui imechangiwa na alipopata habari kwani hujui mengine aliyoelezwa kuhusu wewe.

Mpe muda hasira yake itatulia,kwani kwa muda huu bado anachemka ndani ya moyo wake,na anatafakari mengi japo hajachelewa.
Mwisho wa yote ni wewe kukaa pamoja na huyo mkeo mtarajiwa na kumweleza kwani hukuwana nia mbaya ya kutomwambia kuhusu huyo mtoto mwingine.mwambie asiruhusu yaliyopita yabomoe mipango yenu ya mbele(do not let your past destroy your future) la msingi ni kujipanga kwa upya.
Mungu awe pamoja nanyikatika kipindi hiki kigumu
 
Sasa kwa nini akavunja vyombo? Kwa sababu ya hasira?
 
Una watoto wawili? na yeye akiongeza wawili? lol ndio maana dada wa watu kadata
 
my friend hizo ni dalili za mwanzo za tabia zake(she has exposed some of her true colours),
hawazii umevinunua kwa thamani gani au kwa kiasi gani umejinyima ukanunua hizo zamani za ndani.
Kwa ufupi hafai kuwa mke wako na kama una mpango huo
jua mtagombana daima na anaweza hata siku moja kukuchoma na kisu au kukumwagia maji ya moto.
hasira gani hizo? amejuaje kama yeye atakuja kuzaa?
Kisa kasikia watoto na kwakuta ndio awe mbogo hivo?
kwa ushauri wangu bora urudi kwa kati ya hao uliozaa nao umwoe mmoja
walau watoto wako walelewe na baba na mama.
Achana na huyo dada mara moja
kama unapenda maisha yako yawe marefu na ya amani.
Siku ukithubutu hata kuwaleta awaone watoto
aweza hata wawekea sumu.
Nimemchukia sana bora agereact kivingine lkn si kama alivokuonyesha makucha yake.
 
Pole sana sana ndg yangu, ila huyo mtarajiwa wako sijamfagilia hata kwa ndoto!! yaani hilo ndiyo avunje vitu jamani!!! imagine mmefunga ndoa, na asikie kwa bahati mbaya una mtoto mwingine ( hapo sifagilii ulivyofanya hata kidogo), nadhani atavunja na hao watoto mliojaaliwa kuwapata mkiwa pamoja. Kuvunja vitu sio solution hata kidogo, ni afadhali angethubutu hata kukupiga wewe au kukuchania shati lakini si vyombo, kwa hiyo akikasirika wewe utakuwa unajiandaa kununua furniture upyaa! hiyo itakuwa kazi mno.

Anyway, ushauri wangu kwako, kwanza usiwe na haraka ya kuongea naye, wengine wanakuwa na hasira ya mara moja later anajutia alichokifanya, sasa msubiri ashushe hasira kisha ongea naye kwa utulivu kabisa na uonyeshe unajutia kosa lako la kutomuambia b4, then muombe msamaha mwambie halikuwa kusudi lako na ulidhani kwa kumficha ndiyo unatengeneza kumbe imekuwa kinyume, mwambie unampenda kwa dhati. Anza kuonyesha unaomba msamaha sasa kwa vitendo, mfano mletee zawadi yoyote ambayo unajua anaipenda, kama ulikuwa unapenda kuongea sana punguza kabisa kwa sasa. Pole ila usirudie kuserma uongo ndugu yangu nadhani umeona madhara yake
 
Lakini dada NK wanawake wa hivo ni waaminifu sana kwenye ndoa vitu nitanunua tu lakini hata nikisafiri mwaka na amani, halafu si mpaka nifanye kosa kubwa ndio anavunja vitu ?

umewahi kusikia mwizi akiibiwa huwa anakuwa mkali sana?
 
Pole sana, hukujua kuwa watoto hawafichiki? ungejisalimisha tu................
ila nadhani kawa na haraka kidogo, kwani ulishaenda kujitambulisha kwao au umeshamtolea mahari? anaanzaje kuvunja vitu vyako wakati yeye ni girlfriend tu? anajuaje labda una mpango wa kuoa mmoja wa mama wa watoto wako?
hajafanya vizuri kuvunja vitu, angeongea tu na wewe umwambie mpango wako kwake. Ila kama ndo kweli unampenda kihivyo, ongea naye tu atakuelewa, afterall hayo uliyafanya kabla hajapatikana
 
Honesty is the best policy.

Mkuu Nyani Ngabu, I love this. Wengi wetu hatuwi wazi unapokumbana na new love. Weka bayana kila kitu ili maamuzi sahihi yafanyike. Tofauti na hapo unaleta matatizo mbeleni unapoleta mara ohhh mara vile. Tukue jamani ili mahusiano yadumu.
 
I had the same feeling ila nikaogopa kumkwaza mtoa mada. Watu wasio waaminifu huwa ni wakali sana. Violance yake isikudanganye kuwa eti ni faithful.

umewahi kusikia mwizi akiibiwa huwa anakuwa mkali sana?
 
I had the same feeling ila nikaogopa kumkwaza mtoa mada. Watu wasio waaminifu huwa ni wakali sana. Violance yake isikudanganye kuwa eti ni faithful.

aliyetoa hoja ya kuwa huyo dada atakuwa mwaminifu sana siyo mtoa mada................. all in all, huwezi kusema kama wewe ni mwizi basi ukimkamata mwizi wako ukae kimya............... tena unakuja juu sana ili uonekane wewe ni mwema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…