Kabila la Wanyaturu baada ya Uhuru wa Tanganyika, waliamini kuwa ndege zote zilizokuwa zinapita kwenye anga ya Singida zilikuwa zimembeba Rais Nyerere na zikawa zinaitwa ndege za Nyerere.
Siku moja moja Rais Nyerere akatambelea Singida.
Mnyaturu moja aliyeitwa Ntandu akamtukana Rais Nyerere kwa lugha ya Kinyaturu kwa kusema " mune...... wakwe uyui ni ukukira unto mwitriku reo waja utrenda ntuni hafai"
Tafasiri yake bila kutaja tusi alilomtukana Rais Nyerere ni kuwa alisema " huyu Nyerere ...........(tusi) amekuja kufanya nini Singida na mara kwa mara anatupita kwa juu na ndege yake"
Mtu aliyeyasikia matusi haya alienda kwa mkuu wa Mkoa kumwomba aonane na Rais Nyerere ili amwambie jambo muhimu sana kwa Maslahi ya Inchi.
Mkuu wa mkoa alimruhusu na akaonana na Nyerere. Alimwambia Nyerere matusi aliyotukanwa na Ntandu.
Rais Nyerere alicheka sana na kumwambia yule mtu kuwa " Mimi natukanwa kisa siku , ila ungeniambia kuwa Ntandu anataka kupindua Inchi ningemkamata sasa hivi kwa ajili ya kuisaidia Polisi"
Kwa falsafa hii hakuna kiongozi asiyetukanwa hapa Duniani. Hata Yesu alitukanwa na kuteswa na Mayahudi.
Ila mtu yeyote anayetaka kuharibu usalama wa Inchi ni lazima tumshughulikie kwa Nguvu zote kama tulivyofanya kwa Iddi Amini wa Uganda.