Uwoya adaiwa ndio chanzo cha Dogo Janja kuwa na muonekano wa kike

Uwoya adaiwa ndio chanzo cha Dogo Janja kuwa na muonekano wa kike

Dogo Janja toka ameoa yaan ndio ana kuwa na mambo ya ajabu ajabu zaid.
Sjajua nani alo mroga
mkuu pesa "" biashara ya media kwa sasa bila yakufnya hayo mavituko lazima ufe na njaa hahaa ...so wanajkuta wanalazimika kuwa watumwa wa fikra ili waendelee kubaki midomoni mWa watu
 
Dogo aliimba kuwa "anapewa hadi mambo ya uwani" ktk wimbo wake wa Ngarenaro
 
Shida ya utajiri na umaarufu, mwishowe atakuwa chakula cha watu, ni suala la muda tu.
 
Joti mwenyewe alishasema watu wanamtongoza kwa uhusika anaojivika kuwa mwanamke.
Sasa na huyu dogo ajiandae kukutana na mitongozo
 
Mbona Joti huwa anaigiza kuwa mwanamke pia?

Anyway mimi sikubaliani na hilo suala ila nahisi alikuwa anajaribu kutafuta "attention" ya wimbo wake huo,kwa hilo amefanikiwa coz watu wengi wanakimbizana huko you tube kuutazama.

Usanii ni ubunifu.
 

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dogo janja ambaye sasa hivi ameachia video ya wimbo wake mpya wa 'Wayu wayu' na kuacha gumzo kwa mashabiki kwa kuvaa uhusika wa mwanamke, na kusema kuwa mke wake ndiye alimfanya awe hivyo.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dogo Janja amesema mke wake ambaye ni muigizaji wa filamu za bongo, Irene Uwoya, ndiye alianza kumfanyia make up wakiwa mapumzikoni Zanzibar, na kumvalisha vitu vya kike, ndipo walipopata idea ya kufanya video akiwa kama mwanamke.

“Mke wangu kabla sijaanza kushoot alianza kunifanyia make up na kunivesha vesha tulipokuwa vacation (mapumzikoni) Zanzibar, akawa ananicheka, mpaka siku tunaenda kushoot ile make up ilibidi anifanyie yeye lakini ilitokea dharula hakuwepo, akaniambia niende kwa mtu anifanyie make up ya nude mimi hata siijui, hata lile wigi alinipa mke wangu na mimi nikapita nalo”, amesema Dogo Janja.

Kitendo cha Dogo Janja kuigiza kama mwanamke kimeonekana kuwakwaza watu wengi wakisema sio kitu kizuri mwanaume kuvaa hivyo na kujipodoa kama mwanamke, lakini kwa upande wake amesema ilikuwa ni ubunifu kwa lengo la kuboresha kazi.


Muungwana


Kina Caitlyn Jenner walianzaga hivi hivi....mwisho wa siku alikata dushelele na sasa kawa demu eti anashindana na mke aliyemzalia watoto. Kuwa na mahusiano na hawa mademu wa bongo muvi ni hasara tupu kwa sababu hawana vigezo vya kuwa wake kweli wamezoea kulostisha wanaume wasiojitambua. Sasa hivi tutasikia huyu dogo anashikishwa ukuta na Uwoya.
 
Back
Top Bottom