Uzalendo wa ajabu wa Watanzania: Nchi inatukanwa, Rais anatukanwa, tumenyamaza. Huu ni Uzalendo gani?

Serikali ikiacha kazi ya kutatua matatizo ya wananchi na kuanza kupambana na wananchi walioiweka madarakani inapoteza uhalali wa kuwaongoza wananchi hao na inapaswa iondolewe madarakani hata kwa makofi.

Kama wewe unafurahi kuwa chini ya utawala wa kinyama basi nawewe ni sehemu na mnufaika wa huo unyama.
 

Tuainishe aina matusi tujue sio porojo za kukimbia hoja kwa kusema mnatukanwa
 
Uzalendo wa aina gani?


Mzalendo pia ujiulize
Kwa nn haya yanatokea sasa kuliko awali?
Kwa zitoke classified?
Kwa nn zinatoka huko ndani?
Je, zina manufaa na hasara gani kwa taifa na watu wake?
Kwa nn baadhi ya umma unafurahi?
Kama serikali au taifa wapi wanakosea?

2015 hayakutukia?

Kwa nn umma unafeel being oppressed and exploited?
Do we have another choice to fight for justice and right of being well of as sisters and brothers of this country?
Tukimlinda naye atatulinda na kututetea kwa maovu ya wasaidizi wake?
Nchi nzuri inakuwa hivi?

Wazalendo tukipata majibu basi tutetee serikali!
 
Golden age ended 1995 kwa msemo wao lkn haikuwa bora kwa taifa la mrengo wa kati kushoto Bali kushoto kwa kuwa ilikuwa falsafa yetu
1995 tumesema sana na yerick kabla ya 2015sheria yao ibadilishwe lkn wapi mpaka Leo

Sawa


Tatizo ni falsafa ya ccm
 
Wengi wanataka uliberali lkn nchi na ccm wanang'ang'ania ujamaa uliopitiliza
Uliberali hats trump hautaki ndiyo maana anahaha lkn Democratic wanafurahi na kutia mafuta kwenye moto

Watz nawe ukiwemo hujui falsafa hizi zinavyofanya kazi ndiyo maana ni rahisi kulaumu

Iliberali ni umungu ( Mungu katika ubinadamu) hivyo haulengi kuumiza wala matokeo Bali chanzo (mfumo ulioleta changamoto iliyopo na sio kumaliza changamoto ktk mifumo ile ile kwani isiloshughulikiwa litarudi kama majani ya shamba yanayowasumbuliwa wakulima> ndago, kidila, lusaragasi nk majina ya kilugha


Wewe na paschall mnataka matokeo ya kuisha tatizo na ndiyo kazi ya wahafidhina na mafashisti

Hata chadema na act si waliberali

Kiufupi tz tunasafari ndefu but paschal atatusaidia na wewe tukiwa mrengo wa kati
 
Taarifa zitolewazo na watu ndani na nje ya nchi nyingi ni za kukosoa na siyo matusi. Mimi ninaona tofauti kati ya kukosoa na kutusi. Ni afya kukosoa ila kutusi ni mbaya. Tutenganishe na kupambanua kati ya kukosoa na kutusi. Ila wenye tabia ya kutokubali kukosolewa huwa wanaona kila hoja ni tusi.
 
Watanzania kama watanzania inafaa kutukanana wenyewe kwa wenyewe,ila linapokuja suala la kutukanwa na watu wengine hatuna budi kuhamka.
Ifike siku moja tuwe kama Marekani,matatizo yao wanadeal nayo wenyewe,ukijichomeka katikati yao wanakugeukia kwanza wewe kukupa shughuli pevu baada ta hapo wanarudi kumaliza tatizo lao.
USA USA USA USA......
 
Uzalendo huwepo panapokuwa na usawa na haki kutendeka.

Kila mtu anatenda na kutendewa sawia kadiri ya matendo yake ama uvumilivu unakuwepo.

Viongozi watende yafaayo,na waingie madarakani kwa matakwa ya wanaowachagua.

Upendo,amani,uvumilivu na utiifu wa sheria ndivyo huleta uzalendo.
 
I'm a born soldier if you ask me about patriotism, the test is be able to protest the state at a cost of one's life.
What is a state?
What is a country?
What is a nation?
What is a government?
 
Uzalendo ni kuipenda nchi yako kwanza! Uzalendo wa kuipenda serikali unategemea utendaji wa serikali hiyo Kama inaingiza kwa kufuata katiba ya nchi na kutimiza, kuheshimu na kutenda haki kwa usawa bila ubaguzi! Ikiwa inatenda kinyume, basi uzalendo utakuwa kwa wanufaika wa serikali hiyo!
 
Kwa. Sasa. Tunawaachia. Wanaojiita. Wazalendo. Waonekane.
Nimesoma michango ya wa wadau humu
Kuhusu huzi huu ,da watu wananyongo
aisee na yote kwa yote nimekuja wazo
moja tu
WAZEE WOTE WA NCHI HII KAENI
NA KIONGOZI WA NCHI,
Na mshaurini kwa sasa taifa linataka
maridhiano hali si nzuri kupitia hapa JF
unaweza ukafanya utafiti na ukaona,
Maridhiano kwa sasa ya kitaifa hayaepukiki tena kabla ya uchaguzi.
Asanteni JF tunapata mengi pitia kwenu
 
Bora hizo document ziwekwe hadharani watz wajue madudu ya serikali yao, sio kila document ni siri, zipo za vigogo kuitafuna nchi nazo unataka zifichwe!

Huo sio uzalendo, ni kutetea wizi kwa kujificha kwenye kivuli cha uzalendo.
 
Tatizo kaka pascal wewe unaangalia sana ulipoangukia lakini umesahau kukagua ulipo jikwaa.

Unayoyaona ni matokeo ubabe,k
Ujuaji na kutofuta sheria kwa viongozi wetu tuliowachagua ,viongozi ambao wamejimilikisha kila kitu kwenye hii nchi na kufanya chochote bila kuhojiwa na kiumbe yeyote. Laiti kama wangekua wanafuata sheria na wanatuongoza na si kututawala katika misingi huru,kweli na haki wala tusingefika huko na usidhani kila mtu anafurahi zile taarifa za siri bali tunaumia sana kuona mambo ya hovyo yanafanywa kwa siri kiasi cha kwamba nchi inaingia kwenye hatari.
 
Upuuzi mtupu
 
Uliberali ni nini?
 
Unaju ni hivi..ukweli kabisa kuna tabia za waTanzania wenyewe ambazo ni mbaya sana,mala kadhaa utamsikia mTanzania akisifia vya nje na kuponda vya ndani ya nchi yake,nadhani hua ni kama ujinga tu wa wengi,unaweza sikia mtu akimsifia mtu ilihali yupo huko nje ya mipaka awezavyo tu na hata huyo mtu hamjui wala hajawahi kumsogelea, hapa nchini watu wako tayali kuchafua uongozi ilihali huko huko nje wanakua wanajua wazi Tanzania ina uongozi imara..ni ka tabia tu fulani hivi ka kishenzi,maana ukweli ni kwamba ukitazama viongozi wa hapa Africa ni nani utamlinganisha na JPM? Yamkini wale wa zamani kama kina Nkwame Nkuruma,Patrik Lumumba na mtu kama Ghadafi,na waTanzania hawa hawa wanaona wazi lakini wakikaa tu na watu wa huko nje waponda nchi yao utadhani kuna kitu watalipwa au watabadilika kua watu wa nje, ukiiponda nchi yako nje ya mipaka ni sawa na unajitukana tu wewe mwenyewe, tukiachana na hayo bado ziko tabia nyingi tu..unaweza kua kijiweni unakunywa hata kahawa likapita gari tu kwa mfano zuri zuri hivi na watu wawe wanalijua hilo gari ni la tajiri fulani utaona maneno yanavyosemwa..wataanza kumsema huyo mtu utadhani wanalala nae chumbani kua wanamjua sana,anaweza akapita msichana ukasikia wati wanasema huyo dada kaungua na HIV kitambo,hawajawahi kumpima wala hawamjui,juzi hapa swala la Covid-19 mtu ana idadi ya vifo kwenye kijiwe cha kahawa ilihali hajafiwa na ndugu jamaa wala jirani,ukimbana na maswali anakua mkali anakwambia weww ni CCM. Yani Tanzania MUNGU aiponye tu lakini watu hawa ni tatizo kubwa sana sana. Sielewi tafisiri ya kiswahili vzr kua watu wa hivyo ndiyo wapumbavu,wajinga au wanatakiwa kuitwaje sijui kwa kweli.
 
Mkuu wangu mayalla, nikushauri kitu.
Nenda wafuate hao wanaotukana nchi na Rais ukawakanye.
Kwanini unapita njia ndefu wakati njia fupi ipo!!!
TUWAKILISHE MKUU TUTAKUONA WA MAANA SANA.

Haya unayofanya humu unajidharilisha tu mkuu.
Usiwalazimishe watu kuwa wazalendo, uzalendo huletwa na haki

Nakushauri kajiunge na musiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…