Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

TUMIA CONDOM, HIZO NYINGINE NI HATARI KWA MWANAMKE ANAWEZA ASISHIKE MIMBA MILELE ZINAZOOFISHA OVARIES ZA MWANAMKE ESPECIALLY SINDANO NA VIDONGE
 
Takwimu zinaonesha watumishi wengi wa kada ya afya na familia zao wanatumia Kitanzi, kwa nini kitanzi? Mara nyingi madhara makubwa yanayotokana na dawa za uzazi wa mpango huwa yamesababishwa na muingiliano wa hormones ambazo zinatokana na dawa za uzazi wa mpango zilizomo kwenye sindano kipandikizi au vidonge. Kitanzi hakina hormone hivyo husababisha madhara madogo madogo ukilinganisha na njia hizo nyingine.
Naomba kufahamu mbali na njia za kawaida za kupanga uzazi mfano condom na kalenda no njia ipi ambayo ni salama zaidi kati ya vidonge,Sindano,kitanzi,nanjiti?
 
Salama ni condom na calendar, kama bado unazaa usijaribu sindano. Kijiti ni nziri kuliko hizo zingine tajwa
 
Naomba kufahamu mbali na njia za kawaida za kupanga uzazi mfano condom na kalenda no njia ipi ambayo ni salama zaidi kati ya vidonge,Sindano,kitanzi,nanjiti?
kwanza ww unataka kutumia njia za uzazi wa mpango kwa malengo gani na pia una mume au laah na kama unataka kutumia hizi njia kwa kuchepuka au laah kwan unapo sema atumie kitanzi ndio kitanzi ni kuzur kwa hakina homoni na itakuwa unaingia kwenye siku zako kama kawaid ila sasa unatakiwa kutulia sio kila mda unachokoa ndani huko pia utulie na mume mmoja kwan ukiwa hutulii hiko kitanzi kitasogea so ukitaka ushaur au ufafanuzi wa njia nyingn useme
 
Salama ni condom na calendar, kama bado unazaa usijaribu sindano. Kijiti ni nziri kuliko hizo zingine tajwa
Ni kweli kwamba condom na calendar ni salama lakini ukiangalia failure rate ya hizo njia mbili ni kubwa sana. Kijiti na kitanzi kitanzi ni salama zaidi ya kijiti kwa sababu kijiti kinafanya slow release ya hormones ambayo ndio kidonge na sindano inachofanya tofauti labda inaweza kuwa aina ya hormone iliyopo kwenye kijiti au sindano au kidonge lakini mode of action zinafanana tofauti ni muda wa kukaa mwilini tu. Best of the best ni abstinence au masturbation[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
1483793961059.png
Njia nzuri isiyo na chemical ni kalenda tuu
 
Eti papai linazuia mimba tena kwa kulila tu kama tunda.

 
DAWA YA ASILI YA UZAZI WA MPANGO

Kila mtu angependa kuwa na watoto ingawa kila mzazi hupenda apate mtoto kwa wakati muafaka au muda maalumu atakapokuwa tayari kwa ajili ya mtoto. Wakati mtu anapanga kuwa na mtoto ni wakati mzuri sana katika maisha na unatakiwa kuwa ni wakati uliokubalika kwa wazazi wote wawili kuamua kuwa ni kipindi cha kuwa na kulea mtoto

Ili kuepuka mimba zisizotarajiwa wanawake wengi huamua kutumia vidonge vya kuzuia ujauzito (Vidonge vya uzazi wa mpango/majira). Vidonge hivi huwa na madhara mengine mabaya hapo baadaye vikitumika kwa kipindi kirefu.

Zipo dawa za asili kadhaa nyingi zaidi ya 20 ambazo zinaweza kutumika kama njia za kuzuia ujauzito usiotarajiwa bila kukuachia madhara yoyote mabaya. Dawa hizi ama zinazuia urutubishaji wa yai moja kwa moja au huweza kukusababishia kuona siku zako na hivyo kuondoa uwezekano wa kuwa mjamzito.

Nimekuandalia dawa asili nne kwa ajili hii ambazo nimeona zinapatikana kirahisi mazingira ya hapa kwetu Tanzania na ufurahie maisha yako ya ndoa bila kuwa na wasiwasi.

Mhimu: Kama itatokea umepima na kugundulika ni mjamzito basi usizitumie dawa hizi kwani inaweza kupelekea kuharibika kwa huo ujauzito (miscarriage).

Dawa ya asili ya uzazi wa mpango

1. PAPAI

Papai ni dawa bora kabisa ya uzazi wa mpango. Unaweza kula papai mara 2 kwa siku siku 3 hadi 4 baada ya kushiriki tendo la ndoa bila kinga. Litakusaidia kuepuka kutungisha ujauzito. Mbegu za Papai pia ni dawa nzuri ya uzazi wa mpango kwa upande wa wanaume. Zinachofanya mbegu za papai ni kupunguza idadi ya uwingi wa mbegu za mwanaume (sperm count) na ukihitaji kuzaa unaacha tu kuzitumia na hali yako itarudi kama kawaida.

Kula mbegu za papai kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku. Unaweza kuanza zoezi hili wiki 3 kabla hujaamua rasmi kama ndiyo dawa yako ya uzazi wa mpango.

Watu wa bara la Asia wamekuwa wakitumia mbinu hii tangu miaka mingi iliyopita. Dawa hii haina madhara yoyote.

2. TANGAWIZI

Tangawizi huhamasisha kutokea kwa siku zako. Kunywa vikombe viwili vya chai ya tangawizi kila siku ili kuzuia ujauzito. Tumia tangawizi mbichi na siyo ya unga kwa matokeo mazuri zaidi.

3. KOTIMIRI (Parsley):

Kotimiri inapatikana kirahisi Dar Es Salaam na Zanzibar na ni kiungo mhimu kwenye mahoteli mengi ya kitalii. Kunywa kikombe kimoja (robo lita/ml250) asubuhi na jioni cha chai iliyoandaliwa ukitumia kotimiri mbichi kila siku ili kuzuia ujauzito usiotarajiwa. Hakuna madhara yoyote mabaya ya matumizi ya dawa hii.

4. VITAMINI C

Vitamini C ikitumika katika hali yake ya uasili kabisa inaweza kutumika kama dawa ya uzazi wa mpango. Kwenye vitamini C kuna ‘ascorbic acid’ ambayo huzuia homoni inayouandaa mji wa uzazi (‘progesterone hormone’) kushindwa kufanya kazi zake vizuri na hivyo mimba kukosa mahali pa kukaa baada ya yai kurutubishwa.

Meza viponge vya vitamini C mg 1500 mara mbili kwa siku mbili mpaka tatu baada ushiriki tendo la ndoa bila kinga. Vitamin C ni nzuri pia kwa ngozi yako. Dawa ya asili yenye vitamini C kwa wingi ni unga wa majani ya mlonge. Unga wa majani ya mlonge una vitamini C mara 7 zaidi ya ile ipatikanayo katika machungwa.

Mhimu:

1) Usitumie kiasi kingi sana cha vitamini C kwani inaweza kupelekea mwili wako kutokuwa sawa au unaweza usijisikie vizuri katika mwili wako.

2) Usitumie vitamini C kama unatumia dawa za kuzuia damu kuganda (anti-coagulant medications).

3) Usitumie vitamini C kama una tatizo la sickle cell (sikoseli).
 
hii ya vitamin C mbona kama sio ya asili na kwa mujibu wa maelezo yako umesema ni za asili, ingekua poa kama ukaitoa kama hutojali lakini!!!!!!
 
ndugu zangu naomba msaada,je nitumie dawa gani au njia gani za uzazi wa mpango ambazo hazina madhara maana nasikia most of them zinaleta kansa
 
Mnaweza tumia uzazi wa mpango,like condom, au calendar, na calendar ni njia sahihi Sana kwani haina madhara
 
Mhe Gudboy naomba ushauri kuna mtu anatumia kitanzi cha miaka 12, anatatizo la kutokwa na majimaji mengine na ute mzito mara nyingine una rangi ya cream au kama kijani. Tumempeleka hospital wanasema ni kawaida haina madhara. Ni sawa
 
Maelezo poa kabisa haya, Ila mkuu kuna mambo kadha wa kadha umesahau kidogo na nmeelezea mimi Hapa embu pitia.
 
Ni chachu bandia ya projestini iliyotengenezwa katika maabara ambayo mwanamke hudungwa mg 150 kila baada ya miezi mitatu. Chachu hii bandia huitwa Depot - MetroxyProgesterone Acetate {DMPA}. Depo provera ambayo tumezoea kuita sindano ya Depo Provera ambayo hadi 1996 ilitumiwa na wanawake milioni 30 katika zaidi ya nchi 90 duniani, nyingi zikiwa nchi maskini, inaaminika kuzuia mimba kwa miezi mitatu. Dawa hii ilithibitishwa kwa matumizi huko Marekani mwaka 1992. Lakini mwezi Juni 1993 Idara ya Afya ya Kanada ilizuia matumizi ya dawa hiyo kwa maelezo kuwa sio salama kwa afya ya watumiaji. Ili kuepusha madhara kwa wanawake wa Ulaya, Shirika la Afya Duniani lilifanya majaribio ya dawa hii kwa wanawake wa nchi zinazoendelea, kama vile Kenya, Mexico, Thailand na New Zealand.


3. Utendaji wake
Kwa kadiri ya jarida la ‘‘Upjohn’’ Depo Provera depo provera huzuia utoaji chachu zinazohitajika kwa ajili ya kuivisha yai. Hali hiyo husababisha ngozi nyororo katika mji wa mimba kuwa laini na hivyo kushindwa kumpokea bindamu mpya. Vile vile inabadilisha ute na kuwa mzito na kuzuia mbegu kupenya kwa urahisi kuelekea tumbo la uzazi na mirija yake. Depo provera ni kiua mimba. Wanawake wengi wanaotumia depo provera hupata hedhi asilimia 43 baada ya miezi 12 na silimia 32 baada ya miezi 24. Takwimu hii inatusaidia kufahamu kuwa sio katika wanawake wote dawi hii hufanya kazi kwa kiwango kile kile.

4. Je depo provera ni salama ?
Huko Marekani Shirika la Chakula na Madawa lilikataa kuthibitisha matumizi ya dawa hiyo kwa miaka 20 tangu 1972 hadi 1992. Baadhi ya sababu ni :-

a) Baadhi ya watetezi wa dawa hii, ambao walilishinikiza Shirika la Chakula na Madawa la Marekani kuipitisha walikuwa wanajihusisha na masuala ya udhibiti wa idadi ya watu duniani.
Wakati wa majaribio kwa wanyama, ilionekana kusababisha uvimbe wa matiti kwa mbwa na saratani ya tumbo la uzazi kwa nyani.

b) Dawa yoyote inayoleta madhara kwa wanyama, kuwa hivyo pia kwa binadamu.

c) Dawa hii ilionekana kusababisha saratani ya mlango wa tumbo la kizazi kama ilivyoripotiwa na msemaji katika Taasisi ya Taifa ya Saratani huko Marekani.

d) Dawa hii ilishinikizwa kwa watu weusi (Negro) na Wahindi huko Marekani, na katika nchi zinazoendelea. Vile vile dawa hii inatolewa kwa watu wasio na elimu, wenye mtindio wa ubongo, na kutolewa kwa siri kwa makundi ya vijana. Utafiti uliofanyika kufuatia jambo hili, ulionyesha madhara makubwa kwa watumiaji hasa uvimbe katika matiti yao.



Ufafiti uliofanywa na Jarida la habari la « Upjohn » kwa miaka 11 huko Atlanta kwa watu weusi waliotumia dawa hiyo, ulionyesha kuwa ; baadhi ya wanawake walikufa, wengine walipata saratani, wengine dawa iliwajengea muelekeo wa kujiua kutokana na mgandamizo wa moyo .

Katika miaka ya 1990 baadhi ya nchi kama vile Canada na India zilizuia matumizi ya Depo provera, kutokana na madhara yaliyowapata wanawake.

Shirika la chakula na dawa la Marekani, lililazimisha kampuni ya Frizer kubandika tangazo lenye tahadhari kuwa inaleta madhara ya kutisha, kama vile, kupoteza madini kwenye mifupa. (Osteoporosis)

Madhara zaidi ya depo provera

Mabadiliko ya hedhi, kutoka damu nyingi na kwa muda mrefu (anemia), kutoka damu nzito, kutoka damu kidogo, kutotoka damu kabisa, damu kidogo, kutoka damu matone matone na kutoka damu bila mpangilio.
Kuongezeka uzito na uzito huo huongezeka kadiri ya muda wa matumizi na aina ya mtumiaji (kila 1 hadi 5 kila mwaka) .
1 Kupoteza uzito katika mifupa (osteoporosis)
2 Maumivu ya magoti
3 Kupungua uwezo wa kupokea sukari.
4 Wasichana wengi walio chini ya umri wa miaka 35 huwa na uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya matiti.
5 Mabaka mabaka
6 Saratani ya mlango wa kizazi
7 Kupasuka kwa mishipa ya damu kutokana na kuziba kwa mshipa mkubwa na kuganda damu / hewa.
8 Kuziba kwa mshipa mkubwa na kuganda damu/ hewa
9 Matatizo ya akili
10 Upofu wa macho
11 Kuzaa mtoto mwenye vidole zaidi ya kawaida au walioungana.
12 Kuwa na wasiwasi, kutotulia
13 Kujaa maji mwilini
14 Kichefuchefu
15 Ugonjwa wa manjano
16Kifafa cha mimba
17 Uvimbe katika uke
18 Kupooza
19 Tafiti nyingine zilizofanywa zimesema kuwa wanawake wanaotumia depo provera wana hatari ya kupata magonjwa ya zinaa kama vile Clamdiya, Gonorrohea, Herpes Virus mara tatu zaidi ya kawaida.
20) 50% ya wanaopata mimba, hali wakitumia Depo provera wana uwezekano wa kuzaa watoto njiti.
21) 90% , kama wanaacha Depo provera wiki 4, baadaye wakipata mimba wanazaa njiti.
22) 80% ya watoto wanaozaliwa ambao walitungwa mimba mama yao akitumia au mara tu baada ya kuacha

23. Kuchelewa kupata mimba au kutopata mimba kabisa.

kushare ni muhimu kwani jamii yetu haijui athari za uzazi wa mpango kwa kutumia njia za kisasa, please please okoa jamii

USISAHAU KUSHARE NA KULIKE PAGE YETU YA Mdadisi MAMBO kwa habari za kijamii na kimaisha bila kusahau mapenzi na mahusiano
 
Kwa nchi yetu utekelezaji wa bandiko hili na ushauri itachukua miaka kumi au zaidi ndiyo itapigwa marufuku
 
Upi uzazi wa mpango uliosalama wadau!
Kutokana na ugumu wa maisha! Nilimshauri mwanamke wangu atumie uzazi wa mpango ili angalau asizae mapema.

Lakini kila uzazi wa mpango anaojaribu kutumia naona unamletea majanga tu.
Kwanza alianza Kwa kutumia sindano! Sindano ikawa inamfanya "K" inajaa Maji yaani ukifanya naye mimaji mtupu;

Tukabadili angalau atumie kijiti " pandikizi" lakini nacho kilisababisha apatwe na irregular period! Yaan period haieleweki,

Ikabidi tujaribu kutumia vidonge! Sasa vidonge ndo vimemkata network ya hisia hana kabisaaaa! Yaani hana hamu kabisa! Sasa tufanyeje?

Tumejaribu kumwona daktari akasema njia zote ni salama hazina matatizo!

Swali!
Wakwenu huwa wanatumia njia gani? Naombeni ufafanuzi tafadhali!
 
Kwani lazima atumie uzazi wa mpango. Nyie hamuwezi kucontro, usimuumize mtoto wa watu
 
Back
Top Bottom