Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

Tunashukuru kwa ujumbe, watumiaji watakua wamekuelewa ila kwa hakika uzazi wa mpango ulitakiwa ufanywe na wanaume na si wanawake maana uwezo wa mwanamke kubeba mimba kwa mwaka ni Mara 1 yaani miezi 9 lakini mwanaume anauwezo wa kizalisha wanawake 100 kwa mwaka huo huo mmoja, hebu wanaume mtupunguzie masahibu haya wanawake

Wazo lako ni zuri lakini haya mambo yanafaa kushirikiana na kuelewana hivyo hakuna tatizo wanaume nasi huwa tunashiriki kikamilifu japo kuna baadhi (Wajinga) hawapendi kusikia hii kitu.
 
Kama atakuwa anakula Dagaa, Maharage, Mnafu na Mbilimbi anaweza kuanza kuona ' Hedhi ' yake baada ya miezi 9 mpaka 12

ILA

Kama atakuwa anakula Kuku, Nyama, Chips, Mayai, Maziwa, Makange, Samaki na Tambi anaweza akaanza kuona ' Hedhi ' yake baada ya miezi 2 mpaka 3.

je uwezekano wa kupata mimba hapo ni baada ya mda gani??

je anaweza kupata mimba kabla hata hajaziona siku zake kwa mara ya kwanza??
 
Kikawaida wanasema dawa inafanya kazi miezi mitatu,baada ya hapo tunategemea iwe imekwisha mwilini..

Ila kurudi ktk hali ya kawaida kwa maana ya kuanza kuona hedhi na pengine kushika mimba wakati mwingine inaweza kwenda zaidi ya hiyo miezi mitatu..binafsi nimeona baadhi ya akinamama waliokaa mwaka mzima kabla ya kurudi ktk hali ya kawaida..na wote baada ya hapo waliendelea kuzaa.

Kwa kuwa hii dawa inacheza na mfumo wa homoni za mama,kurudi ktk hali ya kawaida inatofautiana kutoka mama mmoja na mwingine..kwa hiyo hata hiyo miezi mitatu wanayosema ni kwa simple majority, ila kuna minority ambao wanazidisha huo muda.
 
je uwezekano wa kupata mimba hapo ni baada ya mda gani??

je anaweza kupata mimba kabla hata hajaziona siku zake kwa mara ya kwanza??

Kuhusu kupata mimba baada ya muda gani,nimejibu hapo juu..

Na anaweza kupata mimba kabla ya kuona siku zake,jibu ni NDIYO..kwa sababu kibaolaojia,mama anashika mimba kabla ya kuona her next MP..maana kuona MP kunatuonesha kwamba mama amefeli kushika mimba ktk kipindi ambacho alitakiwa kushika!
 
Vitu kama ivi lazima mama aulize kipindi anashauriwa kuchagua njia ya uzazi wa mpango kua endapo ataacha anaweza kupata mimba baada ya mda gani.

Kuna wengine wanapata mimba mapema tu wakiacha ila wengne wanaweza kuchelewa mpaka miezi 10 au mwaka ivi.

Note: Inazuiliwa kutumia njia za muda mfupi kama sindano au vidonge kwa muda mrefu, Ni vyema ukatumia njia za muda mrefu kama unapanga kuepuka mimba kwa muda mrefu.
 
Tatizo ni huu utitiri wa maduka ya dawa..akina mama wengi wanaona unafuu kwenda kwenye maduka kuchoma sindano badala ya kwenda hospitali/kliniki kuweka vipandikizi..sasa hiyo elimu sahihi ya uchaguzi wa njia bora ya uzazi wa mpango kwenye haya maduka ndio shida..
 
Kweli kabisa yani elimu inahitajika sana kabla hawajaanza kutumia ingepunguza sana hizi shida wanazopata.
 
Dawa za uzazi wa mpango ni hormones zilizowekwa kwenye vidonge, sindano na vipandikizi (vijiti) ili kuyafanya mayai ya mwanamke yasikue na yasikomae kabisa kuweza kurutubishwa, hivyo kusababisha mwanamke asipate ujauzito. Hivyo wanaweza kumeza, kuchomwa au kuwekewa hormones hizi. Lakini dawa hizi pamoja na kazi nzuri ya kuepusha mimba zina madhara makubwa yafuatayo ambayo yanaweza kutofaitiana kigogo sana katika kuleta madhara kati ya mwanamke na mwanamke. Yapo madhara yanayotokea papo kwa papo, muda wa kati na yapo yatakayotokea baada ya kuzitumia kwa muda mrefu. Madhara hayo kwa watumiaji ni kama yafuatayo:

1. Uke kuwa na majimaji mengi kuliko kawaida yake
2. Uke kulegea kuliko kawaida
3. Uke kuwa laini kuliko kawaida
4. Matiti kuwa makubwa na laini kuliko kawaida
5. Matiti kuwa na mabuja na kuuma kuliko kawaida
6. Kuongeza uwezekano wa Matiti, shingo ya uzazi na mji wa mimba kupata uvimbe na saratani
7. Kuvurugika kwa mzunguuko wa hedhi
8. Kusababisha ugumba/utasa kwa wanawake
9. Kuongezeka uzito wa mwanamama
10. Kushuka kwa kinga ya mwili
11. Kushambuliwa na fangasi mwilini na ukeni
12. Kupanda kwa shinikizo la damu
13. Kushusha blood pressure kwa wengine
14. Kusababisha damu itembee polepole (varicose vein)
15. kuumwa kichwa (migraine)
16. Kichefuchefu
17. kutapika
18. Kuongezeka kiasi cha hedhi na kusababisha upungufu wa damu (anemia)
19. Kukonda kwa baadhi ya wanawake
20. Kuongeza uwezekano wa kuugua kisukari
21. Kupata mimba, unaweza pia kupata ujauzito ingawa unatumia dawa za uzazi wa mpango.
22. Kupata stroke

Hivyo, uwamuzi ni wako wewe mwenyewe kuzitumia au kuachana nazo. Hata hivyo ziko njia nyingine mbali na hormones hizi ambazo watu wanaweza kutumia kupanga uzazi ambazo ni pamoja na:

1. Kuacha ngono (abstinence)
2. Kutumia kondom
3. Kupumia kitanzi (kuwekewa chuma ukeni)- loop
4. Kunyonyesha watoto (exclusively)
5. Kukata mirija ya uzazi ya mwanaume (vasectomy)
6. Kukata mirija ya uzazi ya mwanamke (BTL)
7. Kung'oa/kuondoa kabisa kizazi cha mama (Hysterectomy )
8. Kutolea mbegu (kukojolea) nje wakati wa kujamia (withdrawal)
 
3a346fcab68be8f3e8c0f6619247c538.jpg

Kwa niaba ya mwenye kiti

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
hapo kwenye dawa za uzazi wa mpango kwa kumeza hapo mm ninavyoelewa ni kuwa kam ulivyosema dawa zote hizo ni hormones ss kama ni hormones na tunavyojua ni kuw hormones ni protein in nature na zikipita kwa alimentary canal lazima zimeng'enywe kwenye tumbo la chakula kutokana na gastric juice iliyopo hapo na kisha itavunjwa vunjwa hadi kuisha kabisa na kugeuzwa source ya nguvu (energy in form of ATP) mm ninavyoelewa ndiyo hivyo .ss kwa mujibu wa maelezo yako hapo kwenye kumeza hapo inakuwaje kuwaje na hizo ni hormones????
 
Zikalishaa mengenywa kwa hiyo amna absorbtion yoyote

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
sijui njia ipi inafaa bila kondomu utamu haupo tunabaki njia panda tu ukisema upige ukojoe nje inang'ang'ania shida tupu haka kamchezo
 
sijui njia ipi inafaa bila kondomu utamu haupo tunabaki njia panda tu ukisema upige ukojoe nje inang'ang'ania shida tupu haka kamchezo
Nimekupa elimu hii ili upunguze maswali na uokoe muda wakati wa kuchagua njia sahihi kwako ufikapo pale kwenye kituo kinachoshughulika na utoaji elimu ya uzazi wa mpango. Hata hivyo kama wewe unajijua kabisa kuwa wewe mwenyewe au kwenye ukoo wako kuna historia ya kuwa na shida ya pressure kupanda au kushuka, uzito wako ni mkubwa sana, una uvimbe kwenye kizazi, matiti au sehemu yoyote, una shida ya kisukari, kuumwa kichwa, HIV, TB, saratani au shida ya ini tafadhali usichague njia hizi za hormones
 
hapo kwenye dawa za uzazi wa mpango kwa kumeza hapo mm ninavyoelewa ni kuwa kam ulivyosema dawa zote hizo ni hormones ss kama ni hormones na tunavyojua ni kuw hormones ni protein in nature na zikipita kwa alimentary canal lazima zimeng'enywe kwenye tumbo la chakula kutokana na gastric juice iliyopo hapo na kisha itavunjwa vunjwa hadi kuisha kabisa na kugeuzwa source ya nguvu (energy in form of ATP) mm ninavyoelewa ndiyo hivyo .ss kwa mujibu wa maelezo yako hapo kwenye kumeza hapo inakuwaje kuwaje na hizo ni hormones????

Hahaha..
Demand jibu mkuu!
 
Back
Top Bottom