Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

hizo ni dalili za kukimbia majukumu. ndo maana ya kuoana,fanya uumbaji bana lol!
 
Ingefaa urudi hospt huko alikopewa dawa hizo watakua na ushauri mzuri na kama utahitaji kuelimishwa watakusaidia tu. Hii ndio shida hutokea mara nyingi hasa wanandoa wanapoacha kuongozana pamoja kwenye huduma za uzazi wa mpango. Mkuu kama nilivyosema nenda ktk kituo cha afya ukatoe duku duku lako.
 
je alishaanza kupata siku zake kabla hajaanza kutumia vidonge au siku zilikuja baada ya kuanza hizo pills. experience ni kwamba pills huwa zinasababisha period kuanza hata kama wakati wake ulikuwa bado (kuna wanawake wakijifungua hawapati hedhi mpaka wamalize kunyonyesha, na hii ni one of the natural ways za kupanga uzazi). wasiwasi wangu ni kwamba isije kuwa pills zilileta hedhi then baada ya kuacha kuzitumia zikapotea tena. sifahamu kuhusu sindano, ila pills zina-interfere mfumo wa hedhi ndio maana mtu akiacha kuinywa siku moja tu anaweza kuconceive siku hiyomhiyo. ila kama unahisi atakuwa na ujauzito, nunueni kipima mimba ili kuondoa wasiwasi wenu. pia ni vizuri mrudi kwa wataalamu wa uzazi wa mpango kwa ushauri zaidi
 
Nenda hospital mkapime na kupota ushauri zaidi kwani wakati mwingine ufanyaji kazi wa vitu hivyo unategemea maumbile ya cells za mtu mwenyewe. aidha wakati mwingine unapobadili njia mojawapo bila kupata ushauri huwa inaleta usumbufu huo na kuchelewa kupata siku zake si ishara ya kuwa na mimba kwani wengine wanaweza kumaliza hata miezi sita bila kuingia kwenye siku zao.
 
je alishaanza kupata siku zake kabla hajaanza kutumia vidonge au siku zilikuja baada ya kuanza hizo pills. experience ni kwamba pills huwa zinasababisha period kuanza hata kama wakati wake ulikuwa bado (kuna wanawake wakijifungua hawapati hedhi mpaka wamalize kunyonyesha, na hii ni one of the natural ways za kupanga uzazi). wasiwasi wangu ni kwamba isije kuwa pills zilileta hedhi then baada ya kuacha kuzitumia zikapotea tena. sifahamu kuhusu sindano, ila pills zina-interfere mfumo wa hedhi ndio maana mtu akiacha kuinywa siku moja tu anaweza kuconceive siku hiyomhiyo. ila kama unahisi atakuwa na ujauzito, nunueni kipima mimba ili kuondoa wasiwasi wenu. pia ni vizuri mrudi kwa wataalamu wa uzazi wa mpango kwa ushauri zaidi

Alianza kupata siku zake mara baa ya miezi kadhaa ya kujifungua, mtoto sasa ana miezi nane na mwanzoni tulitumia vidonge kwa miezi mitatu ya mwanzo wa kutumia, kisha baada ya miezi mitatu kupita tumeanza sindano.
Hizi sasa ndio zimeleta wasiwasi kwa kweli maana haijawahi period kupita kwa wiki zaidi ya mbili hapo kabla!

Lakini pia mke wangu hahisi dalili za mimba kama vile kichefuchefu au zingine za kawaida zaidi ya hili la kutoona siku zake!
 
Uo si izazi wa mpango ndugu yangu ni kuumizana na kutiana ubovu....ebu jiulize kwann nazuia mimba? Ni sawa na yule anaesema mi siolewi mpl nimalize master...
 
Habari thezila..
Sidano za uzazi wa mpango zinasababisha kupata siku unregulary(mara kwa mara) na hatimae usipate kabisa siku zako,kwahio usiwe na hofu juu ya hilo,hio ni mojawapo ya side effect ya hizo dawa...
 
Hilo ni jambo la kawaida kama unatumia sindazo za uzazi wa mpango.Nakushauri acha endapo utaendelela hutozaa kabisaaaaaaa,na unahatari ya kupata kansa,nashauru utumie kalenda ya kawaida.Nenda haraka kamuone dokta
 
Habari yako shamali,
Kuna njia tofauti za uzazi wa mpango ambazo unaweza kuzifata kutokana na matakwa yako
Njia ambayo hutumika na wengi ni ya KALENDA,na kwa njia hii unahesabu siku zako ni muhimu ujue una mzunguko wa siku ngapi ili kuweza kuheshabu siku ipi upo hatarini(unaweza kubeba ujauzito) na siku ipi upo salama.
Njia nyingenezo ni:
  • HORMONSPIRAL:Kwenye picha ya kizazi unaona spiral ipo kwenye mfuko wa uzazi hii inadumu kwa miaka 5.
  • hormonspiral.gif
  • VAGINAL RING ina umbo la mduara na muonekano wa mviringo,hii huwekwa nje ya kizazi.h9991285_001.jpg
  • BIRTHCONTROL PILLS:Vidonge vya uzazi wa mpango,vipo vya aina tofauti vyenye homoni moja tu nayo ni gestagen au mchanganyiko wa gestagen na estrogen
  • Kuna PLASTER ambazo unaweza kutumia,Hizi plaster zina mchanganyiko wa homoni mbili gestagen na estrogen.Unaiweka kwenye eneo la ngozi safi siku ya kwanza unapopata siku zako,unabadili baada ya siku 7,unabadili tena siku ya 15,kisha unachukua mapumziko ya siku 7(kwa wale wenye mzunguko wa siku 22-28)
  • SINDANO ambayo inachomwa kila baada ya miezi mitatu
  • IMPLANTANT:Ni kijiti ambacho unaweka chini ya ngozi ya mkono kwa ndani,hiki hudumu kwa miaka 3 au 5,kutokana na chaguo lako.
  • p-stav_implantat_656162c.jpg
 
Habari wana jf doctor,mimi na mke wangu tumeamua kutumia njia ya uzazi wa mpango ya asili ya kutumia mbegu za nyonyo,naombeni msaada wenu kwa anaejua namna ya kutumia mbegu hizi kuzuia ujauzito.
 
Kwanza namshukuru Mungu kwa kunijalia mtoto wa kike ambaye leo ametimiza miezi mitano nasema asante Mwenyenzi Mungu..ushauri ninahitaji kutokana ni kujua kama sindano za uzazi wa mpango zina madhara gani kwa mwanamke?naomba kuwasilisha kwa wana jf.
 
sindano madhara yake ingawa sio kwa wote unaweza usipate period kwa muda mrefu,wengine inawasababishia heavy period,na wengine ukitaka mtoto wa 2 unaweza kukaa hata miaka 10 usipate ujauzito wa 2.ushauri wangu usitumie.au kama ukitumia tumia kwa muda mfupi tu,maybe mwaka and then acha
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kati ya wanawake wengi niliokutana nao wanaotumia haya mambo ya wazungu walopatwa na madhara ni wengi kuliko wasiopatwa na madhara. Just thinking louder: HIVI WAMAMA WA ZAMANI WALITUMIA NJIA GANI KUPANGA WATOTO? Kuna familia naifahamu wako 7 hawa jamaa (monogamy) wamepishana si chini ya miaka mitatu na last born ni wa 1988. Ina maana zamani kulikuwa na elimu ya kutosha kuhusu kupishanisha watoto kuliko siku hizi?
 
Karibu kila Dawa ina Pande Mbili Faida na Madhara/maudhi hivyo ni vizuri kabra ya Kuanza Kuitumia Ukapata Ushauri kwa Wataaram Husika !!
 
Familia moja kijiji fulani jirani zangu (majina yamehifadhiwa) juma lililopita waliamua kutumia njia za uzazi wa mpango kwa kufunga vizazi vyao (Mke na Mume). Walipofika Zahanati walikuwepo wataalam kutoka ngazi ya hospitali ya Mkoa walihojiwa kupata uhakika wao kuwa kweli wamekusudia kufunga uzazi kwa kukata mirija ya uzazi kwa njia ya upasuaji mdogo!

Ilipofika zamu, Mke alimwambia mume aanze! Mume baada ya kutoka kufanyiwa upasuaji zamu ya mkewe ilifika! Lakini chakushangaza Mke alikataa na akakimbia kuelekea nyumbani. Wahudumu walibaki wakishangaa! Jamani wanafamilia muwe wawazi katika kupanga mambo yenu.

Sasa hivi mume amekuwa mnyonge sana! Nawashauri ndg zangu ktk Jf maamuzi ya kufanya kitu ambacho kikemia twaweza kukiita Chemical change tusikurupuke!
 
Back
Top Bottom