Michelle
JF-Expert Member
- Nov 16, 2010
- 7,628
- 3,535
Kwanza kabisa UONGO NI MBAYA...natumaini umejifunza hilo na hutorudia tena.Kama ungemwambia mwanzo akakwambia hataweza kulea watoto wawili wasio wake mngeechana kabla mpenzi hayajatulia na hasara ya vyombo isingekuwepo.Sasa unaweza kumpoteza ukiwa tayari unampenda sana na hasara juu!!
Nwyz cha kufanya ni kutafuta sababu ya msingi ya wewe kumdanganya ndani yako mwenyewe...kama ilikua ni hofu ya kumpoteza then tafuta jinsi ya kumjulisha hivyo. Ikiwa unajutia kweli ulilofanya na una uhakika kwamba hutaki kumpoteza kaa chini umwandikie barua inayoeleza ni kwa kiasi gani unatamani ungemwambia tangu mwanzo...usivyotaka kumkosa maishani mwako...unavyomhitaji...unavyompenda na mengineyo hata kama mnaishi nyumba moja!!
Ikitokea akakusamehe na kuruhusu muendelee na mahusiano yenu basi bahati ni yako.Hapo mkalishe chini uongee nae kuhusu athari za kuruhusu hasira zake zimtawale mpaka kuharibu vitu....hasara sio yako ni yenu!!!Akishakuelewa kuhusu hilo ongea nae kuhusu malezi ya hao wanao wa mwanzo na wenu mtakaojaliwa ''NASISITIZA'' kuongea nae kuhusu malezi ya wanao hao ili kama hatopenda waje kuishi na wewe uwaache kwa mama zao au uwapeleke kwa bibi ili wasije wakanyanyasika hapo kwako.Kama hajafurahia kitendo cha wewe kua na watoto wawili kabla na vile ulivyomdanganya anaweza kuwaadhibu wanao kwa makosa yako wewe.
Kama walivyosema wengine hapo juu kwamba ''mama wa kambo si mama'' nakubaliana nao kwa kiasi flani japo najua kuna wanawake wenye roho nzuri out there...hivyo basi kama mtakubaliana waje kukaa na nyie itabidi uwe karibu sana na wanao kujua yanayoendelea wakati haupo ili uhakikishe hawanyanyasiki!!!
This is great piece of advice....ni vizuri kuwa wazi kwa mpenzi wako before its too late for both partners...good luck!