Habarini za asubuhi waungwana,.
Kwanza napenda kuwapa pole na shughuli na mihangaiko ya siku, naomba msaada wa ushauri nipo katika wakati mgumu sana. Mke wangu amejifungua mtoto mwaka jana mwezi wa sita, sasa hv mtoto wetu huyu wa pili ana mwaka mmoja na miezi 2.
Kwa kipindi chote tangu alipojifungua tumekuwa tukitumia njia ya uzazi wa mpango kwa kutumia vidonge vya majira, sasa mwezi wa saba mwaka huu tulishauriana abadili njia nyingine kutokana na hali aliyokuwa anajisikia iliyokuwa inasababishwa na vidonge. Tuliamua kutumia njia ya sindano, alikwenda hospitali ya Wilaya wakampa hiyo huduma. sasa mwezi huo wa saba umepita bila kuona siku zake.Jana baada ya kuona muda umepita sana akaamua kwenda kupima ujauzito, majibu yakawa yupo Positive. sasa naomba ushauri wenu ikiachwa hii haiwezi kuwa na madhara kwa mtoto ambaye bado ananyonya? Msada nini kifanyike.