Uzamiaji Afrika Kusini: Mikasa katika harakati za kuzamia Afrika Kusini kwa njia za panya

SAFARI YA KUZAMIA AFRIKA YA KUSINI KWA NJIA ZA PANYA

Sehemu ya kwanza.

Utangulizi

Mimi ni mtanzania mzaliwa wa Mbeya. Kwa sasa umri wangu ni wa kutosha kidogo kwa sababu nipo duniani tangu miaka ya 1980.
Wakati nasoma shule ya msingi kwenye miaka ya 1990 hivi tulikuwa tunaimba nyimbo maarufu wakati huo za kupinga ubaguzi wa rangi uliokuwa unafanywa na serikali ya makabulu kule Afrika ya kusini. Tuliimba nyimbo hizo kwenye Mchakamchaka, mistarini (Assemble) na kwa kutumia kwaya ya shule.

Kwa kweli zile siku za madarasa ya mwanzo ya darasa la kwanza hadi la tatu sikuwa naelewa sababu za kuimba nyimbo zile ni nini na hata Afrika ya kusini yenyewe ni kitu gani. Nilipofika Darasa la nne nilikutana na rafiki yangu wa muda mrefu aliyeitwa Gilbert Simya na ambae kwa wakati ule alikuwa darasa la saba na alikuwa ndio mwanafunzi mwenye uwezo mkubwa zaidi kitaaluma katika darasa lao.

Kwa kuwa nilikuwa namuamini sana kwa ujuvi wa mambo mbalimbali, niliamua kumuuliza ni kwanini tunaimba zile nyimbo za kupinga ubaguzi, ulioku- wa unaendelea nchini Afrika ya kusini na je Afrika kusini ni nchi gani? Ndugu Simya alinieleza sababu ya sisi kuimba zile nyimbo kwa kina sana na zaidi aliweza kunieleza kwa kina kwamba Afrika kusini ni nchi inayopatika eneo la kusini mwa bara la Afrika. Ili kunielewesha zaidi na vizuri alinionesha ramani ya Afrika kwenye eneo linaloonesha nchi ya Afrika ya kusini na kwa hakika nilimuelewa sana bwana Simya.

Jambo ambalo nalikumbuka sana katika yale mazungumzo yetu ni kwamba baada ya yale mazungumzo yetu nilianza kuipenda sana nchi ya Afrika kusini. Niliendelea kufuatilia habari za Afrika ya kusini kutoka kwa walimu na Redio ya Sauti ya Ujerumani (DW) na vyombo vya habari vya hapa nchini tangu wakati ule na hata baada ya uhuru wao mwaka 1994.

Nilipomaliza darasa la Saba tayari nilikuwa nimeshakata shauri kwamba lazima nitatafuta fedha ili niende Afrika ya kusini. Nilijiapiza kwamba siku nitakapo bahatika kwenda Afrika kusini nitakwenda kufanya kazi kabisa na ikiwezekana nitakaa moja kwa moja bila kurejea tena Tanzania. Hivyo, nikaanza kujiandaa kutimiza hiyo ndoto yangu ya Muda mrefu.

Katika kipindi chote ambacho nilikuwa nasoma sekondari, yaani miaka minne ya o-level, nilikuwa najiandaa kwa safari yangu kiujuvi, kirasilimali na kisaikolojia. Baada tu ya kumaliza kidato cha nne, mwaka 2003, kabla hata matokeo hayajatoka, niliamua kuanza safari yangu ya kwenda Afrika ya kusini na malengo yangu yalikuwa ni kufika katika jiji la Johannesburg.

Story hii inaeleza visa na mikasa ya safari za watu wanaojaribu kwenda Afrika ya kusini bila ya kufuata utaratibu, Kwa hiyo, utaweza kusoma safari zangu zote mbili ambazo nilizi- fanya kati ya mwaka 2004- 2006.

Naamini wasomaji wa stori hizi hasa watu ambao bado wana ndoto za kuzamia Afrika ya kusini watakuwa na jambo la kujifunza katika safari zao.

*************************​

Kuanza kwa Safari
Mwezi Januari mwaka, 2004 nilipanda gari aina ya Fuso kutoka katika mji mdogo wa Namanyere ambao ni makao makuu ya wilaya na Nkasi mkoani Rukwa hadi Sumbawanga mjini makao makuu ya mkoa wa Rukwa, kwa kuwa sikuwa na uwenyeji wowote wa mji huo nilipofika nilimta futa rafiki yangu ambae alikuwa anaitwa Edward mizimu. Lengo la kumtafuta bwana Edward ilikuwa ni kwa kuwa malengo yangu kwanza ilikuwa ni kusafiri hadi kufika hapo Sumbawanga hadi jijini Lusaka, mji mkuu wa Zambia, na baada ya hapo ndipo nikajipange kuitafuta Harare mji mkuu wa Zimbabwe.

Ndugu Edward alikuwa na ABC za namna ya kufika Lusaka kutokana na kufanya ziara chache kwenda kwa ndugu zake waliokuwa wanaishi huko Lusaka Zambia. Baada ya kukutana na ndugu Edward Mizimu, tulifanya mjadala wa kina sana, ambapo aliweza kunipa changamoto zinazo weza kuipata safari yangu, pia alinishangaa sana kuona naanza safari bila kuwa na nyaraka yoyote ya kusafiria alinishauri nizitafute lakini nikamwambia mimi malengo yangu nataka nikifika kule nisirejee nchini hivi karibuni sasa nikienda kihalali naweza kugundulika mapema.

Baada ya majadiliano marefu alinipa njia mbili ambazo naweza kuzitumia kusafiria ambapo alisema njia ya kwanza naweza nikapita njia ya Kasanga ambapo nitalazimika kwenda kupanda Meli ya Mv Liemba kutoka Kasanga hadi Mpulungu ambao ni mji wa bandari kwa Upande wa Zambia, katika Ziwa Tanganyika, aliniambia kwamba kwa kupitia njia hiyo kuna vikwanzo vingi vya wanausalama wa Zambia na ni ndefu sana. Baada ya maelezo ya njia hiyo alinieleza njia ya pili ambayo ilikuwa ni kupitia Tunduma-Nakonde.

Alisema njia hii unakwenda moja kwa moja Lusaka kwa barabara lakini changamoto yake ni kwamba ina vizuizi vingi vya barabarani vya Polisi na Uhamiaji, alisema ni njia ambayo ni ngumu sana kutoboa kama huna nyaraka za kusafiria. Baada ya maelezo ya bwana Edward ambayo yalikuwa yameambatana na vitisho na tahadhari nyingi bado sikukata tamaa, zaidi nilichukulia kama changamoto za kawaida katika safari. Nilifanya uchambuzi wa njia zote mbili na kisha niliamua kuchagua njia ya kupitia Tunduma-Nakonde.

Baada ya siku kama nne za kukaa pale sumbawanga mjini nikiwa napanga na kuchora ramani zangu vizuri, hatimae nilianza safari ya kuelekea Tunduma kwa njia ya Lori moja hivi nakumbuka lilikuwa Limeandikwa Nyuma Kanjiranji Trans. Tuliondoka Sumbawanga jioni ya Saa moja tukiwa mimi, Dereva na Makondakta wawili, Gari ilikuwa imesheheni mifugo aina ya Ngombe, kwa hivyo safari
ilikuwa inakwenda taratibu sana, Ilikuwa ni msimu wa mvua maeneo yale na barabara wakati ule ilkuwa haina lami kwa hivyo ilikuwa imeharibika sana. Tulitembea usiku kucha huku tunapiga stori za hapa na pale, kwa bahati mbaya tulipofika maeneo ya kijiji cha chiwanda Gari iliharibika rejeta.

Kutokana na mawasiliano ya wakati ule kuwa magumu pamoja na kwamba kuufikia mji wa Tunduma zilikuwa zimebaki kama Km 30 tu, tulijikuta tuna tumia siku nne pale kijijini. Ilibidi asubuhi kondakta mmoja aende Mbeya mjini kumchukua fundi wa Rejeta kisha wakaja kufungua rejeta wakaenda nayo kuchomelea Tunduma mjini ndipo siku ya tatu usiku wakarejea na hatimae siku ya nne ndipo tukaendelea na safari yetu. Siku zote hizo nne za mkasa wa gari kuharibika nilikuwa nimegeuka na kuwa mchunga ng’ombe.

Nakumbuka nilikuwa nachungia sehemu moja hivi ya pembeni ya kijiji cha Chiwanda ambayo iliitwa Ntachimba. Nilifanya kazi ile kwa moyo sana kutokana na utu wa wale jamaa wa gari ambao walinibeba bure na walikuwa wananinunulia chakula wakati wote wa safari, walikuwa ni watu wema sana, nakumbuka wakati tunaanza safari walikuwa wameniambia kwamba nitalipa nauli ya Tsh 5000 lakini baada ya changamoto za barabarani waliamua kunifanya sehemu ya safari yao hivyo sikulipia chochote.

Baada ya gari kupona tulipakia Ng’ombe na kuanza safari tena, ilikuwa kama saa 10 jioni hivi wakati tunaiacha Chiwanda. Haikuchukua muda mrefu Sana kwani baada ya Kama dk 50 hivi tulifika Tunduma katika eneo linaloitwa Mwaka. Wale jamaa walinijulisha kwamba natakiwa nishukie pale ili wao waendelee na safari ya kuelekea mbeya mjini.

Baada ya kushuka mwaka sikujua wapi nielekee kutokana na ugeni wangu, nilikuwa nimefanya kosa wale jamaa wa kwenye gari sikuwa nimewambia ukweli wa ugeni wangu kwenye ule mji wa kibiashara kwa hivyo kwa kiasi nilianza kupata wasiwasi kwamba sasa kama katika nchi yangu ambayo naelewa Lugha vizuri hali ipo hivyo, huko mbele ya safari mambo yatakuwaje, siyatanikuta makubwa, hata hivyo nilipiga moyo konde na kuendelea na kutokuruhusu roho wa uoga.

Nilikwenda kutafuta chumba cha kulala sehemu moja inaitwa mpakani, kisha nikapata chakula kwa mama ntilie ilikuwa kama saa moja hivi jioni, muda wote nilikuwa nafuatilia stori zinazohusu wazamiaji wa kuelekea Zambia kutoka kwa watu mbalimbali ili nijue namna ya kuvuka Boda ya Tanzania na Zambaia. Jioni hiyo sikufanikiwa kupata habari zozote za maana za hitaji langu. Kesho yake asubuhi niliamka muda wa kawaida kwa sababu sikupanga kuondoka siku hiyo.

Kitu nilicho kifanya siku hiyo ni pamoja na kutafuta habari za safari yangu kwa tahadhari ili nisije nikakamatwa mapema, bahati nzuri kwenye Nyumba ya wageni niliyofikia nilimuona kijana mmoja hivi mcheshi mwenye umri wa rika langu, nikajitahidi kujenga urafiki nae kwa muda mfupi kisha baada ya kumuamini na kupima uelewa wake niliamua kumshirikisha mpango wangu, akaniambia unaweza kufanikiwa lakini kuna vikwazo vingi japo huwa kuna watu wengi tu wanafanikiwa harakati zao za kuzamia Bondeni kwa mzee
Madiba. Kwa hiyo, alinishauri mambo mawili, la kwanza akasema kwamba nibadilishe fedha zangu kutoka shillingi kuwa Z-Kwacha na US-Dollar.

Na la pili nisipandie gari stendi ya hapo boda, bali nivuke boda kwa miguu kisha nikapandie gari mbele ya safari ili niweze kukwepa kizuizi cha mapema cha polisi ambacho kipo nje kidogo mji wa Nakonde upande wa Zambia. Alisema ukikwepa hiyo ‘road block’ utakuwa umefanikiwa kuingia Kilomita nyingi sana ndani ya Zambia. Alinisaidia kubadilisha hela zangu kiasi cha Tsh 370,000 kuwa Z-kwacha na US-dollar na kisha baada ya zoezi hilo aliniambia kwamba ataniunganisha na mjomba yake ambae hufanya biashara za kuvusha sukari ya magendo na mafuta ya petrol upande wa Zambia ili aniombee lifty kwenye gari yake atakapo kuwa anakwenda kwenye madili yake.

Siku hiyo hiyo majira ya mchana yule bwana alinipeleka kwa mjomba yake huyo ambae alikuwa anaishi upande wa Zambia kwenye mji wa Nakonde, baada ya kufika nilimueleza shida yangu na bahati nzuri yule uncle alikuwa hana shida yoyote, akanikubalia akaniambia nitatakiwa niondoke nae siku hiyo hiyo saa 4 usiku na atakwenda kuniacha sehemu moja hivi inaitwa Isoka umbali wa Km 84 kutoka Nakonde, kisha akanishauri kwamba kwa kuwa wewe ni baharia yaani mzamiaji, itabidi usiku huo huo utafute usafiri wa Lori uondoke ili uweze kusogea mbele zaidi ndani ya Zambia ili angalau ufike hata Isoka umbali wa Kama Km 146.8.

Muda wa kuondoka ulipofika tulipakia mafuta ya petroli kwenye gari ndogo aina ya Toyota peak up ambayo yalikuwa yanavushwa upande wa zambia ili wakati wa kurudi warejee na sukari. Baada ya kumaliza kupakia mida ya Saa nne na nusu usiku tuliondoka kwa babarabara kuu iendayo Lusaka na tulipo tembea umbali wa kama Km 5 tu hivi, tulikuta Road Block ya askari polisi wa Zambia. Kutokana na umaarufu wa uncle Chilo tulivuka bila shida, kisha tukatembea Km 10 nyingine tukakutana na Gari aina ya Toyota Land Cruiser, ikatupita kimashamasha sana lakini kwa kasi sana.

Uncle Chilo akasema itakuwa ni watu wa ZRA (Mamlaka ya mapato ya zambia) au Migration wapo kwenye patro, akasema kwa anavyowafahamu kutokana na uzoefu wake kwenye hiyo barabara, lazima watarudi kwa hivyo akazima taa za gari na kisha akaliingiza kwenye kinjia cha porini umbali wa kama Km 1 hivi.

Baada ya muda wa kama dakika 10 hivi ile gari tuliyopishana nayo ilirudi ikiwa kwenye mwendo wa kawaida uncle Chilo akatukumbusha yale maneno yakeya kwamba alisema watarudi, basi tukakaa pale porini kama dk 30 tukaondoka. Wenyeji wangu walisema kwa huo muda hawawezi kurudi tena.

Tulirudi barabarani kisha muda mfupi tu, baada ya kurejea barabarani tukaona gari inakuja mbele yetu, wote kwenye gari tulitulia kimya kila mtu akiwa na wasiwasi sana huku akisubiri kitakachotokea!

Itaendelea...
Tushachoka kulishwa matango pori acha na ww tukuone
 
SAFARI YA KUZAMIA AFRIKA KUSINI KWA NJIA ZA PANYA.

Sehemu ya pili.

Wote kwenye gari tulitulia kimya kila mtu akiwa na wasiwasi sana huku akisubiri kitakachotokea, bahati nzuri tulipopishana
na ile gari ilikuwa gari aina ya Coaster mini bus. Kwa hivyo tukaendelea na safari baada ya saa hivi tukawa tumefika Isoka sehemu ambayo ndio nilikuwa
nashukia, wenyeji wangu pia walikuwa wanarudia pale. Ilikuwa kama saa 6 hivi na eneo lile lilikuwa na baridi kali sana usiku ule nikaenda kwenye kistedi kidogo hivi cha magari, huku naangalia kama naweza
kupata gari hasa Lori, kwenye saa nane hivi usiku lilikuja Lori kubwa aina ya Scania, wale jamaa wa kwenye Lori walikuwa ni watanzania nikaongea nao
wakaniuliza wewe ni baharia mwanangu nikawambia ndio wakaniambia tutakubeba hadi Chinsali ukifika pale utakuwa umesogea.

Wakaniambia wakinibeba zaidi ya pale watapata matatizo mbele ya safari yao.
Basi nikaondoka na wale jamaa niliwapenda kwa sababu walinipa moyo sana, na wakanielekeza vikwazo vya mbela ya safari yangu. Nilifanikiwa kwenda na wale jamaa hadi Chinsali ambapo tulifika asiku ule ule. Baada ya wale jamaa
kunishusha mambo yalibadilika kabisa, kwa sababu mbali ya mazingira kubadilika hata Lugha ilibadilika kabisa sasa nikaanza kusikia watu wanaongea
Lugha yao ya Kinyamwanga, Kiwemba na Kiingereza, hapo nikajua kwamba
sasa ni kweli sipo Tanzania.

Nilianza kuwaza namna ya kutoka pale huku najishauri kama nivizie Lori tena au nipande basi. Nikasogea stendi nikapata uji kwa akina mama wanaouza
uji, pia nikasikia wanasema mabasi yanayotoka Tunduma kwenda Lusaka na
Cooper Belt yataanza kupita saa mbili asubuhi. Nikaamua kujilipua nikakata tiketi kwa wakatisha tiketi ya basi moja hivi ilikuwa inaitwa Jordan. Asubuhi
ya saa mbili hivi basi likafika stand mimi na abiria wenzangu tukaingia ndani
ya basi na safari ikaendelea. Kwenye basi kulikuwa kumetawaliwa na stori chache kwa lugha za kwao, mimi
nilikuwa kimya kabisa nikionekana mtu nisie na amani kutokana na mawazo ya safari yangu ambayo yalitokana na kutokuwa na passport na kitu kingine chochote cha kusafiria nje ya nchi.

Safari iliendelea vizuri huku nikishuhudia nyanda za tambalale na miinuko midogo midogo, pia kulikuwa na misitu ya asili ya kutosha kabisa kando ya barabara. Baada ya muda wa masaa 4 hivi tangu nipande basi hatimae tulikuta mji mkubwa kidogo, na niliposoma kibao cha ule mji niliona kimeandikwa wellcome to Mkushi.

Baada ya muda mfupi hofu yangu ilirudi ghafla baada ya kumsikia kondakta wa basi anasema kwa lugha ya kiwemba “Tufanwe ko mkwai ilefyaikwa ko
ama Reg or amapassipoti”. Yaani samahani jamani inatakiwa muandae na-
tional Identity Card au Passport za kusafiria tumefika kwenye check point ya migration.
Kwa kawaida raia wote wa Zambia wanapo safari ndani ya nchi yao hutakiwa kuwa National Identity Card. Na raia wakigeni wanatakiwa kuwa na passport.
Baada ya dk kama tano hivi gari ilisimama mbele ya Road block na askari wa uhamiaji walikuja wakatuamuru kila mtu atoe passport au National Identity Card. Kama huna ushuke chini, tukashuka vijana watatu ambao tulikuwa hatuna passport wala Reg Id. Tukajaribu kubembeleza kusamehewa ili tuendelee na safari, lakini ikashindikana, ndipo tukarejeshewa sehemu ya nauli yetu na muda huo huo tukawekwa chini ya ulinzi wa askari wenye silaha za kivita.

Sikuamini kilichokuwa kimetokea, tulikaa pale chini ya ulinzi mkali kama dk 15
hivi ndipo ikaja Gari ya polisi na kutupeleka sehemu ambayo nilikuwa siijui ila ni pembeni kidogo ya mji wa Mkushi.

Mbio za Dakika 45.

ulikamatwa majira ya saa sita na dakika arobaini hivi kwa masaa ya Zambia ambapo kwa Tanzania nia saa tano na dakika arobaini, mara baada ya kufikishwa katika kituo cha polisi cha kati tulichukuliwa maelezo ya awali ambayo, yaliainisha kwamba mimi na mwenzangu mmoja ambae alikuwa anaitwa Chiteba tulikuwa ni ‘foreigners’ ambao tuliingia katika nchi
ya watu bila utaratibu na mwenzetu mmoja ambae alikuwa anaitwa Rodrick Chanda alikuwa ni Mzambia ambae kwa bahati mbaya alikuwa anatafutwa na
polisi kwa muda mrefu kutokana na matukio ya kiuaharifu na ujambazi wa kutumia silaha ambao alikua anatuhumiwa kuufanya maeneo ya Cooper Belt
katika miji ya Ndola, kitwe na Mfulira.

Wale wasomaji wa zamani mtakuwa mnaikumbuka timu mashuhuri kutoka
katika mji wa Mfulira iliyoitwa Mfulira Wanderers F.C miaka ya 1970, Namaanisha jamaa alifanya uharifu katika maeneo hayo. Kwa hivyo tukapatikana wahalifu wa aina mbili yaani sisi kama watu tulioingia nchini kwao kinyume cha sheria na bwana Chanda ambae alikutwa na tuhuma za uhalifu wa kutumia
silaha.

Kutokana na muktadha wa tuhuma zetu hasa kukamatwa pamoja na jambazi Sugu ulinzi uliimalishwa sana katika eneo la polisi na utaratibu ukaanza kuan-
daliwa mara moja wa kutusafirisha kwenda makao makuu ya hilo jimbo la kati
(central Province) ambayo ni Kambwe. Kwa kweli mambo yalikuwa yamebadilika sana, nilibadilika ghafla kutoka msafiri wa kawaida katika nchi ya watu
na kuwa mwalifu ambae nimekamatwa pamoja na jambazi sugu, siku hiyo
hatukusafirishwa, tulijulishwa kwamba taratibu za kutusafirisha kutupeleka Kambwe makao makuu ya jimbo hilo la kati zinafanyika.
Tukalala sero siku hiyo, tuliwakuta jamaa wengi tu pale ndani wakiwemo
wenye makosa kama yetu ambao walikuwa wanasubiri kusafirishwa kwenda makwao watuhumiwa wote walikuwa wamekaa sero kwa vipindi tofauti tofau-
ti kutegemea na tarehe uliyo kuwa umekamatwa.

Wapo waliokuwa wamekaa mwezi mmoja, sita, n.k. Pale ndani palikuwa story nyingi hasa kwa waliokuwa na makosa ya uzamiaji,
cha ajabu ambacho hata mimi kilinijenga sana ni kwamba pamoja na msoto wa pale wa kula mlo mmoja wa saa tisa hadi kesho yake tena saa tisa na kutumia debe kujisaidia mbele ya wenzako, bado watu wale walikuwa wameapa kwamba lazima watatimiza ndoto zao za kufika Afrika ya kusini. Tuliendelee kukaa pale hadi siku ya nne huku tukiwa na tumaini la kwamba labda tutasa-
firishwa kurudi Tanzania ili kuja kushitakiwa kwenye mahakama zetu, kwa kawaida ukikamatwa nje ya nchi yaani ndani ya SADC, kwa kosa kama letu
inatakiwa urejeshwe nchini kwako ili ushitakiwe katika mahaka zenu.

Siku ya nne mapema asubuhi tuliitwa mimi na wale wenzangu ambao nilikamatwa nao siku moja, Kiteba na Chanda. Tukatoka nje mara baada ya kufika nje tukaambiwa kila mtu arudi ndani akiwa amebeba debe la mtondoo, kulikuwa na ndoo kubwa na ndogo mbili. Yule bwana Chanda akabeba ndoo kubwa, mimi na bwana Kiteba tulibeba zile ndogo.

Tuliongozwa kuzipeleka sehemu ya kwenda kumwaga ambayo ilikuwa na shimo kubwa karibu na msitu mkubwa wa kupandwa, tulisindikizwa na askari
wawili mmoja akiwa na silaha nzito ya kivita na mwingine na kifimbo tu. Tuliongozwa sehemu ya shimo baada ya kulisogelea shimo nilisikia kishindo
kizito puuuu, nikageuka lakini hata kabla sijageuka nikasikia harufu kali sana
ya kinyesi nikiwa bado nashangaa nikaona askari aliyekua na silaha yupo chini akiwa amevikwa debe la mavi, anapiga kelele kisha nikamuona Chanda
anakimbia kwa kasi kuelekea msituni huku ana tuita mimi na yule mwenzangu.

Hatukuzubaa tukamfuata mbio kutokomea msituni, tukiwa bado hatujafika
mbali tukasikia king’ora cha hatari kimepigwa bila shaka polisi walikuwa wanaitwa kwa dharura. Tulikimbia mfululizo kama dakika 45 hivi bila kusimama, ulikuwa ni msitu mzito sana ambao kadri tulivyokuwa tunakimbia ndivyo ulizidi kuwa mzito.

Baada ya mwendo mrefu tulisimama yule kiongozi wetu wa muda bwana
Chanda alitwambia kwamba ukikamatwa na polisi, kama unajua kesi yako ni kufungwa hakikisha hushindwi kwa urahisi, vijana njooni tupambane kadiri
inavyo wezekana tuikwepe jela. Kisha akatwambia hilo eneo halijui vizuri lakini anakumbuka baada ya huo msitu kuna upande kuna Game reserve ambayo inawanyama wengi tu hatari
kwa hivyo akatujulisha kwamba mbali ya hatari ya polisi tuliyoikimbia kuna hatari ya wanyama mbele ya safari yetu. Pia alitwambia haitakiwi tuumalize msitu wakati wa mchana kwa sababu inawezekana polisi wakawa wameweka
mtego mbele. Kwa hivyo tulitafuta sehemu tukatulia kwanza, kila mtu alikuwa na njaa kali kutokana na kwamba tulikuwa tumekula kwa mara ya mwisho
siku ya jana yake saa tisa jioni ilikuwa imepita zaidi ya masaa 18 bila kula wala kunywa.

Tukiwa pale tulipojificha kila mtu alieleza historia yake na mikakati yake ya maisha, maelezo ya Rodrick Chanda yalinisaidia kumjua vizuri, sasa nilijua kwamba alikuwa ni mhalifu sugu ambae anaweza kufanya lolote muda wowote hata kama ni kuondoa uhai wa mtu, ndipo nikahisi nipo katika hatari kubwa sana ambayo sasa nipo nayo sentimita chache sana. Kwa upande wa ndugu Kiteba niligundua kwamba yeye ni Mganda na ni mzamiaji tu kama
mimi ambae alikuwa kwenye harakati za kuzamia Afrika kusini.
Tulikaa pale mafichoni hadi saa tano usiku ndipo tukaanza kusogea mbele tukiongozwa na kamanda wetu Chanda, tulisongea kwa muda wa kutosha hadi tulipoona msitu unakwisha.

Tulipomaliza msitu umbali kama wa Km 15
hivi tulikuta kibao kimeandikwa kwamba eneo hilo ni game reserve, nikakumbuka maneno ya bwana Chanda aliyokuwa ametwambia awali kuhusu game reserve. Alisema tukifika eneo hilo tuongeze umakini kwani tunaweza kukuta-
na na wanyama hatari muda wowote, tukaendelea kwenda mbele zaidi lakini
baadae tukaamua kuacha kwenda ilikuwa ni usiku sana, halafu tulihisi kama kuna mnyama hatari anatufuatilia tukatulia kimywa baada ya muda wa kama
dakika tano hivi walijitokeza simba wanne mbele yetu, nilitetemeka sana nika-
jua sasa hapa ndio mwisho wangu.
Wenzangu walikuwa na unafuu kidogo, bwana Chanda akasema tukithubutu kukimbia kuna mmoja kati yetu ataliwa kwa hivyo tutulie pale pale, akasema
tugeuke tupeane migongo alafu tu chuchumae chini, baada ya kuchuchumaa
chini wale simba nao wakawa wamelala kwa tahadhali, baada ya muda walitufanyia vituko vya kurusha mchanga, kutimua vumbi na kuunguruma kwa
nguvu lakini kwa kuwa tulijua tunatetea maisha yetu kwa karata ya mwisho tuliendelea kuwa imara kabisa.

Simba wale walikaa pale hadi asubuhi, majira ya saa nne hivi tukiwa bado tumezungukwa na simba walikuja watu wa game reserve wakatuokoa, lakini hatukuokolewa hivi hivi tulikamatwa kama wawindaji haramu. Sasa tukawa na makosa mawili la kutoroka kituo cha polisi na la uwindaji haramu na yale ya
awali. Tulisafirishwa kutoka pale kwa magari yao hadi upande wa pili wa ‘game reserve.’ Tukawekwa chini ya ulinzi wao wakati mawasiliano yanafanyika na polisi na mbaya zaidi walikuwa wanawasiliana na wale wa kituo tulichotoroka, mambo yalikuwa magumu sana, niliwaza namna polisi alivyoogeshwa mavi halafu tunarudishwa tena kituo kile kile sikupata picha kipigo kitakuwaje, moyoni nikajisemea kuwa tutapigwa hadi tufe au wakiamua watatupiga risasi halafu waseme ilikuwa ni majibizano ya risasi kati yetu na polisi.

Itaendelea....
 
Stor yko ipo inspired mkuu
 
hatari sana, polisi kumwagiwa debe la mavi duuuuhhhh

😀😱
 
Back
Top Bottom