Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

Duh mzee punguza kuchochea,tatizo unachochea kama baiskeli kwenye tambarare,kwanini uwe unapasuapasua condom? Tumia condom nzuri kama rough rider na za aina kama hiyo ingawa kwa picha nnayoipata kwako zinaweza kuwa kama 'vipedo' ukizivaa,sio mbaya 7bu huyo ni mkeo. Punguza kuchochea mkuu,nadhan kondom ni njia nzuri ya kupanga uzazi kaka
 
Vizuizi vya Ghafla (Emergency Contraception)
Hii hutumika wakati mwanamke amefanya mapenzi kiholela kupitia kwa uke (vaginal sex) ili kumzuia kupata mimba. Inaweza kutumika pia kama njia za kizuizi zilizokuwa zimetumika hazikufaulu. Hufaa sana kama itachukuliwa kabla ya masaa 72 kutoka wakati wa mapenzi. Huhusisha kunywa dawa mbili za ‘Hormone' zikiachana kwa masaa 12. Hizi dawa vidonge hufaa kwa asilimia 75-89 kuzuia mimba.

Njia nyingine ya kizuizi cha ghafla ni kuwekwa ‘copper T IUD' kwenye tumbo la uzazi kabla siku 7 hazijaisha kutoka wakati wa mapenzi (ngono). Hii njia hufaa asilimia 99.9 kuzuia mimba na inaweza kutolewa wakati wa muezi huo mwingine. Kama tayari ushaishika mimba njia hizi hazitakusaidia. Hii njia za ghafia hazifai kutumika kama desturi.

Povu na utando,

Povu na utando au vidonge vilivyo na kemikali ya kuua mbegu (manii) – spermicide huwekwe ndani ya uke si zaidi ya saa moja kabla ya kufanya mapenzi. Huwa zinafanya kazi kwa kuua manii. Huachwa papo hapo kwa masaa 6-8 baada ya kufanya mapenzi. Kemikali hizi (spermicides) zingine huwa na Nonoxynol-9 ambayo kukulinda kutokana na kisonono na Chlamydia. Nonoxynol-9 hatakulinda kutokana na ukimwi. Kemikali hizi (spermicides) hufaa kwa asilimia 74 kukulinda kushia mimba.

IUD (Intrauterine Device)

Hiki ni kifaa cha plastiki au shaba kilicho na umbo la ‘T' na huwekwa kwenye mji wa mimba/tumbo la uzazi (uterus) ili kuzuia manii kulifikia yai. Hukaa kwa muda wa miezi kadha hadi miaka 10. Hiki kufaa husaidia asilimia 98-99 kuzuia mimba. Kinapowekwa, huanza kazi yake papo hapo. Unaweza kupata kiharusi siku chache baada ya kuwekwa IUD. Kati ya mwezi wa 3 na 6 unaweza kutoa damu kidogo juu zaidi ya damu ya hedhi. Pia mwezi wako/wakati wako wa hedhi utakosa kubainika. Wanawake wengine hutoa damu kwa wingi.

Njia ya kutumia kizuizi

Kondomu za Wanawake/kike
Huu ni mrija mtegevu wa plastiki huvaliwao kwenye uke. Pande iliyafungwa husaliwa ndani karibu na ‘Cervix' na upande uliowazi huvaliwa tu nje ya uke. Hii njia ya kutumia kizuizi hiki huzuia manii kufikia yai. Hii kondomu yaweza kuvaliwa aghalabu masaa 24 kabla ya kufanya mapenzi na hufaa kwa asilimia 79-95 katika uzuizi wa mimba. Kondomu hizi hupatikana kwenye maduka ya dawa. Pia hospitali za mikoa na kliniki hupatiana kondomu hizi bure.

Diaphragm/Cervical Cap (Kiwambo-diaphragm)
Hii njia huzuia manii kulifikia yai. Kiwambo hiki huwa na umbo kama kikombe nayo ‘Cerival cap' huwa na umbo kama kastabini (thimble). Hizi hufunikia ‘cervix' (mwanzo wa tumbo la uzazi) ili manii yasiingie kwenye tumbo la uzazi (womb). Zinafaa kuvaliwa/kuwekwa ndani ya uke kabla ya kufanya mapenzi. Kiwambo hiki hufaa kwa asilimia 80-94 kwa kuzuia mimba. Nayo ‘cervical cap' hufaa asilimia 80-91 kuzuia mimba kwa wanawake ambao hawajawahi pata mtoto, na hufaa asilimia 60-80 kwa wanawake ambao keshajifungua. Unafaa kumwona daktari au mtaalamu wa mambo yahusuyo uke ili
akuweke kiwambo au ‘cap'.


Njia za Hormoni

Vidonge Vya Kumeza (Pill)
Kidonge hufaa kunywewa kila siku na huwa na ‘hormones' mili ambazo ni ‘ostrogen' na progestin ambazo huzuia kifuko cha mayai kwenye uke kutoa mayai. Inapotumika ipayasavyo hufaa kwa asilimia 95-99.9 kuzuia mimba. Kama una miaka zaidi ya 35 na huwa unavuta sigara* au umewahi kuwa na historia ya kuvilia damu au kansa ya maziwa (matiti) au ‘endometrial' daktari wake anaweza kukushauri usitumie kidonge hiki.

Vidonge hivi huongezea hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo, kukimbia kwa damu, kuvilia damu na kufungamana kwa mishipa ya damu. Kuna aina mbali mbali ya vidonge hivi na huwa na vipimo tofauti vya ‘oestrogen' na ‘progestin'. Unafaa kualiza shauri kutoka kwa daktari wako au kutoka kwa hospitali/kliniki kabla hujaanza kunywa vidonge hivi. Vidonge hivi hupatianwa bure katika hospitali za mikoa na kliniki nyinginezo.

The Mini Pill
Hiki kidonge (vidonge) hufaa kunywewa kila siku na huwa na ‘Hormone' moja (progestin) ipunguzayo na kuafanya ute wa ngozi ya ndani ya uke (cervix) kuwa mzito/mnene ili kuzuia manii kulifikia yai. Kidonge hiki pia huzuia yai uliloungana mbegu kukomaa (kujiimarisha) kwenye uke. Hiki kidonge hufaa sana kwa wanawake ambao hawawezi kunywa ‘oestrogen' au kwa wale wana hatari ya kuvilia damu. Akina mama wanaonyonyesha wanaweza kukitumia kidonge hiki kwa sababu hakiadhiri utuaji wa maziwa. Kitumiwapo ipasavyo, hufaa kwa asilimia 95-99.9% kwa uzuizi wa mimba.

Sindano – Depo-Provera
Depo-Provera ® huzuia utoaji wa mayai na hufanya ute wa ngozi ya ndani ya uke (cervix) kuwa mzito hivyo kuzia manii kupenyeza kwenye tumbo.* Pia hufanya tabaka (lining) la tumbo kunenepa hivyo kuwa vigumu kwa yai lililoungana na mbegu kujishikilia. Wanawake hsindano hii kwenye makalio (******) au mkono baada ya kila miezi mitatu. Hufaa kwa asilimia 99.7 kwa kuzuia mimba. Sindano hii haistahili kwa wanawake walio chini ya umri wa miaka 21 ila tu kama wameshawahi kujifungua au hawawezi kutumia njia nyingine ya ‘Harmone' kwa sababu ya matatizo ya kiafya. Daktari wake/mtaalamu atakudunga sindano hii.



Njia za kitabia

Hii huwa mwanamume kuondoa uume wake kutoka ndani ya uke kabla ya kutoa manii ili kuzuia mbegu kufikia yai. Hii njia huhitaji uzuifu mwingi sana (kutokana na msongo) upande wa mwanamume. Hata kwa kutumia njia hii unaweza pata

mimba KABLA mwanamume hajatoa uume wake. Kabla hajatoa manii mwanamume anaweza kutoa manii mengine kabla ya kufika kileleni (pre-ejaculation) nah ii inaweza kusababisha mimba. Hivyo basi hii njia haifai sana kwa kuzuia mimba. Pia,

haitakulinda kutokana na maradhi ya zinaa. Kujinyima/kujifunga kutoka kufanya mapenzi wakati wa mwezi/hedhi au ‘Fertility Awareness' ni njia nyingine, na inayofaa zaidi ya kuzuia uzazi kitabia.

Njia za kupanga uzazi milele

Kufanywa Tasa au Gumba kwa kutumia Upasuaji
Hizi njia za upasuaji huazimiwa kwa watu walio maliza uundaji wa familia au hawataki watoto.

Kufungwa mirija (tubal ligation/tying tubes') hufunga/hukata mirija unaobeba mayai ndiposa kuyazuia mayai kuingia tumboni la uzazi ambako yanaweza ungana na mbegu (manii).

‘Vasetomy' (kufungwa kwa mrija ubebao manii kutoka wakati ufanyapo mapenzi.

Njia hizi haziadhiri uwezo wenu wa kufanya mapenzi. Njia hizi haziadhiri uwezo wenu wa kufanya mapenzi. Njia hizi haziadhiri uwezo wenu wa kufanya mapenzi. Kufungwa mirija hufaa kwa asilimia 95-99.5 % kwa kuzuia mimba. Hata hivyo hazifai katika kuzuia maradhi ya zinaa, kwa hivyo kama wewe si wa mke mmoja utafaa kutumia kondomu.

Family Planning Association of Kenya wana habari kuhusu mambo hayo kwa wanawake na wanaume. Unaweza kuwapigia simu kwa maelezo zaidi au uulize kwenye hospitali au kliniki iliyokaribu nawe. Wanaume wanaweza kufanyiwa upasuaji na warudi makwao lakini kwa wanawake itawabidi walazwe.



MKUU CHAGUA NJIA UNAYOIONA NI NZURI KWAKO KATI YA HIZI NJIA ZA KUZUIA MIMBA.
 
Aaaaa Tizo bana kwani mnatumia brand gani??

natumia salama za sh 200.zile za ulaya ni ghali sana...siwezi nunua condom elfu 2 wakati sina sukar ndani kwangu
 
Vizuizi vya Ghafla (Emergency Contraception)
Hii hutumika wakati mwanamke amefanya mapenzi kiholela kupitia kwa uke (vaginal sex) ili kumzuia kupata mimba. Inaweza kutumika pia kama njia za kizuizi zilizokuwa zimetumika hazikufaulu. Hufaa sana kama itachukuliwa kabla ya masaa 72 kutoka wakati wa mapenzi. Huhusisha kunywa dawa mbili za ‘Hormone’ zikiachana kwa masaa 12. Hizi dawa vidonge hufaa kwa asil asante mzizi mkavv.njia zote nimepa wife azipitie.kisha tutajadili kwa pamoja.
 
roho inauma sana ukifanya mapenz na condom....nani amfaidi mkeo kama sio wewe mumewe?
 
wadau na ni mda gani unafaa kufanya mapenzi na mkeo tangu kujifungua?
 
Mkuu mimi nilienda na my wife wamemshauri wamwekee kachuma kwenye uzazi wanasema hii ni nzuri zaidi.
 
1.Hakikisha mke wako anakunywa glass moja ya maji baridi baada ya kusex not only this stage 2. Munaposex ukieleke kuejaculate chomoa na uejaculate nje ya uke wa mkeo 3.tumia kondomu zenye ubora wa hali ya juu 4. Hakikisha unajua ratiba ya mkewako ya heat days 7day siku hizi hakikisha unakuwa bize msikutane kimwili 5. Dawa ningekushari ukihitaji niambie
hapo kwenye red unamaanisha nini?
 
Usalama mnaouzungumzia cjaujua usalama wa kuepuka mimba au usalama wa kiafya? Kuwen wawaz
 
me naonjia bora n kondom lakm some of us huwa 2naday kuwa haina ladha so dat why wanaendelea kuget pregnant
 
Njia salama kabisa ni kalenda

kweli tena hizi nyingine unaambiwa hazina madhara kwa lengo la kufanikisha adhma yao ya kuweka ratio inayotakiwa lakini kwa wale madaktari bingwa hawatumii na wengine ukienda vizuri wanakushauri tumia kalenda.mimi niliwahi kutumia sindano kwa upande wangu ilikuwa na side effect situmii tena njia nyingine zaidi ya kalenda
 
Ukiwa na Mtoto Mmoja sio mara zote ni kufuata Uzazi wa Mpango..kama hivyo ndivyo, wale ambao hawajazaa kabisa watastahili kuingia katika kundi la wanaofuta uzazi huo wa mpango kwa kuamua kuto zaa kabisa...

Pengine wataalamu wa Uzazi wanaweza kuhoji,ni kigezo gani kilitumika kwa kumwingiza Mwana muziki wa injili kama Flora Mbasha mwenye mtoto mmoja kwenye Tangazo la kuhamasisha Uzazi wa Mpango la Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii??

Yawezekana kabisa familia ikawa na mtoto mmoja kutokana na tatizo la uzazi na sio mipango ya uzazi...hili linatakiwa liangaliwe kwa makini..

Tunafanya uzazi wa Mpango ili iweje? wengine wanasema ni kupunguza mzigo wa familia kwa wazazi..Hivi inakuwaje Mzee Yusufu nae anaingia uhamashishaji wa uzazi wa Mpango akiwa na wake watatu na watoto wawili wawili kila mke??. Huyu anatofautianaje na mwanaume mwenye Mke mmoja lakini akazaa watoto saba waliopishana mwaka mmoja??.
 
Ukiwa na Mtoto Mmoja sio mara zote ni kufuata Uzazi wa Mpango..kama hivyo ndivyo, wale ambao hawajazaa kabisa watastahili kuingia katika kundi la wanaofuta uzazi huo wa mpango kwa kuamua kuto zaa kabisa...

Pengine wataalamu wa Uzazi wanaweza kuhoji,ni kigezo gani kilitumika kwa kumwingiza Mwana muziki wa injili kama Flora Mbasha mwanye mtoto mmoja kwenye Tangazo la kuhamasisha Uzazi wa Mpango la Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii??

Yawezekana familia inaweze kuzaa mtoto mmoja tu kutokana na tatizo la uzazi na sio mipango ya uzazi...hili linatakiwa liangaliwe kwa makini..

You will never believe, mke wangu aliniuliza swali hilo hilo kuwa: Kweli huyu wanamziki wameamua kuwa na mtoto mmoja tu au kuna shida kwenye uzazi. tusidanganyane, kwa Africa bado kuwa na maamuzi ya kuzaa mtoto mmoja na kumpa interval ya namna hiyo kama hakuna tatizo kwenye uzazi wa wahusika. I stand to be corrected!!!!
 
Ukiwa na Mtoto Mmoja sio mara zote ni kufuata Uzazi wa Mpango..kama hivyo ndivyo, wale ambao hawajazaa kabisa watastahili kuingia katika kundi la wanaofuta uzazi huo wa mpango kwa kuamua kuto zaa kabisa...

Pengine wataalamu wa Uzazi wanaweza kuhoji,ni kigezo gani kilitumika kwa kumwingiza Mwana muziki wa injili kama Flora Mbasha mwenye mtoto mmoja kwenye Tangazo la kuhamasisha Uzazi wa Mpango la Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii??

Yawezekana kabisa familia ikawa na mtoto mmoja kutokana na tatizo la uzazi na sio mipango ya uzazi...hili linatakiwa liangaliwe kwa makini..

Tunafanya uzazi wa Mpango ili iweje? wengine wanasema ni kupunguza mzigo wa familia kwa wazazi..Hivi inakuwaje Mzee Yusufu nae anaingia uhamashishaji wa uzazi wa Mpango akiwa na wake watatu na watoto wawili wawili kila mke??. Huyu anatofautianaje na mwanaume mwenye Mke mmoja lakini akazaa watoto saba waliopishana mwaka mmoja??.

Mimi pia lile tangazo linanichefua sana. kwani kuwa na mtoto mmoja tena anamiaka kumi kisha unajisifia niuzazi wa mpango hiyo siyo kabisa. yaani wametuingiza chaka.
Kwa kifupi naona anaumwa ugonjwa ufuatao. ugojwa wenyewe unatokea pale mume na mke wanapokua na group za damu tofauti ,hizi group za damu zinaitwa Rh factor.
Mtoto wakwanza atazaliwa salama ila wengine watafia tumboni kwani kutakua na reaction kati ya mama na mtoto aliye tumboni. more details soma hii.


A woman is at risk when she has a negative Rh factor and her partner has a positive Rh factor. This combination can produce a child who is Rh positive. While the mother's and baby's blood systems are separate there are times when the blood from the baby can enter into the mother's system. This can cause the mother to create antibodies against the Rh factor, thus treating an Rh positive baby like an intruder in her body. If this happens the mother is said to be sensitized.

A sensitized mother's body will make antibodies. These antibodies will then attack an Rh positive baby's blood, causing it to breaking down the red blood cells of the baby and anemia will develop. In severe cases this hemolytic disease can cause illness, brain damage and even death.
 
jipange upya umekurupuka kwe2 tupo wanne tumepishana ratio miaka 3 .shangaz yangu anamtoto 1 nahc walpta matatzo katika ndoa yao.bro wangu ana watoto wawil ke 7yr na me 2yr kasema kashaweka password

Kiongozi upo makini. Kule China, kuongezeka kwa watu kulipelekea kuanza kwa "Family Planning" ambapo raia walilalimishwa kuzaa mtoto mmoja au bahati mbaya ikitokea wawili. Lakini nia ilikuwa kupunguza idadi ya watu ili iendane na mazingira mengine ya kijamii na kiuchumi ya nchi hiyo...Ukiwa na watoto kumi na wake kumi ambapo kila mmoja amezaa mtoto mmoja, Je, unaweza kujigamba kuwa unatekeleza uzazi wa Mpango?? Je, hesabu inafanyika kwa mke mmoja tu au wote uliowaoa?? Mzee Yusuf kwa kesi hii kama ana wake watatu na kila mmoja akiwa na mtoto mmoja bado hawezi kukwepa tatizo la malezi ya familia kubwa (wake na watoto pamoja na ndugu wanaomzunguka). Mtu kama huyu hawezi kujivuna kuwa anafuata uzazi wa mpango ukilinganisha na mimi mwenye watoto watano kwa mfano.

Wengine walizaa mmoja sio kwa kupenda bali ni tatizo la kimaisha...
 
Kiongozi upo makini. Kule China, kuongezeka kwa watu kulipelekea kuanza kwa "Family Planning" ambapo raia walilalimishwa kuzaa mtoto mmoja au bahati mbaya ikitokea wawili. Lakini nia ilikuwa kupunguza idadi ya watu ili iendane na mazingira mengine ya kijamii na kiuchumi ya nchi hiyo...Ukiwa na watoto kumi na wake kumi ambapo kila mmoja amezaa mtoto mmoja, Je, unaweza kujigamba kuwa unatekeleza uzazi wa Mpango?? Je, hesabu inafanyika kwa mke mmoja tu au wote uliowaoa?? Mzee Yusuf kwa kesi hii kama ana wake watatu na kila mmoja akiwa na mtoto mmoja bado hawezi kukwepa tatizo la malezi ya familia kubwa (wake na watoto pamoja na ndugu wanaomzunguka). Mtu kama huyu hawezi kujivuna kuwa anafuata uzazi wa mpango ukilinganisha na mimi mwenye watoto watano kwa mfano.

Wengine walizaa mmoja sio kwa kupenda bali ni tatizo la kimaisha...

Ye hawezi ila wake zake wanaweza ndio maana wakamshirikisha mmoja.
 
Mimi naomba nitofautiane na ninyi wote mliotuma maoni yenu. Kwanza kabisa hakunaga kitu kinaitwa kupanga uzazi ila tunaita nafasi kaati ya mtoto mmoja hadi mwingine(child spacing). kwanini nawakatalia

ANGALIA HAYA-- mama akianza kuzaa na miaka 25 halafu akatumia njia za kupanga uzazi(isiyo ya kufunga), njia yenye kuruhusu kuendelea kutumika kwa dawa zake mwilini ni implanon. Implanon ni aina ya dawa ambayo hufanyiwa implantation ndani ya ngozi ya mama kwa sehem ya juu ya mkon ili kumkinga na mimba. Njia hii inaweza kumkinga na mimba hadi 5 yrs. yaani implant mojaeffect ikaenda hadi 5 yrs.

sasa mama huyu kama atazaa na 25 yrs na ukiassume ataweka impalant akiwa 26 basi atazaa tena akiwa na miaka 36 hapo napo akiweka atazaa na miaka 42, hapo napo akiweka atazaa na miaka 48. hivyo basi kwa child spacing hii huyu mama atakuwa na watoto 4.

Pia ikumbukwe kuwa mama huyu anayepanga hivi, mumewe ana mahawara, let say anaye hata mmoja tu huyu naye anaweza kumzalisha mtoto so baba huyu atakuwa na watano ilihali mama ana4. hapo hapo kma mama amepata bahati ya kupata watoto wa jinsia moja baba atachakachua ili apate wa ajinsia nyingine so nako huku anaweza kuzaa tena.sasa kwa haya hapa hakuna mpango wa uzazi wala uzazi wa mpango.

Nionavyo mimi ni busara kabisa baba na mama wakakubaliana kuzaa watoto kiasi fulan kisha wote kwa pamoja wakaenda kufunga uzazi ili waendelee kula raha huku wanalea watoto. kinyume na hapo bado maisha yanamfanya baba awe na watoto kwa uchache wake 7 iwapo mama atatumia njia hizi za kupanga uzazi. niko tayari kurekebishwa wakuu
 
kwa kweli wizara ya afya haikujua watu wa kuchagua kubeba tangazo lao.

Anyway, ya kuzaa mie napenda watoto wengi hata 12 basi tu afya za kizazi hiki migogoro.
 
Wale ambao hawajazaa hawawezi kuwa kwenye kundi la uzazi wa mpango kwa sababu ili uingie kwenye kupimwa kama umepanga uzazi ni lazima uwe umezaa ili wajue kama huo uzazi umeupanga ama la.Sasa kama hujazaa utapimwaje?Kuhusu hao wanaohamasisha kwenye matangazo inaelekea wamechemsha.Lakini pia kwa mtazamo wangu,uzazi wa mpango ni mbinu ya New World Order ya kumantain population ili waitawale dunia vyema during that NWO na wala sio sababu wanazoleta wao!
 
Back
Top Bottom