Kiongozi upo makini. Kule China, kuongezeka kwa watu kulipelekea kuanza kwa "Family Planning" ambapo raia walilalimishwa kuzaa mtoto mmoja au bahati mbaya ikitokea wawili. Lakini nia ilikuwa kupunguza idadi ya watu ili iendane na mazingira mengine ya kijamii na kiuchumi ya nchi hiyo...Ukiwa na watoto kumi na wake kumi ambapo kila mmoja amezaa mtoto mmoja, Je, unaweza kujigamba kuwa unatekeleza uzazi wa Mpango?? Je, hesabu inafanyika kwa mke mmoja tu au wote uliowaoa?? Mzee Yusuf kwa kesi hii kama ana wake watatu na kila mmoja akiwa na mtoto mmoja bado hawezi kukwepa tatizo la malezi ya familia kubwa (wake na watoto pamoja na ndugu wanaomzunguka). Mtu kama huyu hawezi kujivuna kuwa anafuata uzazi wa mpango ukilinganisha na mimi mwenye watoto watano kwa mfano.
Wengine walizaa mmoja sio kwa kupenda bali ni tatizo la kimaisha...