Wadau,
Kila mara tunasikia Uzazi wa Mpango, na kwamba ni bora na salama kwa afya ya mama na mtoto na kwa manufaa ya Familia.
Baadhi ya manufaa hayo ni;
1. Inasaidia mama kurudi hali yake ki afya ya awali.
2. Inasaidia kulea watoto kwa urahisi na kuwapa maisha bora.
3. Inasaidia mzazi kufanya shughuli za kimaendeleo, si za nyumbani tu.
Sasa basi, tokana na jamii iliyokuzunguka au wewe mwenyewe, unadhani kuna faida nyingine zaidi ya hizo hapo juu zilizotajwa?
Tafadhali naomba shiriki utujuze kile unachoelewa kwa manufaa ya ku share yale ambayo kila mmoja anaelewa.
Wasalaam!