Uzalendo wa ajabu wa Watanzania: Nchi inatukanwa, Rais anatukanwa, tumenyamaza. Huu ni Uzalendo gani?

Namimi najitokeza kushiriki uchaguzi halali viongozi wa nchi wananitukana eti Mimi ni bwege na lofa, sijakutuma unisemee umeridhika wewe binafsi.
 
Baba akiwa hasikii wala hataki kushauriwa au kuambiwa ukweli na watoto wake huwaga watu wa nje wanaommudu wanaingilia kati na kumpa ukweli wake. Mimi mtoto nikimpa mkweli nitachapwa au kuchezea makofi so watoto wanafurahi kapatikana wa kuwasemea hata kama haitafanya kazi ila mesaage inakua SENT.
 

OK,you need to act now,how? By spraying bullets to oppositions and critics or abducting and torturing critics and free-minds? Enlighten me please.
 


Tena pabaya Sana hicho chama kinakutawaleni zaidi ya miaka 50 na marais tafauti weshapita.muda wote huo kulikua hakuna tatizo la uzalendo, hafla kaja huyu munajadili uzalenda badala ya kujadili ujinga,njaa,miundo mbinu ,ajira,afya na kazalika.
Sijui mna ogopa nini au nani.
 
Hivi kati ya wananchi na aliye waambiwa ndugu zangu kule bukoba "mwafa","kwani tetemeko mimi nililiketa" nani katukana mwenzake?
Wananchi wanalalamika hali ngumu(vyuma vimekaza) anayehusika anajibu "pakeni gilisi" hapa nani katukana?
Ndugu yangu yako mengi ya kusema ila ngoja nikukumbushe huenda hujui nini maana ya uzalendo.
Moja ya misingi ya kizalendo iliyowahi kubainishwa wakati wa ujamaa ni huu"NITASEMA UKWELI DAIMA CHUKI KWANGU MWIKO".
Je kusema ukweli,kukosoa,kuhoji ni kutokuwa mzalendo?au ulimaanisha nini juu ya neno uzalendo.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Baba anapaswa kuwa na sifa njema ili aheshimiwe na watoto wake sasa baba ukiwa hueleweki hata watoto watagoma kukutetea ndivyo maandiko yasemavyo kwamba hata baba (mzazi) mheshimu tu katika Bwana soma hapa
[emoji116]

MLANGO 6 6
1 Enyi watoto, watiini wazazi
wenu katika Bwana, maana hii
ndiyo haki.
2 Waheshimu baba yako na
mama yako; amri hii ndiyo amri
ya kwanza yenye ahadi,
3 Upate heri, ukae siku nyingi
katika dunia.
4 Nanyi, akina baba,
msiwachokoze watoto wenu;
bali waleeni katika adabu na
maonyo ya Bwana.

[emoji115]
Baba unapaswa kumtii katika Bwana tu sio blah blah sasa kama mtu mwenyewe unayemwita baba hapendi kuwasikiliza wanawe wanachokitaka tena kilicho chema watoto watamheshimu vipi na kumpigania dhidi ya maadui wanaotumia mwanya wa mpasuko wake na familia yake kumjeruhi?
Katika msingi wa maandiko ni kuwa baba anayetakiwa kupiganiwa ni yule tu anayeishi kwa haki na hekima na familia yake. Baba yangu akiwa mlevi majirani wakamsema kuwa ni mlevi mimi nitakuwa mpumbavu na mwenye mashetani kama nitatetea kuwa baba yangu si mlevi. Hivyo kimya kinachoonekana ni ishara kuwa watanzania wanasapoti kilichosemwa hivyo sidhani kama kuna haja ya kumtafuta mchawi katika hili kabisa, kama anahitaji kutetewa basi watu anaowaongoza wanapaswa kuliona hitaji hilo kwa hiari isiyo na unafiki.

Katika historia yote duniani ni kuwa baba mwenye tabia njema hata kwa familia yake hupendwa na kutetewa na familia yake kwa kuwa ni muhimu sana kwa familia husika na familia yake itampigania kwa gharama yoyote ile tena si kwa vishawishi vya walio nje bali kila mmoja atafanya hadharani na kwa namna kuu kumtetea.

Kwa hivyo nimeshangaa unavyoanza kutengeneza movement ya watu kumtetea wakati watu wanajua kuwa hilo ni jukumu lao iwapo kila jukumu lake kaliweka sawasawa. Sasa hii ya kuingia gharama za TV imenishtusha kidogo maana ni wazi kuna ajenda nyuma ya pazia ukimaliza andaa vipindi vya kuungana na wanaolalamika tuone kama utaweza (kitakuwa kipimo cha kwa nini hawamtetei hao wasiomtetea hadi sasa)
 
Kwani sisi hatupati shida nayeye yupo kunasehemu kuona gari nisawa na kumuona malaika pia kunasehemu vifaa vya ujenzi bei chee pengine bei juu sana lakini nayeye yupo acha kilamtu apambane mwenyewe
 
kuna watu wamekaa wakisubiri habari hasi za taifa, wengine wanataka taifa liwekewe vikwazo wakati vikwazo vikiwekwa watakaotaabika ni watu wa hali ya chini, wengine tena wabunge wanatamani hali iwe ngumu hadi ikulu ikose bajeti lakini hawasemi hali iwe ngumu wakose mishahara na marupurupu yao mwisho juzi kulikuwa na mkutano kati ya rais na wafanyabiashara mambo mengi muhimu yalizungumzwa na kujadiliwa lakini mtu anatoka na hoja kwanini fulani alipewa nafasi lakini hakuzungumza hayo mambo hayawezi kumsaidia mwananchi wa kawaida uzalendo unaanzia kwako maana hao viongozi hawashushwi toka mbinguni bali wanatoka miongoni mwetu kama hatutaipenda nchi yetu tukipata nafasi ya uongozi tutafanya mambo mabaya zaidi ya hao tunaowaona wabaya
 
Nadhani ni muhimu kuweka mipaka kati ya "Uzalendo kwa nchi" na "Mahaba kwa watawala". Unaweza ukapenda ukawa mzalendo na kuipenda nchi yako sana tu, bila kuupenda utawala unaotawala nchi yako kwa wakati huo. Na kuna watu wanaupenda sana utawala lakini mapenzi na nchi yao hawana.

Na katika historia, hili neno "uzalendo" - Patriotism; huwa linatumika sana na watu ambao wanapenda sana kukandamiza watu wenye mitizamo na maoni tofauti na wao. Watu hao huwa wanaamini na wanataka kila mtu aamini kwamba wao tu ndio wenye mapenzi mema na nchi na kila mtu aliyekuwa na mawazo tofauti na yeye basi anaitwa "Msaliti" au "Mkosa uzalendo". Yalitokea kwenye Third Reich, USSR, China ya Mao hata USA wakati wa McCarthyism; aina hii ya kuwapa hatia ya kukosa uzalendo watu wanaopinga mwelekeo wa nchi yalikuwapo. Hii tabia ya kufanya siasa kuwa ulingo wa kupima uzalendo ni dhambi kubwa sana.

Watanzania wamefungwa midomo yao, hawana namna hata ya kusema. Pressure cooker yenyewe huwa inakuwa na outlet valve, pressure ikizidi; mvuke utoke.

Inapotokea watu kama Mange na magazeti ya kimataifa yanawasemea watanzania kwa namna yoyote ile; watu watashangilia tu. Lakini hiyo haina maana kuwa hawaipendi nchi yao, wanatofautiana na uongozi ulipo.

Tushindane kwa hoja sio bunduki, mimi nilikuwa nategemea Rebuttals za point kwa point.

"Ni haki kweli kumuita rais wetu, an authoritarian na erratic president na kumtuhumu kuwa ana transforming a stable, democracy into a brutal dictatorship?. Kuna ukweli wowote hapa?. Hawa watu hivi ndivyo walivyoiambia dunia kuhusu Tanzania, kweli hivi ni vitu vya kunyamazia?."

This is the most accurate description of this president.

Erratic - Ni vigumu hata kutabiri nini kitatokea kesho. Anatoa matamko freewheeling , kesho yanakuwa sera ya Serikali. Hapendi kuona mabinti waliopata mimba wanarudi shule (Mind you ilani ilisema utafutwe utaratibu), bila hata kuchambua vizuri tatizo anasema hataki warudi shule. Mkurugenzi wa halmashauri anamwambia kwa hivi sasa sina jibu la swali lako, kesho kapoteza kazi. Na mengine mengi sana. Mtu mwenye tabia kama hizi unamwitaje?

Authoritarian - Hili halina hata ubishi. Hana heshima na mihimili mingine, mara amwambie Spika "kawabane wapinzani bungeni", mara awaambie Majaji wanaamua kesi vibaya na kuna makesi mengi ya kodi huko, tukishinda hizo hela nitaipa mahakama. Kazuia shughuli za kisiasa, amevibana vyombo vya habari; Mara anafanya utafiti yeye mwenyewe kuamua wapi benki binafsi ikajenge matawi yake.... tuishie hapo maana tutajaza server.

Tena alipaswa kuongezewa na ya Ubaguzi wa kisiasa. Wananchi wanabaguliwa kutokana na siasa zao; Kimara wabomelewe tu, Kahama na Mwanza; hawa msiwaguse ndio wapiga kura wangu.

Ngoja niishie hapo.... ila my main point is "Uzalendo kwa nchi" na "Mahaba kwa watawala" are mutually exclusive. Sio lazima yaende pamoja.
 
Paskali- ukiungana na wanakijiji wanaomuita mama yako mzazi mchawi furaha yako haitadumu kwani hautapita mda mrefu utaitwa mtoto wa mchawi na baadaye kidogo mchawi
 
Pascal Mayalla
Ndugu hongera kw akutambua udhaifu w aserekali hii na CCM na vijawake kwa ujumla.
1. Naamini wewe wajua ni udikteta uopi tunalalmika na upo wazi.
2. Hongera tena kw akupata udhamini hakika utaupata na hutokufa njaa mjini hapa wakati sisi tukilia vyuma vimekaza wewe na kipindi chako utakuwa ukiimba vyuma vimelegea!

Hongera tena!
 
"Rais wa nchi ni km baba kwnye familia"
Unaakili timamu kweli ww jamaa??
Baba anaweza kula rambirambi?
Baba anaweza kukwambia hakupi chakula wkt anacho na anajua ww hujapata?
Baba anaweza ukapatwa na tatizo la nyumba yako kuangukiwa na mti mkubwa alafu anakuja kukwambia mm sikukuangushia mti kwa hiyo cwezi kukusaidia?
Hivi nyie ccm kwa nn hamtumii kabisa akili zenu??!!
 
Paskali, njoo usome points za huyu bwana sio upupu wako ulioandika..... unajua nyie wasukuma hamjuagi kuficha ujinga wenu, mnajua mwenzenu anakosea but still unajifanya kumdefend flan.... so far hasemwi vibaya ila ni ukwl tupu huwa anambiwa raisi.
 
Pascal Mayalla,

..kwa maoni yangu jukumu[wajibu wa] la kujibu makala ya The Economist linaangukia kwa msemaji wa serekali, mwandishi wa habari wa raisi, msemaji wizara ya mambo ya nje, au balozi wetu ktk nchi ambako jarida hilo linachapishwa.

..Sasa labda bado wanajipanga kuwajibu The Economist. Kwa kumbukumbu zangu Jaridi hili linatoka kila wiki au kila mwezi. Hivyo tuwe na subira kuona kama hao niliowataja wamejibu makala hiyo, na kama The Economist wamekubali kuchapisha majibu ya serekali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…