Uzalendo wa ajabu wa Watanzania: Nchi inatukanwa, Rais anatukanwa, tumenyamaza. Huu ni Uzalendo gani?

Uzalendo wa ajabu wa Watanzania: Nchi inatukanwa, Rais anatukanwa, tumenyamaza. Huu ni Uzalendo gani?

@Moderator tafadhalini hii ni JF si FB au mitandao mingine ambayo matusi ni ruksa. Humu lazima staha iwepo si matusi namna hii. Hawa madogo hawajielewi kabisa, unadai demokrasia lakini huwezi kumvumilia mwenzako akitoa hoja tofauti. Ndio maana wengine tumeamua kuwanyoosha ili upinzani na mashabiki wake wabadilike na tujifunze namna ya kujenga hoja huku tukilinda maslahi ya taifa na kuwa na staha kwa viongozi wetu.

..una hoja nzuri sana.

..ila una tatizo dogo ktk "mtazamo" wako.

..kwa mtiririko wa hoja zako inaelekea unaamini viongozi wako serekalini tu, huko kwingine hakuna viongozi.

..sasa napenda nikukumbushe kwamba hata ktk vyama vya upinzani kuna viongozi.

..na viongozi wa upinzani wanadhalilishwa, wanatukanwa, wanabugudhiwa, wanaumizwa, na wapo waliouwawa.

..ili tuwe na "udhu" wa kuwatetea viongozi wetu wa kitaifa wanaosemwa huko nje, ni vema tukaanza kwa kuwatetea viongozi wa upinzani kutokana na madhila wanayoyapata hapa nchini.
 
Tatizo ni rais wetu amezungukwa na kundi la wanafki. Na hao wanafki wanamtukuza ili wapate cheo, au wapate chochote kutoka kwake.

Sijui kama amewashtukia ,maana kama anawachekea ndio hao wanamponza na kumpelekea kufanya maamuzi ya ajabu huku wale wanafki waki mtukuza kuwa yuko sawa.
Niseme wanafki hao si wazalendo. Ni walamba viatu., na walamba viatu wamekuwa wengi kuliko wazalendo halis wa nchi hii
 
For sure kuna tatizo kwenye mfumo wetu wa elimu. Mbona watu ni wajinga kiasi hiki?
Hakuna anaesema rais yuko sahihi, hata mleta mada ameelezea hayo yote, Someni Muelewe lengo la mleta mada,
Tatizo ni kwamba watanzania hawaoni haja ya kumtetea Magu anapotukanwa na vyombo vya nje.
 
Mwakyembe na shinza wanakazi ya kumjibu diamond kwani ndio size yao

Haya ya vyombo vya habar vya nje ni s size yao
 
..una hoja nzuri sana.

..ila una tatizo dogo ktk "mtazamo" wako.

..kwa mtiririko wa hoja zako inaelekea unaamini viongozi wako serekalini tu, huko kwingine hakuna viongozi.

..sasa napenda nikukumbushe kwamba hata ktk vyama vya upinzani kuna viongozi.

..na viongozi wa upinzani wanadhalilishwa, wanatukanwa, wanabugudhiwa, wanaumizwa, na wapo waliouwawa.

..ili tuwe na "udhu" wa kuwatetea viongozi wetu wa kitaifa wanaosemwa huko nje, ni vema tukaanza kwa kuwatetea viongozi wa upinzani kutokana na madhila wanayoyapata hapa nchini.
Hawa jamaa wanapolazimisha wote tuwaze wanayoyawaza wao.
 
Wale wasukuma ambao walimoiga kura jpm hadi hawakubomolewa nyumba zao na wanaofaidika na huu utawala ndo wakaongoze kampeni za kumtetea baba yao. Ila sisi hapana.

Uzalendo kwa nchi tunao ila sio uzalendo wa kutetea upumbavu.

Au kama vipi nchi iuzwe kila mtu apewe chake au unasemaje mwanangu Bavaria
 
Nikisoma comments za watu wengi humu najiona mtu mwenyewe akili sana! Watanzania ni nani alituloga? Mnaombeza Paskali Hivi mmesoma kwa umakini alichoandika kweli?
Kaandika au anahamasisha? Uzalendo anaounadi umevurugwa na nani? Hizi dhana za kujificha kwenye kuilinda amani na uzalendo ni chaka la kufanyia maovu na ufisadi! Simameni katika haki na acheni kumega nchi vipande kwa ukabila!
 
Watu humu vilaza sana,yaani kuna watu unaweza ukawaona wa maana kumbe hata kuelewa vizuri andiko kama hiki wameshindwa wamebaki wanatoa oovu tu..
Ona na wewe unatutukana kisa sio wazalendo! Wewe uzalendo wako ni upi na umelifanyia nini taifa lako? Unatukana watu kisha unawadai uzalendo? Ni Tanzania tu inakopatikana hii kitu ya kuwaita wananchi malofa, vilaza, wapumbavu na vinyago kisha uwadai uzalendo wao kama fidia! Wajirekebishe na wajivue huo uungumtu kwanza ili tumwelewe mleta hoja!
Isitoshe, wapo wasemaji wake na yeye mwenyewe sio? Mbona wamekaa kimya? Kama wanaosemwa wapo na hawajachukua hatua sisi ni nani hadi tujipendekeze? Huoni kuwa tutabatizwa jina la viherehere na kuwashwawashwa?
 
Boss Pascal Mayalla Nikiri kwanza sijalisoma Gazeti lako lote, ila Kaka wewe ni Mjanja sana, Mbona unaongelea upande mmoja tu wa Baba???!!! Umeongelea Kusemwa kwa Baba ila haujasema kuhusu Ukali wa Baba??? !!! Ongelea pia Ukali wa Baba unavyowaogopesha Watoto, Baba akiingia nyumbani tu, watoto Amani inatoweka.

My Take: Siungi mkono kusemwa kwa Baba.
 
Baba ni Baba tu..."hao wazungu watakuwa wana wivu na rasilimali zetu,halafu ni wapiga 'madeal' na wamenyimwa tenda kujenga viwanda na flyover

na rais amegoma kusafiri nje na kukaa kwenye hotel zao za garama kubwa pia wanaona donge zaidi tz ya viwanda,uchumi ukizidi kupaa...bila hata mikopo yao ya masharti mengi..

~Anayeelewa huyu Paskal kaandika manini anitafsirie~

'..an authoritarian and erratic president who is transforming a stable,if flawed,democracy into a brutal dictatorship..'
 
Mkuu Pascal Mayalla sio kwamba hatuna uzalendo tatizo ni yeye mwenyewe ndiye anajidhalilisha, unaendaje mahali ambapo watu wamepatwa na tetemeko la ardhi wamefiwa, wana uchungu wa kupoteza nyumba na mali zao halafu unakurupuka na kuwambia wafanye kazi Serikali haitatoa msaada wowote, asiyefanya kazi na asile na asipokula afe, haya ni maneno ya hovyo sana
umeongea point my dia yaani kweli watu wako unawaongoza wako kwenye majanga ya kupoteza mali na hata ndugu zao walikufa wewe kama kiongozi unaongea hovyo badala ya kuwafariji unadhani hao watu watasemaje watkakuwaje
 
Mimi nadhani Rais awapunguzie nguvu Polisi hao ndio wanamuhalibia sana. Na nguvu zenyewe ni zile za kubambikiza watu kesi za uchichezi, wenyewe wanajua Rais yuko nyuma yao. Pili aruhusu na vyama vingine vifanye siasa, angalia CCM Polepole anazunguka nchi nzima kufanya siasa, Mwenyekiti UVCCM nae anazunguka nchi nzima. Achilia mbali hayo, angalia jinsi polisi wanavyowanyanyasa wapinzani kila siku kuripoti polisi, hili lina mkono wa Rais, yeye awategemee wananchi sio polisi. Sasa hapo utakataa nini kuwa huo sio udikteta?
 
Bwana Pascal Mayalla hao unawashangaa leo kwamba wanamkashifu na kumdhalilisha Magufuri ndio walewale waliokuwa wakimsifia mwaka wake wa kwanza serikalini mpaka hashtag zikatengenezwa kwenye mitandao ya kijamii na kwenye media houses duniani na ku-trend dunia nzima,cha muhimu ni Magufuri na serikali yake kujitafakari na kujiuliza,What has gone wrong?
Pili,kuhusu hii hoja yako bwana Pascal Mayalla si kwamba uoni au hujui kinachoendelea na kufanywa na serikali ya Magufuri,unajua haswa,labda kama ulivyoongelea hapo juu kwamba pia unaandaa na kipindi cha TV na kutafuta nafasi ya kukutana na kadha wa kadha na inawezekana pia ni kutafuta nafasi ya kusikika na kuonwa maana style ya utawala awamu hii ni wateule wote na expectant kumwaminisha mteule kuwa yeye ni malaika,hana mawaa na ni mzalendo pekee nchini,na kwamba wanaomkosoa si wazalendo,hawaitakiia mema nchi na hawastaili kuishi.
Magufuri must clean his act he should know even in Heaven a devil was/is an Angel.
 
Back
Top Bottom