Uzamiaji Afrika Kusini: Mikasa katika harakati za kuzamia Afrika Kusini kwa njia za panya

Uzamiaji Afrika Kusini: Mikasa katika harakati za kuzamia Afrika Kusini kwa njia za panya

SEHEM YA 5

Tulibaki pale pale porini kama dakika arobaini nyingine tukiwa hatujui
la kufanya, ghafla nikamuona rafiki yangu Jim ambae nilibaki nae pale
porini anaanza kufurahi kwa kurukaruka nikamuuliza kulikoni mwenzan-
gu akaniambia dogo tumetajirika.
Akaendelea kusema wewe si unatafuta hela sasa zimejileta zenyewe, si-
kumuelewa lakini baadae akaniambia kwamba nafasi kama hiyo alikuwa
anaiombea sana kwa muda mrefu sasa imewadia akaniamuru inuka twende,
basi tukaanza safari ya kuelekea barabarani, nikamshauri kwamba kwa nini
tusirudi Lilogwe tukawakomboe jamaa zetu akasema dogo we achana nao,
bosi wao atakuja kuwatoa.
Baada ya muda mfupi ikapita gari dogo ya abiria coster, tukapanda ilikuwa
inaelekea Boda ya kasumulo upande wa Tanzania Sehemu ambayo tulikuwa
tunaelekea haikuwa mbali sana kutoka pale mwendo wa masaa kama mawili
na nusu hivi, kabla hatujafika boda ya Kasumulo ilikuja gari ya polisi ile ile ya
mwanzo ambayo iliwachukua jamaa zetu ikatupita na kisha ikapaki Mbele ya
gari yetu.
Baada ya hapo wakashuka askari na kuamuru abiria wote tushuke, ikafanyika
searching ya nguvu pale na hatimae mimi na yule jamaa yangu tukabainika
kwamba tumebeba mihadarati kwa hivyo tukakamatwa na kurejeshwa tena
Lilogwe polisi central, tulipofika pale polisi tulikuta wale wenzetu wapo kaunta
bado wanachukuliwa maelezo, walipo tuona wakakubaliana kwamba waseme
hawatujui ili wasiingie kwenye mtego wa madawa lakini pia itakuwa rahisi
kututoa tukiwa wawili kuliko timu nzima ikiwekwa ndani.
Tulichukuliwa maelezo na kisha tukawekwa sero, kesho yake ikawa ni siku ya
kusafirishwa kutoka Malawi mimi kuja Tanzania na Jim kwenda kwao Zam-
bia kwa sheria za kimataifa mhalifu anatakiwa arejeshwe kushitakiwa nchini
kwao. Kwa hivyo, mimi niliungana na watanzania wengine watatu ambao naowalikuwa wanarudishwa kwa makosa mbalimbali.
Polisi ya Malawi walikuwa tayari wameshawasiliana na wenzao wa Tanzania
kwa hivyo tulipofika tu pale boda tulikuta gari jingine la polisi wa Tanzania lik-
iwa na askari wa kikosi cha FFU. Tuliposhushwa tu makabidhiano ya kimaan-
dishi yakafanyika na baada ya muda mfupi safari ya kuelekea Mbeya ikaanza,
sikuwa na hofu sana kutokana na uzoefu wangu kwenye matukio kama hayo.
Tuliondoka Boda pale saa mbili asubuhi, tulipofika Mbeya maeneo ya Uyole
kwenye muda wa saa tano hivi askari mmoja alishauri kwamba kwa kuwa
tumeondoka Boda kasumulo Kyela bila ya kula sisi na wao wenyewe tupit-
ie kwenye mgahawa tule mana tusipokula tukifika centra itatuchukua muda
mrefu sana kutuchukua maelezo. Wazo lake likakubalika na mkuu wao wa
msafara na kisha tukaamuliwa kushuka wote kwenda kula, tulipofika ndani
wakatutoa pingu tukaagiziwa chakula, walikuwa ni askari wastarabu sana.
Tukaanza kula, nikiwa nakula nilichungulia sehemu ya jikoni ya ule mgahawa
nikaona kuna mlango wa kutokea nje, pia ilikuwa ili uende chooni unapita
kwenye korido la kupitia karibu na hapo jikoni, nikawaza kwamba ngoja nijari-
bu bahati yangu ya mwisho ya kujiokoa na jela. Nikaomba kwa afande kuwa
naomba niende chooni akakubali kwa kujiamini kwamba choo kipo mle mle
ndani alikuwa hajauona ule mlango wa jikoni.
Nikaenda uani kweli lakini sikukojoa kwa sababu nilijua zile dakika za kukojoa
ndio za kuzitumia kwenye jaribio langu la kutoroka, kwa sababu nilijua ikipita
muda wataanza kuwa na wasiwasi. Kwa hivyo nikageuka haraka nikainama
nikatokea sehemu ya jikoni nikamkuta dada anapika nikatoa dola kumi pale
kumonesha yule dada akasema hapana baba nenda tu zitakusaidia mbele ya
safari.
Nikatoka pale kwa mbio za wastani nikatembea mita kama 40 hivi, nikakumbu-
ka lile begi lenye mali limebaki kwenye gari ya polisi. Nikaanza kurudi kuelekea
gari ya polisi ilipo huku roho nyingine inaniambia niondoke, nikapiga moyo
konde nikaenda hadi pale kwenye defender la polisi nikachukua kile kibegi na
kutokomea nacho Uyole ya kati. Kilichobaki kikaendelea Mimi sijui ila nina-
chokumbuka ni kwamba mimi nilipona kwenye hiyo issue kimaajabu, nadhani
itakuwa ni Mungu mwenyewe aliamua kuniokoa.
Nilipofika maeneo ya Uyole ya kati nilivuka upande wa pili wa barabara, Mbeya
sikuwa mwenyeji kwa hivyo faida tu niliyo kuwa nayo ni kwamba nilikuwa
naongea lugha ambayo naijua vizuri yaani Kiswahili. Nilitembea hadi eneo
linaloitwa Igawilo karibu na eneo wanaita Road kuna baa moja inaitwa Mbigu-
ni ambayo inaambata na vyumba vya wageni, nikachukua chumba pale kwa
ajili ya kulala nilipo kamilisha taratibu za kukabidhiwa chumba nikatoka nje
kutafuta chakula.
Nikiwa pembeni kidogo ikafika gari ya polisi ikiwa na speed kali na haraka
sana hata kabla haijasimama vizuri askari waliruka na kuizunguka ile bar. Ba-
hati nzuri nilikuwa mbali kidogo kwa hivyo nikajivuta pembeni kidogo nikawa
nachungulia kwa mbali ili nione kitakachotokea na hasa kuhusu begi langu
nililoacha ndani. Baada ya msako wa kama dakika 10 hivi niliwaona wametoka
na lile begi langu lenye mihadarati, kwa kiasi fulani sikusikitika sana kwa saba-
bu niliona wamenitua mzigo ambao sikuwa najua pa kuupeleka.
Nikaondoka pale na usiku huo huo nikafika Mbalizi. Nikaulizia njia ya kwenda
Chunya na kaondoka usiku ule ule na gari aina ya Fuso iliyojaa shehena ya
bidhaa za dukani, nilikwenda nayo hadi sehemu moja hivi inaitwa Mkwajuni
ambapo tulifika saa moja asubuhi. Nilivyolisoma eneo la mjini pale Mkwa-
juni nikaona kuna kituo cha polisi, nikahisi watakuwa wanataarifa zangu kwa
hivyo nikaamua kuondoka na kwenda sehemu moja hivi inaitwa Saza sehemu
ambayo nilijua hawatanishangaa kutokana na ukweli kwamba eneo lile lina
machimbo ya madini ya dhahabu kwa hivyo si rahisi wenyeji kukushitukia ku-
tokana na eneo hilo kutapakaa wageni wengi. Nikaweka kituo kwa siku kadhaa
pale huku nafanya tafakari mwanana kabisa ya safari yangu ya kuzamia Afrika
ya kusini ilivyoshindwa kutimia.
Hivyo ndivyo jaribio langu la kwanza la kwenda kuzamia Johannesburg Af-
rika ya kusini lilishindikana katika utaratibu huo uliojaa maajabu ya kutisha,
nilijikuta nimerejea Tanzania bila gharama zozote za nauli wala chakula, nil-
isafirishwa na kulishwa kwa sehemu kubwa na polisi wenyewe, kilichobaki
kinaendelea kwa yule jamaa yangu mganda Kiteba pale Lusaka sikujua, pale
Malawi kwa wale vijana wa bosi mzungu sikujua na hata kwa bwana Jim am-
bae alisafirishwa kutoka Malawi kurudi kwao Zambia sikujua, nilichojua tu
ni kwamba serikali ya Zambia, Malawi na Tanzania zilikuwa zinanitafuta kwa
matukio yaliyotokea.
Pamoja na hayo, nia na sababu ya kurejea tena safari yangu ya kuzamia Afrika
ya kusini ilikuwa pale pale na ndio kwanza nilianza kujipanga upya mara moja
nikiwa pale pale Saza-Mkwajuni Chunya mahali ambapo siku hizi ni makao
makuu ya wilaya mpya ya Songwe.
Mkuu embu shusha epsod ya sita Mkuu nipitia wakt nasubiria mama kuzungumza nyongeza
 
Hii ni link au "view attachment"? Unaelewa maana ya view attachment mkuu?

Anewei tupe heading ya huo uzi ulioweka hiyo link ili tuutafute wenyewe, maana hujui ku paste link.
Kama unepata link tafadhali wasilisha
 
SEHEMU YA 6

Nilikaa pale Saza kwa muda wa wiki moja nikiwa na washikaji wachimba
madini huku tukiwa tunapiga stori za hapa na pale, walikuwepo watu wa
kutoka mikoa mbalimbali na hata nchi jirani kama Malawi, Mozambique
na Uganda.
Baada ya kukaa wiki, niliamua kuondoka kuelekea machimbo mengine ya
dhahabu huko Mpanda mkoa wa Katavi. Niliamua kwenda kujaribu kuchim-
ba dhahabu ili kama nikifanikiwa nipate fedha za kuniwezesha kuanza safari
yangu kwa mara nyingine ya kwenda Afrika ya kusini. Pia niliamua kuondoka
Chunya kwasababu nilijua Askari wanaonitafuta hawapo mbali sana na mimi
wale wa Mbeya mjini na pia eneo sikulipenda sana kutokana na kuwa na watu
wengi sana.
Wakati naondoka nilikuwa nimebakiwa na kiasi cha fedha kidogo sana amba-
cho ilikuwa ni Tsh 300 tu. Kwa hivyo nilianza safari yangu kwa njia ya miguu
kuelekea ziwa Rukwa. Nikatembea kama masaa 4 hivi nikalikuta ziwa Rukwa
kwenye kambi ya wavuvi, wale wavuvi walinisaidia chakula, pia waliniambia
kwamba kwa kutembea kwa miguu safari yangu ingechukua hata wiki nzi-
ma ndipo nifike ninakokwenda. Kwa hivyo wakanishauri nisuburi kesho yake
nivuke ziwa na mtumbwi, ukivuka ziwa tu tayari unakuwa umefika mkoa wa
Rukwa. Kwa hivyo kesho yake niliondoka nao kwa kutumia kimtubwi kidogo
ambacho hakitumii mashine kuendeswa, tukaabiri muda mrefu wa kutosha
ndipo tukafika upande wa pili wa ziwa.
Baada ya kufika upande wa pili niliendelea kuambaa na mbonde la ziwa Rukwa
hadi nilipofika sehemu inayoitwa Maji ya moto-Mpibwe, nikaweka kituo pale
kama siku tatu hivi kisha nikaendelea na safari yangu ya kuelekea kwenye ma-
chimbo ya dhahabu Mpanda lakini kabla sijatoka pale Maji ya moto nilikutana
na jamaa moja akanishauri kwamba kama nataka kufanikiwa huko kwenye
madini niende nikamuone mtaalamu (mganga wa jadi) ili atengeneze mambo
yangu.
Nikamwambia tatizo nililonalo kwa wakati huo ni kwamba fedha nilikuwa
nimeishiwa kabisa hata safari yangu nilikuwa naifanya kwa kutembea kwa
miguu, kutokana na ukosefu wa fedha hata chakula nilikuwa naomba tu kwa
wasamalia wema au wakati mwingine nafanya vibarua. Nakumbuka hata huyo
jamaa nilikutana nae wakati tunafanya kibarua cha kuvuna mpunga kwenye
shamba la jamaa mmoja alieitwa msukuma.
Yule jamaa akaniambia atanipeleka kwa huyo mzee mtaalamu kwa sababu
yeye anafahamiana nae hata kama hatuna fedha atatusaidia, nikamkubalia
siku iliyofuata tukaenda kwa huyo mtaalamu wake na kwa kuwa walikuwa
wanafahamiana tulipo fika tulipokelewa vizuri sana kisha nikamueleza shida
yangu kwa kusaidiwa na yule jamaa yangu.
Mzee huyo aliekuwa anaitwa Matofari akakubaliana na maombi yetu, akasema
kwamba dawa yake ina masharti kidogo ambayo yatachukua dozi ya siku tatu
kunitengeneza. Akasema dawa zake huwa hazihitaji kafara yoyote. Kwa hivyo
akaniambia nisiwe na wasiwasi lakini kinachotakiwa ni ujasiri na uaminifu.
Akaseme tutaianza dozi kesho yake alfajiri.
Ilipofika saa 11 alfajiri, nikaamshwa nikapelekwa kwenye jalala la takataka la
huyo mzee nikakalia chungu kikubwa cheusi, nikawekewa mkia wa ng’ombe
kichwani, yule mzee akiwa anasema maneno ambayo sikuyaelewa. Baadae
akaanza kunichanja miguuni na mikononi huku ananipaka dawa.
Baada ya hapo tukaondoka pale kwake na kwenda umbali wa Km kama 15
hivi polini kwenye pango analofanyia kazi nikaendelea kutengenezwa. Baada
ya hapo tukarejea nyumbani akaniambia kuwa zoezi la kwanza limekamilika
imebaki mazoezi ya kupima ujasiri, kwa hivyo akasema ikifika jioni ya saa 11
atalianza hilo zoezi, muda ulipofika akaniambia niingie kwenye moja ya vyum-
ba vyake vya kiganga nikaingia kisha akafunga mlango.
Baada ya mlango kufungwa gafla chumba kile kilijaa giza nene na kikabadilika
ukawa msitu mnene mithiri ya misitu ya Kongo au amazon, wakati naingia
sikupewa siraha yoyote kwa hivyo nikajikuta nipo mwenyewe tu pia aliniambia
kitu chochote kikija nisikifanye kitu chochote, nikiwa na hiyo kumbu kumbu
ghafla mbele yangu nilimuona chatu mkubwa anakuja mbele yangu kwa ki-
asi nikapatwa na ganzi mwili wote, nikatulia yule chatu akaja akapita kwenye
uvungu wa miguu yangu hali yangu ilikuwa mbaya sana

Chatu alipomalizika tu akaja chui na mtoto wake alionekana ana njaa kali sana,
akaja akaninusa nusa na kuniramba akaondoka nikajua nimepona lakini niki-
wa natafakari hilo alikuja nyoka aina ya cobra akawa ananirukia kifuani lakini
nilikomaa sikumfanya kitu. Baada ya cobra wakaja simba wanne hawa siku-
waogopa sana kwa sababu nilikumbuka jinsi tulivyo wadindia wale simba kule
Zambia hadi tukaokolewa kwa hivyo pamoja na ukweli kwamba nilikuwa na
wasi wasi sana lakini bado nilikuwa na faida ya uzoefu wa simba walau hilo
lilikuwa tukio la pili.
Baada ya hayo majaribio hatimae saa tatu usiku nilijikuta nipo kwenye chum-
ba cha kawaida kabisa nikalala hadi asubuhi, Yule mzee akasema kijana wewe
ni shujaa sana kwa hivyo umefanikiwa majaribio yangu yote. Akanipa dawa na
hela kiasi cha Tsh 5, akasema utaendelea kutumia hii hela kwa kitu chochote
hadi utakapo pata hela zitakazotokana na madini aina ya dhahabu, nikashan-
gaa sana na kujiuliza kweli haya yanawezekana, basi nikamalizana nae lakini
akaniambia ukishapata mali, ukiuza uje na hela zote hapa kabla hujatumia hata
senti moja ili nije nikutengenezee dawa ya kukuongoza na kulinda pesa zako,
akasisitiza kwamba hakikisha unazingatia hilo usipofanya hivyo mambo yako
yataharibika.
Baada ya hapo nikaondoka kwa mzee hadi maji ya moto sehemu ambayo
nilionana na yule rafiki yangu alienipeleka kwa mzee ambae yeye alitangulia
kuondoka, nikamuelezea yote yaliyojiri kisha nikaenda stendi nakuchukua gari
nikiwa na ile Sh 5, yangu huku nina kawasiwasi kidogo kama wataikubali hela
yangu. Muda wa nauli ulipofika nikatoa ile shilingi 5 yangu konda akapoke
akanirudishia na chenji kidogo lakini nikaichukua tu ile hela yangu zingine
nikamrudishia kuwa umenizidishia chenji. Akanishukuru sana akasema kaka
wewe ni muungwana sana, moyoni nikajisemea hujui utendalo ndugu.
Nikafika mpanda mjini kisha nikapanda treni inayoenda machimboni, siku
hiyo hiyo jioni nikafika kwenye machimbo nikawakuta vijana wengi sana wa-
najiita masorovea wakiwa wanaendele na pilika za uchimbaji. Sikuwa na zana
yoyote ya uchimbaji jambo ambalo lilifanya wachimbaji wenzangu waanze
kunisema kwamba huyu jamaa vipi anakujaje mgodini huku akiwa hana vifaa
wala chakula, wakanitenga akabaki jamaa mmoja tu ambae alikuwa anaitwa
Charles Mwanisandi, huyu jamaa alinitia moyo na akaniambia nitatumia vifaa
vyake wakati najipanga.

Basi siku hiyo hiyo jioni nikaomba jembe na beleshi lake kwa lengo la kwenda
kuandaa sehemu ya kuanza kuchimba dhahabu kesho yake. Nikiwa naandaa
sehemu hilo wakati nafukua mchanga nikafukua jiwe la ajabu sikuwa naijua
dhahabu vizuri lakini lilikuwa ni jiwe lenye uzito wa ajabu. Nikaenda kumu-
onesha yule rafiki yangu, akasema hiyo ni dhahabu pure kabisa. Akanichukua
hadi kwa Wanunuzi, walipoiona wakasema ni dhahabu safi kabisa. Tulipowe-
ka kwenye vipimo ikaonekana ni nzito sana na thamani yake hakukuwa na mtu
mwenye uwezo wa kuinunua. Kwa sababu za kiusalama tajiri mmoja akasema
tuondoke pale usiku ule ule kuelekea Mpanda mjini ili achukue pesa benki
anilipe. Tukaondoka usiku ule ule.
 
Hahaha shusha in (baba levo voice)
Screenshot_20210501_121538.jpg

Hiki ndo kitakachofata🤣🤣
 
Kabisa, pale kwenye ajali polisi wote wakafa halafu wao wakatoka salama tayari nikaona hapa hakuna kitu, nikakosa na interest ya kuendelea kusoma. Mwamba alipotoa link ya kitabu sikutataka hata kuendelea kusoma.
Yan ww jamaa nuksi kinoma na kweny huu umekuja mlikua wap kuleta hicho kitabu siku zote mnasubil mtu aanzishe Uzi mdandie kutafuta umaarufu
 
Hayo ni maoni yangu kwamba ni chai, naamini sijavunja sheria za JF wala za nchi kwa kutoa maoni hayo.

Pole kama nimekukwaza mkuu.
Umeambiwa tunahitaj maoni yako hapa acha utoto wako nenda jukwaa la katiba ukatoe maoni yako sio hapa
 
konda msafi ,wewe ni mtu mzima tayari, jaribu kupunguza utoto, naona siku hizi umejivika cheo cha utambuzi whether story fulani ni kweli au sio kweli ,wewe ndio umekua hakimu

By the way story yako ulishaileta, imesomwa ikaisha, kaa pembeni, tulisoma story yako mpaka mwisho, hata ilipo onesha kuwa na makando kando, wengine sisi tunataka burudani.
Halafu hata kama ametunga lakini inatufurahisha tulio wengi, wewe ni nani hadi uje uanze kutoa shambo.

Kuna watu humu wameshaleta visa vya kweli ,story kali za kusisimua, kuliko hata hako ka story kako.Wakina Analyse,kigayoko, yule alieandika how I I met my wife, na nyingine nyingi za kutafuta utajiri kwa njia za kishirikina.

Lakini huwezi wakuta waki tangatanga kwenye story za watu kuziharibu, wewe sio mtanzania wa kwanza au wa mwisho kufika south,watu bado wanaendelea kwenda.

Unaudhi sana asee, kaa kwa kutulia, acha tupate buruani hayo mengine ya story ni kweli au sio kweli tumuachie mtoa mada,.au roho kama inakuuma jaribu kuomba kazi ya umoderator uwe unazifuta juu kwa juu.
Kwel mkuu huyu jamaa kawa hovyo sana yani akiona tu neno south Africa basi anasimamisha masikio na kutoa macho nilisoma comment kama 60 sijaona comment yake Mara paa huyu hapa sijui anajikuta ndio nan ndan ya south mtu mwenyew umeenda kwa ndege na kurud kwa ndege lakn unajidai unaijua kila boda
 
Kote alienda vizuri hapo kwenye ajari ndo kaharibu, na pale kwenye Gari imeharibika eti kulikuwa na gazeti lenye habari na Wale wenye lori wakawatambua kwamba wanatafutwa then wakawabeba hadi Lusaka, Hakuna mwenye akili timamu ata risk kiwango hicho cha kubeba wauaji,
Gari imeharibika porini ...gazeti wamelinunua sa ngapi....madereva wengi kutoa hela kununua gazeti sidhani labda magazeri ta Sports
 
Back
Top Bottom