Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

njia gani ya kienyeji!!!!!na njia hiyo ni kwa ajili ya nini

Njia za kienyeji/asili ni njia ya kunyonyesha,hii inawafaa akina mama ambao wanapokuwa wananyonyesha huwa hawapati siku zao,njia nyingine ni kalenda,hata hivyo hakuna njia yeyote iwe ya kisasa au ya asili inayoweza kuzuia mimba 100%.
pamoja na hivyo njia za asili zinabaki kuwa chaguo bora zaidi.
 
Kimsingi hakuna njia izuiayo mimba kwa 100%, mbaya zaidi njia ya madawa huwa inapelekea mabadiliko ya ghafla ya vichocheo au pindi mtumiaji anapoacha basi utakuta hata utaratibu wa mzunguko wake umebadilika...

Hakuna cha kufanya zaidi ya kulea mimba na kutarajia mtoto mwingine Mungu akijaalia...
 
Pole kaka, hyo mimba nyie muilee tu vzr no way na huyo mtt aachishwe nyonyo then muwe mnamtengenezea unga wa lishe, changanya nafaka zifuatazo; mchele, soya, mahindi bisi, ulezi, uwele, mtama mweupe, karanga, ufuta na ngano,. nenda sokoni kanunue hvo vtu kila variety robo kilo then osha vizuri uanike ukauke, karanga na soya ukaan then ukasage afu uwe unamkorogea uji kla cku afu ukoroge kwa maziwa ni vzr ukapata maziwa ya ngombe wa kienyeji. huyo bibie akijifungua salama aenda hosp sasa ajaribu kuwekewa vpandikizi vitamsaidia kupanga uzazi,.
 
Ndio imeshatokea hivyo, inabidi mkubali hali halisi.

Leeni mimba na dogo ale vizuri maisha yaendelee. Sidhani kama kuna madhara yoyote yale zaidi ya kuangalia afya ya mama iwapo mara ya mwisho alijifungua kwa operesheni.

majibu yako Lizzy yanajitosheleza.
 
Last edited by a moderator:
Habarini za asubuhi waungwana,.
Kwanza napenda kuwapa pole na shughuli na mihangaiko ya siku, naomba msaada wa ushauri nipo katika wakati mgumu sana. Mke wangu amejifungua mtoto mwaka jana mwezi wa sita, sasa hv mtoto wetu huyu wa pili ana mwaka mmoja na miezi 2.
Kwa kipindi chote tangu alipojifungua tumekuwa tukitumia njia ya uzazi wa mpango kwa kutumia vidonge vya majira, sasa mwezi wa saba mwaka huu tulishauriana abadili njia nyingine kutokana na hali aliyokuwa anajisikia iliyokuwa inasababishwa na vidonge. Tuliamua kutumia njia ya sindano, alikwenda hospitali ya Wilaya wakampa hiyo huduma. sasa mwezi huo wa saba umepita bila kuona siku zake.Jana baada ya kuona muda umepita sana akaamua kwenda kupima ujauzito, majibu yakawa yupo Positive. sasa naomba ushauri wenu ikiachwa hii haiwezi kuwa na madhara kwa mtoto ambaye bado ananyonya? Msada nini kifanyike.

Pole sana Mkuu!
Pole tena kwa kutumia njia za kizamani, however hizo njia zinatolewa hadi leo ktk hospitali zetu (nadhani ziko kiuchumi zaidi!)
NJIA SALAMA, YA KISASA NA RAHISI NI KUTUMIA CALENDER!
Ni mzuri sana:
1-unakula mbuye halisi (Ndom, sindano na madonge huondoa uhalisia)!
2-unajiamini!
3-kwa uwezo wa Mungu, unaweza hata kupanga kama unataka mtoto wa kiume au wa kike!
 
HILI NALO NI JANGA LA KITAIFA!
basi tu watu hatukubali ukweli!
 
Ndio imeshatokea hivyo, inabidi mkubali hali halisi.

Leeni mimba na dogo ale vizuri maisha yaendelee. Sidhani kama kuna madhara yoyote yale zaidi ya kuangalia afya ya mama iwapo mara ya mwisho alijifungua kwa operesheni.

eeeehhh bi dada mzima lakini nilikumicje karibu tena
 
kuna mila zilikuwa haziruhusi mama akipataja ujauzito kunyonyesha ilisemekana mtoto anapata maziwa yasio mazuri na kuzorotesha afya ya mtoto anayenyonya sina uhakikika kitaalam sijui labda MziziMkavu Riwa watafafanua ......njia nzuri isiyokuwa na madhara 100% kalenda
 
Last edited by a moderator:
Kuna njia1 inaitwa COETUS WITHDRAWING,yaan kupizia nje!(yataka moyo maana kunakuaga na kausumaku flan ivi wazungu wakpga hod!)
 
Usitoe hiyo mimba kwani huyo ni mtoto wako. Mpe mama lishe ya kutosha, na kama unaogopa kunyonyesha zaidi basi mpe mtoto maziwa ya ng'ombe na vyakula vyenye lishe. Mtoto wa zaidi ya mwaka hawezi sumbua sana.
 
Mkuu.@Kinyengel Fuata ushauri wa mkuu.@Junior Mselle ushauri wake ni mzuri utaweza kukusaidia.

JINSI YA KUZUIA MIMBA KWA NJIA ZA ASILI.


Njia ya asili ya kuzuia mimba ni mbinu pekee ambayo wanamama wa miaka ile kabla ya madawa ya kisasa(kizungu) kugunduliwa.

Njia hii inauhakika wa asilimia 96-mpaka 98 kama zilivyo njia nyingine za kuzuia mimba kama vile vidonge, sindano, patch, Coil.

Njia nyingine asilia ni kumwaga nje (withdrawn), lakini hii unahitaji zaidi ushirikaino wa mpenzi wako, mawasiliano wakati wa tendo kwani akijisahau au kuchelewa ujue kitu na box.




Mipira (Condoms) ndio kinga pekee inayozuia mimba na magonjwa yote ya ngono kwa asilimia 99 na ile moja iliyobaki ni kwa ajili ya sababu za kisheria kulinda Makampuni incase mtu akatumia vibaya na kushika mimba au gonjwa la zinaa. Vilevile Kinga hii (Condom) ndio pekee ambayo ham-badilishi mwanamke kihomono au kimaumbile.

Njia ya asili ya kuzuia mimba hutumiwa na wanawake ambao kwa namna moja au nyingine hawataki kutumia madawa ya kisasa ili kuepuka mabadiliko ya miili yao kama vile kunenepa, kutokwa na majimaji ukeni na pia kuna tetesi kuwa yanaongeza uwezekano kwa mwanamke kupata Saratani ya Kizazi na Matiti.

Kuzuia mimba kwa kutumia tarehe inauhakika ikiwa mzunguuko wako ni uleule na sio mrefu (siku 32-35) wala mfupi (siku 18-24) bali ni ule wa kawaida ambao ni siku 28.

Ili kutumia mtindo/mbinu hii ya kuzuia mimba unapaswa kuanza kuhesabu siku zako sasa na fuatilia kwa karibu mzunguuko wako na kuhakikisha kuwa una siku 28 sio chini wala juu ya hapo.

Kwa kawaida unaaza akufuatilia kwa miezi mitatu hadi sita (kama umewahi kutumia madawa ya kuzuia mimba) kabla hujaanza kuitumia njia hii.



Namna ya kuhesabu
Ili kuwa na uhakika na urefu au ufupi wa mzunguuko wako unapaswa kuhesabu siku ya kwanza utakayo ona damu mpaka utakapo ona damu ya mwezi utakao fuata.

Mfn; leo tarehe 9 mwezi wa nane ndio umeanza hedhi basi hedhi ya mwezi ujao itakuwa tarehe 7 mwezi wa tisa.....hii ni kama mzunguuko wako usiobadilika (sio mrefu au mfupi) ambao ni siku ishirini na nane tu.

Siku ya kwanza ya hedhi mpaka siku ya tisa ni salama nahuwezi kushika mimba.

Baada ya hapo mpaka siku ya kumi na nne (yai linapevuka)unakuwa hatarini.

Siku ya kumi na saba mpaka siku ya ishirini na mbiliunakuwa salama tena mpaka siku ya ishirini na tatu mpakaishirini na saba (yai pevu linashuka) hatarini

Lakini ile ya ishirini na nane siku ya hedhi nyingine unakuwa salama tena......

Ili kuwa na uhakika kuwa uko kwenye mstari kuliko kuegemea kwenye tarehe tu unatakiwa kujua mabadiliko ya mwili wako.

Unapokuwa hatarini kushika mimba mara nyingi utahisi nyege zaidi n avilevile utoko wako utabadilika na kuwa mlaini zaidi (kama lotion) na wakati mwingine utahisi ute unatoka (ule kama udenda/mlenda)....ukiona hivyo hakikisha unatumia Condom vinginevyo utashika mimba.


Unapokuwa salama mara nyingi hamu ya kungonoka inakuwa haipo sana unless "uchokozwe", vilevile utoko wako unakuwa mzito (kama cream/mafuta mazito)na mweupe sana yaani hata wakati wa kujiswafi inakuwa taabu na inaweza kukuchukua muda mrefu zaidi.

Hali ikiwa hivi ujue uko salama kusex bila kinga ya kuzuia mimba.
 
Mbona hamna madhara hapo mwana!!! Hao watoto watakuwa wanepishana kwa almost two years..., kitu ambacho ni kawaida sana kwa familia za kitanzania...
 
Mke wangu ana mtoto mdogo, ili kupanga uzazi tuliamua kwa pamoja kufuata njia za kisasa za uzazi wa mpango.
Tulianza kwa mke wangu kutumia vidonge baadae akaanza kuchoma sindano, sasa tangia achome sindano ya kwanza amepitisha siku zake kwa kiwango ambacho tuna wasiwasi isije ikawa ni mimba.
Tunaomba wazoefu mtutoe wasiwasi je ni kweli mwanamke akichoma sindano hizi za majira anaweza kutoona siku zake? Na ni kwa kipindi gani?
Saidia mimi kufahamu hili waungwana.
 
Back
Top Bottom