Uzalendo wa ajabu wa Watanzania: Nchi inatukanwa, Rais anatukanwa, tumenyamaza. Huu ni Uzalendo gani?

Watanzania si MAZWAZWA wa kumtetea dhalimu aliyejaa dhuluma, muongo, fisadi, mwizi, anayedharau Watanzania, anayedharau katiba, mahakama, Bunge, muuaji, anayejichotea trillions Ikulu bila idhini ya Bunge, mbaguzi, asiyeshaurika wala kuambilika mtu ambaye ni hatari sana kwa mustakabali na mshikamano wa Tanzania na Watanzania.

Ulikuwa wapi alipowatusi wastaafu, Mawaziri na Watanzania?

Acha unafiki wako wa kumtetea huyu dhalimu anayedhani yeye ana hati miliki ya Tanzania.

Mwambie awajibu Maaskofu.

WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini
 
Paskali unajivunjia heshima bure, taaratibu unaanza kuwa hayawani (samahani kwa tusi).

Unaanzia wapi kumtetea Raisi Magufuri?

Umezisoma vyema hoja za majarida ya nje hususani “The Economist”? Kila walichoandika ni ukweli usiopingika!

Wanashindwa vipi kukuita dikteta ikiwa katiba ya nchi inaruhusu maandamano halafu Raisi unapinga? Je, huko sio kukiuka katiba?

Wanaacha vipi kukuita dikteta ikiwa umezuia mikutano ya kisiasa? Kabla yake Raisi Magufuri mikutano ilikuepo kwani nchi haikuendelea?

Ikiwa unatoa amri nyumba za watu zivunjwe sehemu moja (dar) halafu Mwanza unasema walikupa kura wasivunjiwe, huu sio udikteta?

Halafu wewe Paskali unasema ni Raisi wa wote, hao wa dar wakisema sio Raisi wao maana anawaone na kupendelea wa Mwanza watakua wamekosea?

Sisi kama watanzania tunaanzia wapi kupingana na ukweli ambao tumeshindwa kuusema wenyewe. Magazeti ya ndani yalipoandika yalifungiwa, ya nje yameandika unapanza sauti kusema ni uongo!

Ukiwa na baba mlevi, halafu jirani akasema “baba yako ni mlevi” atakua amekutukana?

Baba yako mlevi huyo akiwa anampiga mama na kunyanyasa watoto sio haki kumlipoti polisi? Ikiwa Raisi wa nchi fulani anavunja haki za binadamu, je UN wakae kimya?

Uzalendo hauna maana utetee maovu ya viongozi wa nchi bali kutafuta msaada wa ndani na nje ya nchi. Moja wapo ikiwa kukemea na kushauri. Sasa hapa kwetu wakisema wazee wataambiwa wana washwa washwa!

Kwaheri Mayalla, wewe na uzalendo wako uliopotoka.
 
Kwa wakongwe wa JF watakumbuka mada za pasco zikivyomuongelea Magufuli na kumpa hilo jina au sifa ya udikteta....alifanya hivi consistently na matokeo ya maandishi yake ndio haya ambayo leo kwa unafiki uleule anataka kujikosha....na ukiiangalia kwa jicho la kitaalamu zaidi bado mada hii ni muendelezo wa ajenda yake.
Msimamo ni kitu kizuri sana....@Mshanajr
 
Paskali tafadhali sogea upande huu tujadili hii reply ya jingalao ukikaa kimya bila kusema neno itatafsiriwa ndio ukweli
 
Wazelendo waliisha 1970's uko mm saa ivi sioni MZALENDO. Kama viongozi sio wazalendo unategemea wananchi waweje, viongozi wetu hawayaishi wanayo ya sema, wanaweka maslai yao binafsi mbele kuliko ya taifa kila decision lazima ziwe zina wa favor
 
Mie kwenye huu uzi mchango wangu utakuwa kulike tu kwa wale wanaoandika point na kuignore kwa wale ambao sijaelewa chochote
 
BAK, kila ukiquote huo uzi kuhusu waraka wa Maaskofu jamaa wanaogopa sana na hawathubutu hata kuufungua.

Wanajua Maaskofu wamebeba maelfu ya watu ambao kwao Viongozi wa dini ni muhimu kuliko madikteta Uchwara wengine.

Wabillah Tawfiq
 
Mwananchi huyu ambaye kabomolewa nyumba Kimara

Mjomba wake kabomolewa nyumba Buguruni

Mamake mdogo katimuliwa vyeti vyeki isivyo kihalali

Hawezi kuelezea mawazo yake wazi wazi,

Anapigwa kodi kubwa, analipa kodi na wanasiasa kuitumia vibaya tena kwa jeuri

Akiumwa Hospitali hapati dawa

Bibi yake kule kijijini hata akiumwa hatibiwi sembuse barabara ya kwenda Hospitali hata bodaboda haipiti

Mdogo wake kijijini anasoma kakaa kwenye mabanzi.
 
Sijaelewa!Ni kama unajipofusha tu,ni wakati gani,mahali na saa ambayo Mtanzania anaweza akamsema raisi wakati wowote Tanzania akabaki salama?
Au akasikilizwa?Au akaruhusiwa kuzungumza???Kumkosoa raisi Tanzania ni kosa la jinai...Kujieleza kwa namna yeyote ni MARUFUKU na mwiko Mkubwa.
 
Kifupi siku hizi kawa kama kinyonga au panya anang'ata na kupuliza.

Ila nnahisi hii ndiyo style mpya ya sasa ya uandishi pasipo kusahau kuna ile nyingine ya kupiga dongo sirikali kwenye IG, FB au TW afu baada ya masaa kadhaa unaposti tena kwamba mtu alihaki account yako ili kuweza kukwepa kukutana na wale watu wasiojulikana
 
Naam Mkuu hajibu. Mtu mwenye kuitakia mema nchi yake na raia wenzie KAMWE hawezi kukaa kimya kuhusu waraka wa kutahadharisha na kuonya kuhusu muelekeo wa nchi yetu.

Na huyu mnafiki naye anafuata nyayo za dhalimu hasemi chochote kuhusu waraka ule ambao umebeba ujumbe mzito sana.


BAK, kila ukiquote huo uzi kuhusu waraka wa Maaskofu jamaa wanaogopa sana na hawathubutu hata kuufungua.

Wanajua Maaskofu wamebeba maelfu ya watu ambao kwao Viongozi wa dini ni muhimu kuliko madikteta Uchwara wengine.

Wabillah Tawfiq
 
mkuu huu ni uzalendo unaotengenezwa na tuliowapa dhamana ya kutuongoza, viongozi wote sasa hivi kwa kiasi kikubwa, lugha zao ni za kibaguzi. shughuri za serekali kwa kiasi kikubwa zimekua za kichama. mkuu WA chama anaweza kusimama na kujinadi maendeleo hayana chama, lkn mkuu wa mkoa anasema hapa sitatoa ushirikiano kisa mmechegua chama flani. serekali ya awamu hii ni yakibaguzi kupita kiasi.
 
Mayalla,Unakumbuka swali lako kwenye press conference ikulu? Eti alikwambia ulizaliwa wakati wa njaa .Nadhan alikusudia fikra zako finyu.Ile unajua maana yake?? duh ulipata jibu mujarab?? ulisoma kile kifungu 35 au sijui gani kama alivyokitaja? au hukujiridhisha .Basi ndo ivyo jomba mimi ndio ninaye gawa hela na pia nitakupangia mda wa kulala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…