jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 36,197
- 29,717
Basi Tanzania itaendelea kama exception piaAaah
China ile ni exception mkuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Basi Tanzania itaendelea kama exception piaAaah
China ile ni exception mkuu
Mwananchi huyu ambaye kabomolewa nyumba Kimara
Mjomba wake kabomolewa nyumba Buguruni
Mamake mdogo katimuliwa vyeti vyeki isivyo kihalali
Hawezi kuelezea mawazo yake wazi wazi,
Anapigwa kodi kubwa, analipa kodi na wanasiasa kuitumia vibaya tena kwa jeuri
Akiumwa Hospitali hapati dawa
Bibi yake kule kijijini hata akiumwa hatibiwi sembuse barabara ya kwenda Hospitali hata bodaboda haipiti
Mdogo wake kijijini anasoma kakaa kwenye mabanzi.
Ni kweli mkuu, kwasababu naona kila mara huo waraka ukiwekwa hapa anapotea kama vile hauoni.Naam Mkuu hajibu. Mtu mwenye kuitakia mema nchi yake na raia wenzie KAMWE hawezi kukaa kimya kuhusu waraka wa kutahadharisha na kuonya kuhusu muelekeo wa nchi yetu.
Na huyu mnafiki naye anafuata nyayo za dhalimu hasemi chochote kuhusu waraka ule ambao umebeba ujumbe mzito sana.
Mkuu huyu jamaa akiamua kujitoa ufahamu kuhusu yanayojiri nchini anakuwa mtu wa ajabu sana kwa pumba anazoandika humu.
Wanabodi,
Naendelea na Makala zangu ziitwazo Kwa Maslahi ya Taifa, ambazo huchapishwa kwenye gazeti la Raia Mwema toleo la kila siku za Jumatatu. Hizi Makala zinaitwa Kwa Maslahi ya Taifa na Pascal Mayalla, zinafuatiwa na Kipindi cha TV chenye jina hilo hilo ambacho kitaanza kutoka kwenye vituo kadhaa hivi karibuni, vikiangazia hoja mbalimbali muhimu kwa maslahi ya taifa letu la Tanzania.
Kwa wiki kadhaa sasa nimekuwa nikijadili hoja ya Udikiteta Tanzania. mada ya leo ni kuhusu uzalendo wa ajabu wa Watanzania kuunyamazia uongo unaoenezwa kuhusu udikiteta Tanzania, Jee Tuna Uzalendo Gani Kunyamazia Uongo wa Udikiteta?, Au ni Kunyamaza Huku Ndio Kukubali Kwenyewe Kuwa ni Kweli Taifa Letu Tanzania Tuko Kwenye Udikiteta?.
Wapenzi wa Safu Hii, bado naendelea na hoja kuu kuhusu Udikiteta Tanzania, nab ado namtafuta Waziri wa Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi, kutufafanua kuhusu haya yanayofanyika Tanzania kinyume cha katiba kama ni udikiteta kweli au laa.
Angalizo Kuhusu Uzalendo.
Rais wa nchi ni kama baba kwenye familia, na sisi wananchi wote, haijalishi umri, rais ni kama baba yetu, sisi ni kama watoto, hata kama kuna waliomzidi umri. Inapotokea baba anakosea, mfano baba ni mlevi, na akilewa huwa anampiga mama huku sisi Watoto tunaona, tunaweza kumzuia, kumkosoa na hata kumtukana, baba acha ulevi, na isiwe a big deal!, lakini inapofikia baba yako ananyooshewa vidole na majirani au mitaani kuwa Fulani ni mlevi, au watu baki wanamtukana baba yako, huwezi kufurahi wala kushangilia!, haiwezekani kuona baba yako anatukanwa na wewe ukakaa kimya, vivyo hivyo kwa rais Magufuli, pamoja na madhaifu yake yote ya kibinaadamu, Watanzania wazalendo, hawawezi kuona rais wao akitukanwa na kusingiziwa uongo, huku tumekaa kimya. Ukiona rais wako anatukanwa na kudhalilishwa kwa vitu vingine vya uongo na uzushi na wewe ukawa unajua ni uongo, lakini bado ukakubali na kukaa kimya au hata kushangilia, ujijue una matatizo!, ukimuimagine rais Magufuli kama ni baba yako, hutakubali atukanwe, adhalilishwe, na asingiziwe uongo, ila kama yote yanayosemwa ni ni kweli, then, its ok japo hupendi, lakini hakuna jinsi, acha tuu aambiwe, hata kama ukweli huo ni mchungu vipi, au unauma vipi!, itakubidi tuu ukae kimya na kunyong'onyea.
Leo tuuzungumzie uzalendo wa Watanzania, ni uzalendo wa aina gani ambapo Taifa lako linatukanwa, umenyamaza, rais wako anatukanwa, umenyamaza, huu uzalendo wa Watanzania, ni uzalendo gani ambapo uongo, ukisemwa sana, na kuachwa kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, mwisho wa siku, sio tuu uongo huo utaonekana kama ni ukweli, bali unaweza kabisa kubadilika na kuwa ukweli kwa sababu kauli huumba!.
Baada ya rais Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli, kushinda uchaguzi huru na wa haki, na kutangaza rasmi kuwa uchaguzi umekwisha, sasa ni wakati wa kupiga kazi ya ujenzi wa taifa kwa falsafa ya “Hapa Kazi Tuu” kuanza kuhimiza maendeleo ya taifa badala ya kukalia siasa, kwa kupiga marufuku mikutano ya kisiasa ya kitaifa, na kubakiza ile ya majimbo tuu, na pia kuanza kazi ya kulinyoosha taifa hili katika vita dhidi ya rushwa, ufisadi na ubadhirifu kwa kutumia tumbua tumbua, na amsha amsha ya ziara za kushutukiza na kuviamsha vyombo vya dola kutimiza wajibu wake kikamilifu, ndipo kelele za udikiteta zilipoibuka.
Wapinga udikiteta kila siku huupinga kwa kauli tuu na kutoka kufanya mikutano na maandamano, lakini siku zote kwenye kauli zao, huweka hoja maridhawa kuhusu udikiteta, wajibu hoja ambao ni serikali, hakuna hata mara moja huzijibu hoja kuhusu udikiteta, wao kazi yao ni kutumia tuu nguvu kubwa kupinga maandamano, lakini hakuna juhudi zozote kujibu hoja kuhusu udikiteta, matokeo yake, hufanikiwa kuzuia maandamano, lakini hoja za maandamano hayo kuhusu udikiteta huwa hazijibiwi na hubaki pale pale.
Hata haya maandamano ya tarehe 26/04/2018 yanayopigiwa upatu kwenye mitandao ya kijamii, watu wote wenye akili timamu, wanajua kabisa kuwa kiukweli tarehe 26/04/2018, hakuna maandamano yoyote ndani ya JMT, hivyo hakuna sababu kabisa za serikali yetu kutishika hadi viongozi wetu kuweweseka na maandamano hewa hadi kutoa kauli za vitisho kuyapinga maandamano hayo.
Natoa wito kwa viongozi wetu, wasijikite sana kuyapinga maandamano hewa, bali walizijibu hoja kuhusu sababu za maandamano hayo, kwa sababu ni hizo hoja ndizo zinatumiwa kulichafua taifa letu na kumchafua rais wetu.
Kama ni hoja kuhusu udikiteta na yanayosemwa ni uongo kuwa Tanzania hakuna udikiteta, wahusika wajitokeze hadharani kuzipinga hoja hizo za uongo kwa hoja mbadala za ukweli. Ndio maana nikasema namtafuta waziri wetu wa sheria, Prof. Kabudi kujibu hoja.
Uongo huu kuhusu udikikiteta ukiachwa kuendelea kusemwa sana bila kukanushwa mwisho wake unageuka kuwa ndio ukweli, hivyo dawa ya uongo ni ukweli, uongo ukisemwa, kama kuna mwenye ukweli autoe tuu ukweli huo hapo hapo kwa kuuknusha uongo ili kutoupa fursa uongo huo kuendelea kusemwa na kuenea.
Kuna uwezekano, kwa vile wapiga kelele kuhusu udikiteta ni wapinzani, wenye majibu kuhusu uongo wa udikiteta, wanayo, lakini wameamua kuwapuuza wapinzani kwa hoja za kelele za mlango, au kelele za wapangaji, haziwezi kumkosesha mwenye nyumba usingizi, lakini kelele hizi zinapofikia hatua ya kuungwa mkono na vyombo vya habari vya kimataifa, BBC, DW, SABC, Jarida la The Economist, etc, kama ni uongo, sii za kupuuziwa hata kidogo. Redio mestini (redio za jeshini JKT), redio mbao (uvumi wa mitaani) zikitunga uongo na kueneza uongo kuhusu udikiteta, unaweza kuzipuuzia, kwani zinasikilizwa na nani?, lakini inapofikia BBC, DW Radio, VOA, SABC wakaudaka uongo huu na kuuvumisha, hili sii jambo la kupuuzia hata kidogo!.
Au Gazeti za Tanzania Daima, Raia Mwema, au gazeti lolote la Tanzania, likisema rais Magufuli ni dikiteta kwa kumnukuu Mbowe au Lissu, mnaweza kupuuza, kwani magazeti haya yanasomwa na nani?, si ni magazeti ya kufungia tuu samaki, maandazi na chapati, lakini udikiteta unaposemwa na majarida ya kimataifa, The Economist, The Financial Times, The Newsweek, etc, hivi sio vyombo vya kupuuzwa hata kidogo!. Unaweza kulipuuza Tanzania Daima na Raia Mwema, lakini huwezi kulipuuza The Financial Times na The Economist!.
Mimi nimewahi kutoa hoja hizi kule kwenye mtandao wa Jamiiforums
Tusikubali udhalilishaji wa Jarida la The Economist, lamwita Rais wetu "Dinasauria wa Dodoma” na "bullheaded socialist"
baada ya kutokukemea magazeti ya nje kuandika uongo kumhusu rais wetu na kumuita majina ya ajabu ajabu, huku sisi na serikali yetu tumenyamaza , sasa ni zamu ya jarida la The Economist, limemtukana rais wetu "dinasauria wa Dodoma" kisha wakamuita a bad president na hadi kumtukana Baba wa Taifa, "a bullheaded socialist!". Pia kumsingizia mambo mengi ya uongo katika toleo lake la hivi karibuni.
Serikali ikanushe uongo huu wa SABC kumsema vibaya Rais wetu Magufuli kuwa ni Dikteta!.
Uzalendo ni kutokubali na kutonyamaza kimya wakati rais wako anaposemwa vibaya kwa hoja za uongo na media za nchi nyingine, bali ni kwa media zetu kujitokeza, kuukanusha uongo kwa kuusema ukweli na ikibidi serikali yetu sio tuu ikanushe bali pia ihitaji kuombwa radhi na kibidi tudai fidia!. Hata Kikwete aliposingiziwa kuhongwa suti nilitoa hoja hii Tuhuma za Rais wetu kuhongwa suti: Marekani ituombe radhi!, na Ikulu yetu iliingilia kati.
Pamoja na matatizo yake yote na mapungufu ya kibiinadamu ya rais wetu Magufuli, kwa sababu na yeye ni binadamu na sio malaika, Watanzania wote wazalendo wa kweli wa nchi yetu, kamwe tusikubali rais wetu kudhalilishwa kwa kusemwa vibaya, kwa kusingiziwa uongo na media za nje bila ya media za ndani na viongozi wetu, kukanusha na kumtetea, au kuunyamazia udhalilishaji kama huu ni sawa na kushangilia rais wetu kudhalilishwa.
Hoja hii ilitolewa na SABC News - Tanzania’s Magufuli descends from darling to despot:Sunday 9 April 2017.
Serikali yetu Kuitwa "Sinister" na "Authoritarian": Je, ni kweli? Kama si kweli, Tusiukubali Uongo huu, Tuukanushe!
Jarida la Africa Confidential toleo la 58, story number 20 lililochapishwa Oktoba 6, 2017, limesema hivi kuhusu Tanzania kuwa serikali yetu ni "sinister" na pia inaendesha nchi kwa mtindo wa "authoritarianism"!. Haya sio maneno mazuri kwa serikali iliyoingia madarakani kwa ushindi halali katika sanduku la kura, kupitia uchaguzi ulioendeshwa na Tume huru ya Uchaguzi, hivyo uchaguzi ulikuwa ni huru na wa haki, hivyo matokeo ni halali, na nchi yetu inaendeshwa kwa kufuata misingi ya katiba, na kuheshimu utawala wa sheria.
Ikulu yetu, Waziri Mwakyembe na Idara yetu ya Habari, tusikalie kuyafungia tuu magazeti ya ndani kwa kutoa habari za kweli msiopendezwa nazo, huku tukikaa kimya wakati habari za uongo kuhusu nchi yetu zikienezwa na media za nje!, habari yoyote ambayo sii ya kweli, kuihusu Tanzania na rais wetu, ikitolewa, tusikae kimya, ikanushwe!, vinginevyo itaonekana ni kweli!.
Sio mara moja wala mara mbili, nimekuwa nikisisitiza humu, uongo ukisemwa sana, na kuachwa kujirudia rudia bila kukanushwa, mwisho wake sio tuu utaonekana kama ni ukweli, bali unaweza kugeuka ndio ukweli wenyewe kwa sababu kauli huumba!.
Ni muda sasa jarida la The Economist limekuwa likiisema vibaya nchi yetu, na kumsema vibaya rais wetu, ikiwemo kumuita majina ya ajabu ajabu, mimi nikiwa ni mwandishi wa habari, kanuni kuu nambari moja kwa mwandishi wa habari, ni kusema ukweli daima, hivyo sina tatizo kabisa na chochote kitakachoandikwa kwenye gazeti, kuihusu nchi yetu Tanzania, au rais wetu Magufuli, kama kitu hicho ni cha kweli, lakini natatizwa sana na uongo wowote unaoandikwa kwenye magazeti na majarida ya kimataifa, likiwemo jarida hili la The Economist, kwa lengo la kuhadaa ulimwengu kwa kutoa story za uongo kuhusu Tanzania na rais wetu, na kuzieneza kimataifa zisambae dunia mzima, wanaoujua ukweli kuhusu haya yanayosemwa ni sisi Watanzania, nchi yetu inatungiwa uongo, tumenyamaza!, rais wetu anatungiwa na kusingiziwa uongo, tumenyamaza!, rais wetu anapachikwa majina ya ajabu ajabu, dikiteta, dinasauria wa Dodoma, na sasa ameitwa rogue, tumenyamaza!, rais anadhalilishwa na kutukanwa huku sisi tumenyamaza!, huu ni uzalendo gani?!.
Kuna wanaoamini kila kinachosemwa na media za nje kuhusu Tanzania ni kweli, na kila kinachosemwa kumhusu rais Magufuli ni kweli, huo ni mtazamo wao kutegemea na uwezo wa uoni wa jicho lao, linaona vipi, kuna kitu mmoja anaweza kukiona ni sawa, na mwingine akakiona sii sawa, mimi kwa upande wangu, naona sii sawa kwa nchi yetu kusemwa vibaya na rais wetu kuzushiwa uongo na kusingiziwa uongo.
Kwa vile uongo huu unasambazwa kimataifa na huku sisi Watanzania wenyewe tumenyamaza bila kuukanusha, matokeo yake sio tuu, jamii ya kimataifa, utauamini uongo huo, bali hivyo ndivyo itakavyo tuelewa na hivyo ndivyo itakavyo muelewa rais wetu, bali uongo ukisemwa sana bila kukanushwa, uongo huo hugeuka kuwa ukweli!. Hii tabia ya kusikia uongo na kuunyamazia, kunaweza kabisa kupelekea haya ya uongo yanayosemwa sasa, kuja kuwa ya ni ya ukweli na yatakuja kutokea Tanzania kwa siku za usoni!, ni mpaka pale yatakapokuja kutokea, ndipo watu watalia na kusaga meno!, tena wakati huo ukifiki, it might be too little too late.
The Economist walianzia hapa Tusikubali udhalilishaji wa Jarida la The Economist, lamwita Rais wetu "Dinasauria wa Dodoma” na "bullheaded socialist"
Tukanyamaza, sasa wameibuka tena na uongo mwingine
Tanzania's rogue president - Democracy under assault - The Economist
Katika report hiyo, wamemtukana rais wetu kuwa Rogue President. Kwa vile mimi sijui Kiingereza, ilinibidi nikatafute kwanza kamusi kuangalia neno rogue maana yake ni nini, mtu anaeitwa rogue ni mtu wa namna gani, na taifa likiitwa rogue state ni taifa la namna gani, naomba kwa heshima ya rais wetu, nisitoe tafsiri ya neno hilo, ila kwa kifupi ni kuwa, rais wetu ametukanwa!.
Kwenye report yao, japo kuna mambo machache ya kweli kuhusu Tanzania, lakini pia wamechomekea mambo mengine mengi ya uongo kumhusu rais wetu na hoja za udikiteta ambazo inabidi zikanushwe.
Story yenyewe ni hii, naomba nisiitafasiri nisije nikabadili maana,
Democracy under assaultTanzania’s rogue president
Na jarida lao la wiki hii limekuja na uongo mwingine kuhusu Tanzania.
Jarida la The Economist ladai uchumi wa Tanzania unaporomoka, lahamasisha Rais Magufuli adhibitiwe kwa vikwazo kiuchumi
Hii ni Makala toka jarida la The Economist, linamsakama sana Rais Magufuli, katika Makala hii, linahamasisha rais Magufuli adhibitiwe kwa kuwekewa vikwazo vikali kabisa kiuchumi.
How to save Tanzania
hawa watu wanamuita rais wetu, Dr. John Pombe Magufuli, kuwa ni an authoritarian and erratic president who is transforming a stable, if flawed, democracy into a brutal dictatorship.
Ni haki kweli kumuita rais wetu, an authoritarian na erratic president na kumtuhumu kuwa ana transforming a stable, democracy into a brutal dictatorship?. Kuna ukweli wowote hapa?. Hawa watu hivi ndivyo walivyoiambia dunia kuhusu Tanzania, kweli hivi ni vitu vya kunyamazia?.
Wakati haya yakisemwa, wiki hii hii, ndio hii wiki, waziri wetu wa habari, na naibu wake wako busy kumshupalia Diamond, mwanamuzi kijana mdogo anayejituma, hadi kufikia kiwango cha naibu waziri kufanya mahojiona ya kujidhalilisha, na Diamond akajibu mapigo kwa kumdhalilisha zaidi!.
Waziri Prof. Mwakiembe, Naibu, na Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Dr. Abasi, fanyeni press conference mjibu hoja serious kama hizi zinazohusisha reputation ya taifa letu kimataifa na sio kujikita kwenye trivia issues za sanaa, mambo ya sanaa, waachieni Basata, nyinyi mjikite kwenye serious policy issues, inchi yetu inadhalilishwa kwa hoja za uongo kuhusu udikiteta, nyinyi mnadiscuss nyimbo za Bongo Flava, sijui wamevaaje etc, this is nonsense!.
Huku sio kudhalilishwa kwa Rais wetu na Media za Nje? Je, watanzania tukubali, Tukae kimya? Kuna wakati aliyekuwa rais wa Zanzibar, enzi hizo Komandoo Dr. Salmin Amour alisemwa vibaya na BBC Swahili, hakukubali aliwashitaki, alishinda na alilipwa fidia, kama hizi media za nje, zinasema uongo kuhusu udikiteta Tanzania, kwanza tukanushe, tudai kuombwa radhi, na ikibidi, tuwashitaki, tulipwe fidia.
Mhe. Waziri wa Habari, Dr. Harrison Mwakyembe, usinyamaze kimya wakati rais wetu akidhalilishwa na media za nje. Pia Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, na Idara ya Habari Maelezo msinyamaze kimya, jibuni mapigo kwa kuusema ukweli kuihusu nchi yetu na kumhusu rais wetu hawezi kudhalilishwa kuhusu udikiteta, huku nyinyi mpo mmenyamaza.
Watu pekee wenye uhalali wa kumsema vibaya rais Magufuli ni sisi Watanzania wenyewe ambao ndio tulimchagua rais Magufuli kuwa rais wetu. Ilitokea sisi haturidhishwi na utendaji wake, sisi Watanzania ndio wenye haki hiyo ya kumsema vibaya au vyovyote kwa sababu sisi ndio waajiri wake!, na media zenye haki hiyo ni media zetu Tanzania na sio media za jirani au media za nje.
Kama sisi wenyewe tunampenda rais wetu na kumkubali sana, kwa nini tusiwatimue nchini kote raia wote wa kigeni walio nchini ambao wanamsema vibaya rais wetu?.
Haki ya Kukosoa na Kumsema Vibaya Rais wa Nchi. Ina Mipaka!.
Wenye haki ya kumsema vibaya Trump kwenye media ni Wamarekani wenyewe, vivyo hivyo wenye haki ya kumsema vibaya rais wetu Magufuli kwenye media ni sisi Watanzania wenyewe!.
Jee Rais Magufuli ni Malaika?.Hakosei, Asisimwe?.
No rais Magufuli sio Malaika, ni binadamu hivyo anakosea kama binadamu mwengine yoyote, lakini haki ya kumkosoa kwenye makosa ya mambo yetu ya ndani, ni haki ya Mtanzania na media zetu na sio media za jirani!.
Kitendo cha media za nje kumshupalia rais Magufuli ni kumdhalilisha.
Kama ilivyo ngazi ya familia, unaweza kukaa jirani na wife battering neighbours na kila siku unasikia vilio vya mke wa jirani akichezea kichapo na asubuhi unamuona na manundu, hata kama huyo mke anayechezea kisago hajalalamika kwako, wewe kama jirani huna ruhusa ya kumtangazia vibaya jirani yako huyo kuwa ni mbaya humpiga mke!.
Kwa vile Tanzania ni nchi ya kidemokrasia inayoongozwa na katiba yanye kuheshimu haki na utawala wa sheria, taratibu na katuni, kila kinachofanywa na rais wetu ni kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, na hata rais wetu yuko chini ya katiba na anapaswa kufanya kila kitu kwa mujibu wa katiba kwa kufuata sheria taratibu na kanuni na ikitokea rais akafanya kinyume cha katiba, sheria, taratibu na kanuni, pia ziko sheria taratibu na kanuni za kumshughulikia rais anapokwenda kinyume cha katiba au sheria.
Kama ni kweli rais wetu Magufuli anatenda kinyume cha katiba na sheria, na taratibu za kumshughulikia zipo lakini sisi Watanzania wenyewe tumeridhika naye na utendaji wake huo huo, hivyo hivyo anavyotenda iwe kwa kuvunja katiba au kinyume cha sheria, Watanzania wenyewe tumeridhika na kukubali, who the hell is jirani yasiyomhusu, anayekuja kutusemea kwenye media yao kuwa rais wetu amekosea?. Kama wenyewe tumekubali na tumeridhika, huyu jirani anamsemea nani?!. Kwa nini Watanzania tunanyamasia uongo huu?.
Wiki ijayo, nitakuja na set ya maswali kuhusu hoja za udikiteta ambayo nitayaelekeza kwa Waziri wa Sheria na Katiba. Prof. Palamagamba Kabudi.
Jumamosi Njema.
Paskali
You a genius, Ms. Lincoln. Did anybody ever told you that?Sijaelewa!Ni kama unajipofusha tu,ni wakati gani,mahali na saa ambayo Mtanzania anaweza akamsema raisi wakati wowote Tanzania akabaki salama?
Au akasikilizwa?Au akaruhusiwa kuzungumza???Kumkosoa raisi Tanzania ni kosa la jinai...Kujieleza kwa namna yeyote ni MARUFUKU na mwiko Mkubwa.
Hapana mkuu!You a genius, Ms. Lincoln. Did anybody ever told you that?