Uzalishaji wa Cement Tanzania ni takriban mara mbili zaidi ya Kenya

Kwa hiyo Dangote anayetaka kuja kufungua kiwanda kikubwa cha cement hapo Kenya hajui nini anafanya?. Unadhani kuna mkenya gani atakayeendelea kuzalisha Cement hapo Kenya kuanzia 2023 mara tu tutakapoanza kuzalisha umeme toka bwawa la Nyerere ambao utakua 70% cheaper kuliko huko Kenya?, jiandaeni kuona viwanda vingi vikufunga uzalishaji na kuwa mawakala wa Cement ya Tanzania.
 
Ninataka kujua ni bidhaa gani muhimu Kenya inaizidi Tanzania katika uzalishaji, ninajaribu kutafuta lakini sioni zaidi ya siagi na Jojo.

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
Endelea kujitia hamnazo, yaani unafananisha sekta ya viwanda nchini Kenya na 'viwonder' vya Tz? Mwaka wa 2019 viwanda vya Kenya viliingiza $7.12Billion kwenye uchumi wa nchi ya Kenya, viwonder vya Tz vikaingiza $996Million tu kwenye uchumi wa Tz. Tafakari hayo. Kenya Manufacturing sector vs Tanzanian's
 

Sasa kama kuna viwanda vingi na uzalishaji ni mkubwa, mbona baadhi ya mikoa ikiwemo Arusha kuna sehemu kuna upungufu wa cementi? Au ndo kusema imepelekwa kwa majirani zetu?
 
Umeshalinganisha bei ya cement ktk EAC ?!. Ukifanya utafiti huwezi kuleta uzi kama huu humu !!. Tanzania ndiyo bei ya bidhaa hiyo ni kubwa kuliko jirani zetu .

Kusifu na kuabudu hakutabadilisha realty
 
Kenya ndio the biggest market in East Africa. Msipouza Kenya mtauza wapi? Hehehe
Tutapiga marufuku saruji kutoka Tanzania. Mbona tununue saruji kutoka kwa jirani mwenye roho mbaya?
Kwani kuna saruji ya Tz ambayo inauzwa Kenya? Viwanda vya Kenya vinauza saruji UG hadi na DRC. Cha ajabu nchi ya Kenya ina demand kubwa ya saruji zaidi ya Tz, ambayo kwa size ni karibia mara mbili ya Kenya.
 
Weka ushahidi wacha kupiga kelele, bidhaa gani muhimu ambayo Kenya imezidi Tanzania, Kama Cement, Sugar, Iron sheets, cooking oil, food and fruits,Tiles and Textile tunawapita kwa mbali?
 
Sasa kama kuna viwandda vingi na uzalishaji ni mkubwa, mbana baadhi ya mikoa ikiwemo Arusha kuna sehemu kuna upungufu wa cementi? Au ndo kusema imepelekwa kwa majirani zetu?
Kaka jaribu kutumia akili unapiuliza maswali hapa hadharani, si vizuri kila kitu utafuniwe Kama mtoto mdogo, unajua maana ya supply chain?.
 
Tanzania ya viwanda, safi sana
 
Mafuta yapi?, Cooking oil Tanzania tunazalisha zaidi ya Kenya, Kahawa na textile Tanzania tunazidi Kenya, sukari Tanzania tunazidi Kenya, labda Chai na maua ndio mnatuzidi.
Textile Kenya tunaexport to USA kupitia Agoa ambayo TZ mlikataa kutia saini. Tunawashinda kwenye textile na ukitaka data sema nikuletee ya Kenya na wewe ulete ya TZ. Mafuta, Kenya inaimport na kuuzia wafanyabiashara wengine wa nchi za EAC ikiwemo UG na Rwanda.
 
Kaka jaribu kutumia akili unapiuliza maswali hapa hadharani, si vizuri kila kitu utafuniwe Kama mtoto mdogo, unajua maana ya supply chain?.

Sasa kuuliza ni kosa? Wewe ambaye unatumia akili ungejibu tu swali langu kama liko ndani ya uwezowako kulijibu. sasa majibu yako yanasababisha nikuulize swali lingine - ni nini maana ya supply chain?
 
Kwani kuna saruji ya Tz ambayo inauzwa Kenya? Viwanda vya Kenya vinauza saruji UG hadi na DRC. Cha ajabu nchi ya Kenya ina demand kubwa ya saruji zaidi ya Tz, ambayo kwa size ni karibia mara mbili ya Kenya.
Wewe ninakujua ni msema hovyo hujui unachozubgumza ni mtu wa kusifia bila ushahidi wowote, pia unapenda kubadilisha mada unapoona umeshindwa, mada inahusu uzalishaji wa Cement, wewe unaleta kuhusu matumizi ili uonekane umeshinda, sasa ngoja nikuonyeshe ulivyo mjinga.

Mahitajia ya Cement Tanzania ni tani za Ujazo 6M(Soma ktk link hapo juu)

Mahitaji ya Cement Kenya ni tani za ujazo 5.07. Update on Kenya - Cement industry news from Global Cement
Punguza kupenda kuzungumza vitu usivyojua, hovyo kabisa wewe
 
Kwani kuna saruji ya Tz ambayo inauzwa Kenya? Viwanda vya Kenya vinauza saruji UG hadi na DRC. Cha ajabu nchi ya Kenya ina demand kubwa ya saruji zaidi ya Tz, ambayo kwa size ni karibia mara mbili ya Kenya.
Ndio nauliza watadump wapi hio extra cement? Kenya tayari tunajitosheleza kimahitaji. Wao demand yao ni less than 5 million tonnes ilhali wanazalisha 10 million tonnes na wanapanga kujenga kiwanda cha 7 million tonnes. Yaani capacity ya Tz itakuwa 17 million tonnes in the next few years yet demand yao ni less than 5 million. So I was just saying that Kenya tusiwakubalie hawa watu wadump cement yao huku. Itaua industries zetu coz TZ cement will be cheaper and will bring competition to our local industries. We already have anti-dumping regulations, we just need to apply them. TZ is producing far more cement than they need coz their goal is to export the surplus to other African countries. Our local tyre industry was killed by importation of cheap Chinese tyres. Yana tyre closed because of competition from chinese tyres.
 
Tuanze na mafuta kwasababu ni rahisi, kisha tutamalizia na Textile. Mafuta gani Kenya mnazalisha, kutoka zao lipi na wapi linalimwa hapo Kenya?
 
Tuanze na mafuta kwasababu ni rahisi, kisha tutamalizia na Textile. Mafuta gani Kenya mnazalisha, kutoka zao lipi na wapi linalimwa hapo Kenya?
Hatuzalishi mafuta. Tunaimport kisha tunawauzia wafanyibiashara wa nchi jirani kisha tunapata faida nono. Wacha nikutafutie nakala niliyosoma kuihusu. Lakini pengine unaweza kusema kuwa hio sio kuzalisha bali ni kununua na kuuza. Kama hicho ndicho kigezo chako basi tunaweza kutoa mafuta kwenye hio listi niliyopost.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…