Uzalendo wa ajabu wa Watanzania: Nchi inatukanwa, Rais anatukanwa, tumenyamaza. Huu ni Uzalendo gani?

Mkuu bila shaka ulisoma Law of Tort, na unakumbuka hii principle "Res ipsa loquitur". Kwa kupitia utawala wa sheria na democrasia, wananchi wamesha-surrender powers zao kwa hao wanaoitwa madikteta. Ni wajibu wa hao "madikteta" kukanusha kwa niaba ya wananchi-watanzania kuwa wao siyo ma-Dictators...na huo ndo Uzalendo. Bila shaka wasingekuwa "madikteta" wangelisha-kanusha zamani sana.

Mkuu, kama hutojali jaribu kupitia comment yangu ile ya hivi karibuni..
@Pascal Mayalla
 
Sijaisoma yote hii habari lakini,najibu kutokana na kichwa cha habari kinavyoleza.,
ningeenda kukujibu kuwa uzalendo unakuja kutokana na raia kuona anapendwa na nchi yake..

Raia anapoona nchi yake inamlinda na mkumpenda,raia anakuwa anajivunia nchi yake,majivuno ya nchi yako ndio uzalendo wa nchi yako...

Serikali ya Tanzania,raia wake ndio maadui zake,...sifikirii kama kutakuwa na mtanzania atakae kuwa na majivuno na Tanzania...Uzalendo haupo Tanzania,period
 
Pascal Mayalla uzalendo wa WaTz upo mioyoni mwao lakini ipo siku ya moyoni yatageuka vitendo.
Kwani wewe ulikuwa unashauri tufanye nini!
Kuna moshi unafuka mahala mahala ujue kuna moto utakaounguza msitu
Nikushauri ongeeni na huyo anaitwa dikteta anatukanwa ajirekebishe
Mwambieni Tz ni yetu sote sio ya chama kimoja
Aache vitisho bali awe mnyenyekevu na msikivu
Amtoe mvuruga amani bashite
Asikilize vilio vya wananchi
Arudishe amani yetu upendo wetu na usalama wetu
Hatatukanwa vinginevyo ataendelea kutengwa
 
Ndugu Mayalla, kama maandamano ni hewa na hayapo, kwanini unasema viongozi wajikite kujibu hoja za maandamano hewa na ambayo hayapo?.
Hivi baba alisema Mayala maana yake nini vile....??
 


Hebu tupe tafsiri ya neno tusi kwanza. Kwa kiwahili sio kisukuma.
 
Mmeona anayofanya yote yako sahihi? Mbona sijaona yeyote toka chama chake akikemea ukiukwaji mkubwa Wa katiba unaofanywa na huyu mtukufu mtakatifu mnayetaka kutuaminisha hakosei? Kiongozi Wa nchi kuigeuza nchi kama familia yako utaambulia mashambulizi tu. Kama yeye anafurahia maumivu kwa wenzake ni halali wenzake kufurahia maumivu yake pia.
 
Mbona Pascal anaeleweka sana au siku literature haisomwi. Refer kitabu kama animal farm au kusadikika
 
Sometimes Pascal unazingua sana.

Mshana alisema humu kwamba hata Mungu aliruhusu Uhuru wa kutoa maoni.
 
OK,you need to act now,how? By spraying bullets to oppositions and critics or abducting and torturing critics and free-minds? Enlighten me please.
Hawa wetu wamechukulia upinzani kama uasi!! Mwafrica mpinzani wake anamchukulia gaidi na muasi
 
Pascal Mayalla acha kucheza na maneno,si watanzania wengi wanaojua kuwa media za nje wanamwita Rais wetu majina hayo mabaya. Hicho kipindi sidhani kama lengo lake ni jema
 
Watawala wanatuchukulia sie ni Wanyonge hivyo kutunyonga kwao wanalichukulia poa sana... ila wajue Bubu hutaka kusema mambo yanapomzidia....
 
Mbona sisi tunatukanwa kwakuitwa vilaza
Pointi ya Paskali ni kwamba muwe wavumilivu, sio tu umeambiwa ukatandike bango kwenye kitanda cha mke wako nawe unanyanyua kifua unataka kujibu.

Maadili yetu hayaruhusu kujibizana na Wakubwa.
 
Dk Abbas anapwaya sana pale habari maelezo
Ukizungumzia Mwakyembe na Shonza hawajui hata kazi yao pale wizarani wanadeal na petty issues ambazo hazina tija yoyote kwa nchi isipokuwa vinawapa media coverage tu.
Kuhusu vyombo vyetu vya habari tangu lini vikadeal na maswala nyeti kama tofauti na kupiga mbinje za kitoto tu ?
At least we have a platform to speak out JamiiForum tupaze sauti zetu pale nchi yetu inapodhalilishwa na vyombo vya habari vya nje.
Lakini na serikali ipunguze kufanya mambo yanayoidhalilisha.
 
Uzalendo ni dhana pana, nafkiri inaweza ikaamuliwa maana yake kulingana na sehemu, falsafa ya nchi n.k.
Kwangu mimi ni muumini wa State, My Faith and My Family hivi vitu vitatu come first to my priorities. Nikihisi mtu anahatarisha their survivor then come what may.
Lakini kuna mambo ya state wakati mwingine yanakupa ukakasi ktk morali haahasa yanapokuwa yanafanywa unpatriotically na mengine hayakanushwi kwa hoja stahiki.
 
Pascal unajidhalilisha sana. Labda kuwa verified kunakunyima kuwa huru. Epuka kufurahisha watu.
Ukifanya vyema unapongezwa. Ukivurunda unakosolewa na kusahihishwa. Wako watu kwa ajili ya kumtetea Rais. JF si watetezi wa Rais. Tunatetea maslahi ya nchi. Rais si nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…