Uzalendo wa ajabu wa Watanzania: Nchi inatukanwa, Rais anatukanwa, tumenyamaza. Huu ni Uzalendo gani?

Kabila la Wanyaturu baada ya Uhuru wa Tanganyika, waliamini kuwa ndege zote zilizokuwa zinapita kwenye anga ya Singida zilikuwa zimembeba Rais Nyerere na zikawa zinaitwa ndege za Nyerere.
Siku moja moja Rais Nyerere akatambelea Singida.
Mnyaturu moja aliyeitwa Ntandu akamtukana Rais Nyerere kwa lugha ya Kinyaturu kwa kusema " mune...... wakwe uyui ni ukukira unto mwitriku reo waja utrenda ntuni hafai"
Tafasiri yake bila kutaja tusi alilomtukana Rais Nyerere ni kuwa alisema " huyu Nyerere ...........(tusi) amekuja kufanya nini Singida na mara kwa mara anatupita kwa juu na ndege yake"
Mtu aliyeyasikia matusi haya alienda kwa mkuu wa Mkoa kumwomba aonane na Rais Nyerere ili amwambie jambo muhimu sana kwa Maslahi ya Inchi.
Mkuu wa mkoa alimruhusu na akaonana na Nyerere. Alimwambia Nyerere matusi aliyotukanwa na Ntandu.
Rais Nyerere alicheka sana na kumwambia yule mtu kuwa " Mimi natukanwa kisa siku , ila ungeniambia kuwa Ntandu anataka kupindua Inchi ningemkamata sasa hivi kwa ajili ya kuisaidia Polisi"
Kwa falsafa hii hakuna kiongozi asiyetukanwa hapa Duniani. Hata Yesu alitukanwa na kuteswa na Mayahudi.
Ila mtu yeyote anayetaka kuharibu usalama wa Inchi ni lazima tumshughulikie kwa Nguvu zote kama tulivyofanya kwa Iddi Amini wa Uganda.
 
Uzalendo wa ajabu wa Tanzania unaendelea, sasa umehamia kwenye Corona.
Rais Magufuli ametusisitizia tuchape kazi, TV ya jirani zetu Kenya ikamtangaza vibaya kwa kumuita Mkaidi.


Kitu cha ajabu, kuna Watanzania wenzetu wanafurahia rais wetu kusemwa vibaya na media za nje
HILI NI LIKAIDI SIYO MKAIDI
Safi sana Kenya, endeleeni kuexpose this man's folly
Kweli tuna Rais chizi....!
Nimemsikia ATI anasema, nanukuu" CORONA-VIRUS Ni KAUGONJWA KADOGO KATAPITA TU KAMA UPEPO....!!!"
Kama huu siyo Ukaidi ni kitu gani?
Huu ni uzalendo gani?.
Rais wa nchi ni kama baba kwenye familia, hata kama anakosea, huwezi kushangilia baba yako anasemwa vibaya na watoto wa jirani halafu wewe unashangilia.

Kwenye janga la Corona, nchi za jirani wametishwa na Corona ya Italy na Iran na wakatishika, wameamua kusimamisha kila kitu na kuhimiza watu wao wajifungie ndani. Rais Magufuli amesema Tanzania hakuna hata mmoja aliyekufa hivyo tusitishane na kututaka Watanzania tuendelee kuchapa kazi, kama huu ndio msimamo wa rais wetu, na sisi Watanzania tunasimama na rais wetu, who the hell is jirani kumsema vibaya rais wetu?.

P
 
Mbona na wewe unafurahia baba yangu kutukanwa na kutumbuliwa jukwaani huku mashabiki wake wakishangilia kwa vigelegele hapo hawamjui wala hawajawahi kumuona.
Kila mtu apambane na hali yake.
 
kila nchi ina katiba ake na muongozo wake,wao kama wanaona amekaidi na kwa watanzania wote tumeona ni sawa tufanye kazi sababu ya mafua ndo tuache kufanya kazi tukae ndani je uchumi ukiyumba wanataka tukawaombe msaada kwao,tukisem tukae ndani je wauguzi nao watataka likizo,ya kijikinga na corona itakuaje hapo.
sio kila mtu atakubali ufanyapo jambo lako mze kaisha sema tupige kazi tunapiga nyie kaeni ndani tu matokeo badae. hakuna wa kukuletea chakula usipo tumia akili watakufa njaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tena aliwaambia kwa kuwadahalilisha... KATERERO wao MAJANGA wao UKIMWI wao ni asavali utukanwe kuliko kudhalilishwa
Kwani ni uwongo Katerero iko Bukoba, kwenye somo la Kiswahili darasa la 4, kuna somo la "Siku ya Gulio Katerero.
Kwani ni uongo ugonjwa wa ukimwi hapa kwetu ulianzia wapi?.
Huko sio kuwadhalilisha ni kuwaeleza ukweli mchungu.

Rais wa nchi ni kama baba ndani ya nyumba, anaweza kukosea na hata kugombezwa na mama, au inaweza kutokea baba akamchangamsha kidogo kwa tu kofi tuwili tutatu, hayo ni mambo ya ndani.

Lakini ukisikia baba yako anasemwa vibaya na majirani jinsi anavyomchamsha mama kwa tukofi tuwili tutatu, huwezi kufurahia. Vivyo hivyo agizo la rais Magufuli ni kwa Tanzania na Watanzania, sio Kenya au majirani. Kama wao wametishika na kusimamisha kila kitu ni wao, sisi rais katusisitiza tusitishane na tuendelee kuchapa kazi, kwanini wamseme vibaya rais wetu?.

Na wewe kama Mtanzania Mzalendo, rais wako anasemwa vibaya na majirani, unawezaje kufurahia kushabikia na kushangilia?.
Huu ni uzalendo wa aina gani?.
P
 
Kaka Pascal wengi huchangia mada sijui kwa mihemko!? But linapokuja kuja swala la utanzania haijalishi u chama wala ukabila, imetupasa kuwaamini viongozi wetu, kwani wanataarifa nyingi na sahihi kuliko tujuavyo sisi.

Mzalendo huwezi kukubali jirani amdharau/amtusi mtanzania mwenzako kwa vyovyote vile, sembuse Rais?

Tuwe wazalendo. Tusimame na Rais wetu katika raha na changamoto kama hizi za Corona.

Mtingi1.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni mimi nisingesema Mkaidi ningesema " Asiye na elimu ya Corona" hapo wamempa sana kichwa kumuonyesha kuwa ni jeuri, kumbe anaweka maisha ya watanzania hatarini. Rais hawezi kuwa baba...Mimi nina baba mwenye busara, asiyeongea matusi ovyo. Jirani hawamsemi ila ni media ya jirani na hiyo ni kukua kwa demokrasia na si vinginevyo.
Kwani ni lazima mtu afe ndiyo tuweke Quarantine? Paskali acha hizo.....wewe umeamua tu kumtetea home port wako. Basi mwambie kuwa kama ana hadhi ya baba aache kuwaonea watoto wengine, kuwaumiza, kuwateka na kuwapoteza.
Kwa hiyo baba yako akifanya ujinga, majirani wasimseme? Acha mambo ya Kisukuma wewe Paskali.
 
Nani kakwambia watanzania wanaukubali udikteta?. Hawana uwezo wa kupigana tu lakini hakuna apendaye udikteta. Mtu akitukanwa kama kaonewa hutetewa na watu wema, wapenda haki. Kama kaelezwa ukweli wewe ukaatafsiri kwamba katukanwa ,basi wewe ndo una matatizo
 
Hii ya kuumiza, kuteka na kupoteza ni hisia tuu zisizo na ushahidi. Kauli huumba, sio tuu kauli huumba, hata kumuwazia mtu mabaya au maovu kunaweza kumletea uovu huo. Hivyo muwazie mema ili awe mwema na kutenda mema.
P
 
Ushahidi! Ushahidi! Uthibitisho!!
Ipo siku wanasheria halisi watatuletea aina za ushahidi.
Tuisubiri hiyo siku ifike ndipo tuseme. Kwenye serious allegations sio vyema kuwahisi watu bure bila ushahidi.

P
 
Niliona kwenye Gazeti lao la Monitor. Uzuri niliwachana vizuri sana,kuna mwandishi nimemsahau aliandika KITABU kinaitwa :Mzigo wa Mtu Mzalendo" Aliyaelezea haya yote ambayo Ndugu Mayalla umeyaona leo..Tumezalisha kizazi cha hovyo sasa ambacho kwao hakuna jema.Mark Twain alipata kusema hivi:Ni jambo la kushangaza sana kuona Vijana wajinga wanavyokuwa Wazee wajinga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ya kuumiza, kuteka na kupoteza ni hisia tuu zisizo na ushahidi. Kauli huumba, sio tuu kauli huumba, hata kumuwazia mtu mabaya au maovu kunaweza kumletea uovu huo. Hivyo muwazie mema ili awe mwema na kutenda mema.
P
Hisia vipi wakati watu wanaokotwa kwenye magunia wamekufa kwa makumi wametupwa baharini. Magunia waliyookotwa nayo ni ya rangi moja, wananchi wengi wamefuatiliwa na magari ambayo yanajulikana ni ya TISS, wengine wametekwa wakapotea, waliorudi kama Roma Mkatoliki wameeleza walichofanyiwa ingawa walipewa karipio wasiseme ameulizwa nini. Maswali yaliyoulizwa mengi yanaelekea kule kule kumhusu Magufuli...Kama vile kwanini mnamwimba vibaya kwenye nyimbo zenu, Lissu alipigwa risasi 30 baada ya kumsema (challenge) Magufuli, Ben Saanane alipotea baada ya ku-challenge elimu ya Magufuli! Mo Dewji alitekwa kwa sababu fulani fulani hata mtoto mdogo anajua waliyemteka ni nani.
Paskali, hayo mambo mbona yanatokea kipindi hiki cha uongozi wa huyu Magufuli???
Alikotoka huyu Magufuli, visa vya mauaji ni vya kawaida...Wazee wanauawa (I hope Paskali hamkumdhuru babu na bibi), Albino wanauawa na viungo vyao vinachukuliwa kwenda kwenye machimbo.
Ukisoma magazeti ukiona mauaji na kunyofolewa viungo utaona ni Geita, Sengerema au Maswa nk. Mtastaarabika lini? Uchawi uchawi tu mpaka kwenye mikutano.
Hapa hatupo mahakamani Paskali, kwani hata hizi mahakama zinatenda haki? Majaji na Mahakimu wanapewa maelekezo ya kufanya ili kuumiza wananchi wasio na hatia. Bunge ndilo hovyo kabisa...wewe mwenyewe kama mwananchi wa kawaida ulionjeshwa joto la jiwe ulipoitwa Dodoma.

MBONA MAMBO HAYA HAYAKUTOKEA KATIKA SERIKALI ZA AWAMU ZILIZOPITA?
 

https://www.bbc.com/swahili/habari-52313325
Angalieni, rais wetu Magufuli anatukanwa na media za jirani, ni JF na BBC ya Uingereza tuu ndio wanatupigania kwa kulaani, media zetu kimya...kwao it's OK.

Mungu Ibariki Tanzania.
P
 
Hoja za huu uzalendo wa ajabu wa baadhi ya Watanzania wenzetu, bado unaendelea, sasa uzalendo huu umehamia Twitter, watu wanafurahia hadi kushangilia wakati siri za ndani kwenu, nyumbani na chumbani kwa baba na mama, zinaanikwa hadharani!.

Baadhi ya siri hizi za taifa letu zinazomwagwa Twitter ni classified information, nyingine ni secrets, na hali hii ikiachwa iendelee hivi hivi inavyoendelea, kuna siku folder la top secrets za ile Idara yetu, zitakujashuka kwenye public domain!, kiti ambacho ni threat to our national security, mfano itokee yule jamaa akute kumbe wale 'jamaa', waliofanya kile kitendo cha lile shambulio, pale 'mahali' ni inside job!, kutakuwa na usalama, amani na utulivu?.

Kitendo cha kupublish taarifa classified information kuhusu nchi yako, hivyo kuzifanya zionekane nje ya nchi, ni uhaini, ila uhaini huu sio wa kusambaza tuu, bali hata wale wanafurahia taarifa hizo, ni kuufurahia uhaini, hivyo huu uhaini wa kufurahia uhaini kwa nchi yako, japo haina any criminal liability lakini it has something to do with uzalendo wako.

Huu ni uzalendo wa aina gani?.
P
 
Mwizi ni mwizi tu hata kama ni mtoto wako wa kuzaa, huwezi kusema kwasababu aliyenivamia na kunikata mapanga na kupora simu yangu, ni mtoto wangu, basi nisimshitaki polisi, jizi ni jizi tu,
Hata kipindi cha Cold war, wapo, diplomat kibao, wa soviet waliamua kutoa siri za nchi yao na kuamia West, usa na uk, huwezi kusema idara hii hii ambayo imekuwa kama State terrorist Group ambayo inaumiza wananchi kila kukicha, ikivuliwa nguo huko mitandsoni, sie tukasirike kwa lipi jema ililotundea tangu awamu hii imeingia,
Ilisalitiwa KGB, sembuse TISS,
Tunataka TISS ya Kambarage iliyoikomboa Africa irudi sio hii, iliyojaa mabishoo vilaza, wanaotutishia bastola mtaani ili wachukue mademu zetu,
Motherfuckers
 
Mkuu Pascal. Yakupasa kufahamu kuwa uzalendo wetu uko compromised na utandawazi. Utandawazi umepelekea importation ya "demokrasia ya kimagharibi" ambayo kwao ni genuine ila kwetu huku ni fake na haitufai. Rejea usemi wa hayati Mwl. Nyerere kuwa tunaweza ku-import bidhaa kama pikipiki ila demokrasia sharti tuizalishe wenyewe.

Imported democracy ndiyo chanzo cha ulimbukeni unaouona twitter ambayo ndiyo social media inayoakisi kiwango cha "usomi" wa watanzania. Ndiyo, twitter ndiko utapata "wasomi" wengi kuliko facebook au youtube.

Kwa kifupi daraja la kati liko compromised kupita kiasi kana kwamba kuitukana serikali au viongozi ndiyo harakati mpya kama ilivyo ughaibuni.
 
Sasa Pascal we ndio unaipaisha Twitter locally! Wengine tulikuwa hatuijui umetufanya tukaitafute tuone hilo vuguvugu unalolipigia kelele! 😜
 
Sasa hawa wendawazimu wanaotunga sheria wao wasishitakiwe bali wale wananchi wanaoita wanyonge ndiyo washitakiwe, hata wakitukanwa si sawa tu. Kwani wa faida gani!? Kujipa umungu wa kuhukumu wengine ndio kazi waliyoomba kwenda kufanya madarakani? Takataka kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…